Dar es Salaam ni mkoa uliojaa masikini wengi wanaojificha kwenye kivuli cha miundombinu tu

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Acha ukweli usemwe DSM ni mkoa wa kimaskini sana, kelele kibao lakini uhalisia ground maisha ni mabovu sana DSM, watu wana stress, maisha duni ndio mana DSM ni mkoa unaongoza katika idadi ya ufukara na vifo katika ngazi ya kaya ama familia.

Matajiri wachache wanaibeba DSM, ila watu wanateseka sana.

Watu wanaoishi DSM wanateseka sana na maisha. Ukiwa mtafutaji huwezi kukaa dsm mwezi mzima wakati maisha yako mwanza, Arusha, Iringa,Mbeya, Dodoma, Kahama.

DSM endeleeni kujifariji na starehe ya pombe na umalaya nje na hapo tokeni Maghettoni.

Watu wa DSM wengi hawana savings kwenye account zao maisha yao ni kauka nikuvae.

Ni hayo tu tukutane kwenye comments.

Benjamin Mkapa Stadium tarehe 20-10-2023 ntakuwa VIP B dadeki.

Za kichwa na mjegeje umejaa

Wadiz
 
Daah kuna kaukweli hapa! Njooni wana Dar es Salaam! Ila kusema kweli Dar kama hauwezi kupata fedha ya saving na baadae kuinvest hautakaa utoboe utabakia kuongea kiswahili kingi tu bila mafanikio mwaka nenda rudi!
 
Dar ndio sehemu pekee mtu anakuja kwa nauli ya kupewa na anaishi. Uko Dodoma kwenu nani aje vijijini Godegode, Kibakwe au Chololo bila connection na atoboe?

Dar mtu anakuja analala kwenye maboksi anaweka juhudi anapiga hatua kidogo kidogo. Mtu anaamka asubuhi hajui kazi ataipata wapi na atafanya nini ila ana uhakika wa kazi. Dar kila siku ni msimu, hakuna bidhaa utakosa hata iwe bei ghali. Nachingwea unapata maembe mwaka mzima? Sasa mtengeneza juisi Nachingwea kama hakuna msimu huwa anafanya nini vibarua au.

Labda kwa wafanyakazi wa serikali. Mwalimu wa Dar anaweza zidiwa na mwalimu wa Morogoro kama wote wana akili sawa za kujiongeza. Ila fundi ujenzi au mshona viatu sahau
 
Watu wanajifariji tuu, mimi kwa sasa sipo Dar, ila ukiongelea kwa ujumla dar ina advantage kubwa sana kwa mpambanaji.
 
Dar ndio sehemu pekee mtu anakuja kwa nauli ya kupewa na anaishi. Uko Dodoma kwenu nani aje vijijini Godegode, Kibakwe au Chololo bila connection na atoboe?

Dar mtu anakuja analala kwenye maboksi anaweka juhudi anapiga hatua kidogo kidogo. Mtu anaamka asubuhi hajui kazi ataipata wapi na atafanya nini ila ana uhakika wa kazi. Dar kila siku ni msimu, hakuna bidhaa utakosa hata iwe bei ghali. Nachingwea unapata maembe mwaka mzima? Sasa mtengeneza juisi Nachingwea kama hakuna msimu huwa anafanya nini vibarua au.

Labda kwa wafanyakazi wa serikali. Mwalimu wa Dar anaweza zidiwa na mwalimu wa Morogoro kama wote wana akili sawa za kujiongeza. Ila fundi ujenzi au mshona viatu sahau
Usiwadanganye watu hapa sie tupo Dar hapa hapa kikubwa kila mtu apamabane na hali yake hapo alipo! Ila kusema Dodoma au mkoani watu hawana maisha endelea kujidanganya! Nenda na zunguka Arusha,Mwanza au Kahama kama utarudi hapa kuandika ujinga tena!
 
Kaka Dar inaadvantage kwa mpambanaji sikatai ila kuwadanganya watu kwamba Dar ndo mkoa pekee watu wanatoboa wadanganye ambao hawajawahi kutembea! Tena miji kama Arusha,Njombe ,Kahama Mwanza na Dodoma ndo inafursa kubwa kwa watu wanaopambana kwa sasa! Dar chanagamoto kubwa ni gharama za kuanzisha mradi!
 
Daslama inawachengua sana wakuja, mbona mikoani watu ndio maskini sana ? Mkuu umetumia data gani ? Daslama mtu anaweza kuja hana hata mia na akawa tajiri, na hata watu ni wengi pia so hiyo inatosha kueleza kuwa kutakuwa na kitu tu kwanini watu wakimbilie dar ? Mkuu simba inayokupeleka vip B , kwanini isiwepo kantalamba huko ? Kila mkoa unamaskini mkuu, kila mtu ashinde match zake, maskin wengi yes ila na maboss wengi, ukitoka vip b nenda hata kule kama unaenda bahari beach kashangae utaacha kutukana watu hovyo hovyo mkuu…
 
Back
Top Bottom