Dar es Salaam ni mkoa uliojaa masikini wengi wanaojificha kwenye kivuli cha miundombinu tu

Wewe ukishaona sehemu inajengwa bila idhini ya ofisi za mipango miji wala kibali cha ujenzi kuhusika. Jua sehemu hiyo ni ya watu hohehahe.
 
Kwa nini na wewe unakaa DSM kwenye mji wa ufukara badala ya Kwenda kuishi kwenye hiyo miji ya utafutaji?
Watu wanaoishi DSM wanateseka sana na maisha. Ukiwa mtafutaji huwezi kukaa dsm mwezi mzima wakati maisha yako mwanza, Arusha, Iringa,Mbeya, Dodoma, Kahama.
 
Exposure ni kitu kikubwa sana Kuna ndugu mmoja yupo Finland ni mtanzania mwenzetu...

Katika kubadilishana mawazo aliwai tamka ukitumia fursa za hapa nyumbani unatoboa kirahisi sana mfano Finland huwezi amka asbuh ukakaanga maandazi au kuchoma chapati au kufungua mama lishe au babalishe bila kufuata utaratibu....ila bongo dar es salaam unajianzishia kiholela holela

Mambo ni mengi muda mchache
 
Dar kuna mzunguko mkubwa wa pesa

Kuna wale tumezaliwa Dar mpaka sasa tuko hapa na wale wamehamia hapa Dar kujitafuta na wengine wamejipata, lazima tutakubaliana;

Dar usipokuwa na kazi, biashara (mtaji), ujuzi au mishe yoyote ya kukuingizia kipato plus connection utaishi maisha ya kifukara sana

Na hata kama unaingiza kipato lakini ni kidogo utaishi maisha ya kimasikini pia kwa sababu ya gharama kubwa za maisha

Ukitaka uone ufukara, umasikini na ugumu wa maisha ya Dar nenda uswahilini. Watu wanatia hadi huruma ukiangalia mwonekano, makazi na mfumo wa maisha wanaoishi inasikitisha

Watu wa Dar tukubali kujifunza fursa haziko tu hapa hata nje ya Dar fursa zipo usikubali kuishi kinyonge eti kisa uko jiji kubwa

Kuna wadau wamepiga hatua kubwa kimaisha hapa Dar lakini maokoto wanayakusanyia mikoani
 
Ndiko tunakoelekea.Kwenye masuala ya usalama wa chakula huko Kwa Wenzetu wako very strict ila bongo ni Bora liende.

Pamoja na hivyo watu Bado hawana akili huko Dar kwenu.
 
Hiyo Hali ya umaskini ni zaidi ya nusu ya watu wa Dar.

Mkoani Kuna umaskini ila sio wa kukosa makazi au chakula Sasa hapo Dar ,kula na kulala Kwa watu wengi ni shida
 

Kwa pisi za kwenda dsm imeongoza.
 
Kabisa mkuu,

Kwenye usafiri ni kero tupu, Watu
wana jazwa na kushindiliwa kwenye Mwendokasi kama mapanya...
Wee hujui faida ya mwendokasi! Unataka kuniambia kabla ya mwendokasi watu walikuwa hawashindiliwi kwenye daladala? Bora ushindiliwe kwenye mwendokasi utumie dakika 45 kutoka kimara hadi feri kuliko ilivyokuwa kwenye daladala unashindiliwa alafu unatumia masaa 3 hadi 4 kufika!
 
Huu uzi una kila aina ya watu,waliokulia dsm wakatusulia dam,walio toka mkoani wakafanikiwa dsm,kuna waliokulia dsm ila hali tete wakaenda mkoani wakafanikiwa,na waliotoka mkoani wakaja dsm wakaangukia pua[emoji28].

Maisha ni popote pale unapopata maokoto,ila kwa fursa na harakati za kutosha dsm itabaki kuwa juu.
 
Hiyo Hali ya umaskini ni zaidi ya nusu ya watu wa Dar.

Mkoani Kuna umaskini ila sio wa kukosa makazi au chakula Sasa hapo Dar ,kula na kulala Kwa watu wengi ni shida
Nakubaliana nawe

Wengi hapa Dar kati ya milo mitatu ya siku kuna mmoja wanapiga pasi ndefu

Wadau wanasema Dar kupata mbususu ni rahisi ila ni ugumu wa maisha unafanya mabinti watoe nyuchi kwa pesa ndogo
 
Daah kuna kaukweli hapa! Njooni wana Dar es Salaam! Ila kusema kweli Dar kama hauwezi kupata fedha ya saving na baadae kuinvest hautakaa utoboe utabakia kuongea kiswahili kingi tu bila mafanikio mwaka nenda rudi!
Eti kiswahili kingi umenichekesha sana nikakumbuka misemo pendwa ya misheni town ya Dar kama ile ya"Mwanangu nitakucheki mida kuna mishe naifukuzia" na misemo mingine ile ya machawa kama"Kiongozi unayumba hausomeki siku hizi"[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
"Kuna mchongo nausikilizia"
 
Umewahi kufika wilaya ya bahi Dodoma au kongwa? Tema mate chini aisee
 
Umemaliza huu ndio ukweli.
Mwisho wa siku maisha ni popote inategemea akili yako na bahati.
Hakuna utofauti na watu waliozamia kwenda ulaya na nchi zingine ughaibuni wapo wanaotusua na wapo wanaoangukia pua.
 
siku hizi wanofuga kisasa,wanolima,wanaochimba madini kwa tija wote wanatoka mijini,wavijijini wanababaisha tu kidesturi
 
Nyie ongeeni ila dar uwezi kufananisha na mikoa mingine isee..
Ogopa sana mkoa unawatu milioni 6 na point na wote wanasurvive na kazi na vibarua vya hapa na pale..

sasa imagine new York huko hii miji mikubwa ni inamizunguko mikubwa sana ya hela kwahiyo ni rahisi kusurvive..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…