Dar es Salaam nzima haijawahi kutokea Baa yenye sifa na mvuto kama Kwa Macheni

Mkuu Extrovert tia neno. Maana kuna vijana wamekuja mjini baada ya Macheni kufa, ndio maana wanaifananisha na vijiBar vya uchochoroni.
Kwa macheni,kill time,Lego bar, travertine, diamond jubilee,Chaga bite,nandoz,steers,vijana club,silent inn,beach comber,mikadi bichi,mwee nimesahau nyingine
Those days time flies for real
 
Useme tu kwa wakati wako uliikuta hiyo bar ipo juu na kuvuma kila pembe ya nchi hadi nje ya mipaka yetu (kama ulivyodai mwenyewe) lakini hata huko nyuma kuna bar na kumbi nyingi za starehe zilizovuma sana na kuwa gumzo mfano kuna safari resort kule kimara,hunters club n.k acha ambazo leo hii hata alama hakuna tena kutokana labda kupita miundombinu mingine au kubadilishiwa matumizi.
Nihitimishe tu kwa kusema kila jambo lina wakati wake.
 
Kwa macheni,kill time,Lego bar, travertine, diamond jubilee,Chaga bite,nandoz,steers,vijana club,silent inn,beach comber,mikadi bichi,mwee nimesahau nyingine
Those days time flies for real
Dah enzi zetu kweli tulifaidi mkuu.
 
Mkuu nakubaliana na ww kwamba kila zama na kitabu chake. Najua kabla ya macheni au baada ya macheni bar kulikuwa na maeneo mengine yaliokuwa moto kweli kweli.

Ila ki ukweli hazikuwahi kufikia moto ule wa macheni. Macheni ilijulikana mijini na vijijini. Kuna watu hawakuwahi kufika lakini walikuwa wakiisikia huko walipo. Tofauti na maeneo mengine unakuta labda yanajulikana Dar tu lkn ukivuka nje ya mkoa hayajulikani na kama yanajulikana basi ni kwa uchache mno.
 
Macheni Bar. Dar nimekumbuka mbali sana. Nilijuwa sikosi pale kushuhudia muziki wa dansi. Zaidi ya mara mbili nashtukia tu saa kumi na mbiki hii hapa. Kweli kila kitabu na zama zake.
 
Macheni Bar. Dar nimekumbuka mbali sana. Nilijuwa sikosi pale kushuhudia muziki wa dansi. Zaidi ya mara mbili nashtukia tu saa kumi na mbiki hii hapa. Kweli kila kitabu na zama zake.
Yani hata zifunguliwe baa na sehemu zingine za starehe kama vile kitambaa cheupe, kitambaa cha kijani, blue nk kamwe hazitoweza kuifikia kwa Macheni.

Kuna watu walikuwa wanatoka Kenya, Uganda, Zambia, Congo, Burundi nk just kuja kula tu bata kwa Macheni na baada ya bata walirudi kwao mikono mitupu baada ya kumaliza kila kitu walichokuwa nacho mifukoni kwao. Unafanya mchezo na Macheni nini!!!
 
Hakuna kitakachodumu, enzi hizo kwa macheni ni macheni kweli.. Jina kubwa sana.
Mtu yoyote aliekuja Dar kutokea mikoani au nje ya nchi, akiondoka kurudi kwao bila kufika au hata kupita kupaona kwa Macheni, basi huyo hakuaminika kama alifika Dar. Yani ili uaminike wakati huo kama ulifika Dar basi ni lazima uwe na picha au simulizi mbili tatu za kwa Macheni ndo watu wakubali.
 
Na hapo macheni,inawekwa taarifa ya habari iliyorekodiwa kuwa ni saa 2kamili kumbe saa SITA usiku ,tukiwa tunakata kiu,we jamaa acha castle baridiii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…