Baa ya macheni ilianza kuyumba wakati serikali ilipoanza bomoa bomoa ya watu waliojenga katika hifadhi ya barabara. Bar ilikuwa nje ya hifadhi lakini maeneo ya kujidai kama vile watu kunywa, kuchoma nyama, kucheza mziki nk yalikuwa nje ambapo ndio ilipopita barabara. Kifupi lile lilikuwa eneo la nyumba tu za kawaida watu kuishi ambapo nje ndo ilikuwa barabara ya kawaida tu gari mbili tatu kupita. Sasa macheni alipofungua baa gari zikawa zinalazimika kuzunguka kupitia njia nyingine haswa mida ya usiku unakuta viti, meza na watu wametapakaa kila sehem ya barabara ile. So serikali ilipoanza upanuzi wa barabara kutokana na uhitaji wa watu ikabidi eneo zima lipitiwe. Ikawa hakuna tena sehem ya watu kujiachia kwa nafasi maana kwa ndani baa ilikuwa ndogo sana, na joto la bongo wengi walipenda kukaa nje.
Kuhusu Macheni yeye ashakufa. Alikufa na presha kutokana na kutokea matatizo makubwa kati ya yeye na mkewe.
Ila kuhusu kifo hapo Mungu na ndugu ndio wanaojua zaidi, maana kuna wengine wanaeema kafa kwa presha, wengine ukimwi na wengine wanasema kisukari. So siri ya kifo chake aijuae ni Mungu mwenyewe.