Dar es Salaam nzima haijawahi kutokea Baa yenye sifa na mvuto kama Kwa Macheni

Dar es Salaam nzima haijawahi kutokea Baa yenye sifa na mvuto kama Kwa Macheni

Hahahah, na enzi hizo...alooooh mlienjoy maisha...buku tu, je aftatu??

Kila zama na kitabu chake. Kipindi hicho mziki wa dansi upo juu, pedeshee kibao mitaa hiyo. Pesa ilikuwa na thamani kiasi kipindi hicho cha Mkapa. Ila Waya ulikuwa mkali sana dawa ARV zilikuwa bado wanazipata matajiri, ndio miaka hii mtu anakufa kilo mbili😁
 
ashura macheni.JPG
Wasiomfahamu huyu ndiyo Macheni na mkewe Ashura
 
Ila maisha haya, starehe hizi zimeumiza sana watu weengi..mm kuna bar zipo kigamboni, Ngamia..unalewa mpaka saa kumi na moja mnabebana kipombe mpaka nolasco, saa mbili asbh utahisi ni saa sita usiku watu nyomiii ni kubebaba tu, kusaka lodge.
Nolasco sijsibuka siku nyingi. Day moja nikiwa pale nitaku dm tugonge chiaz
 
Nimekunywa sana kwa Macheni, Magomeni na Kinondoni hakukua na miujiza wowote. Ni bar tu za Kiswahili
Mkuu hapa nimezungumzia zaidi umaarufu wa baa yenyewe. Sikatai kwamba kulikuwa na baa kali nyingi zaidi ya macheni ila hazikuwahi kujulikana kama ilivyojulikana macheni.

Nasema hivi kwa sababu nina ushahidi wa watu wengi wa nje kuifahamu baa ya macheni kuliko baa nyingine yoyote iliyokuwepo nchini.
 
Gridi
Pole sana.

Ningali kijana enzi hizo nilikwenda pale na demu fulani mzuri sana pamoja na mdogo wake wote walikuwa wazuri sana. Demu mwenyewe alikuwa ana biashara yake ya Insurance agency pamoja na clearing and forwarding. Tulivyokaa mezani badala ya kuconcentrate kwenye maongezi yetu yeye akawa anazunguka zunguka kwenye meza nyingine na mara akazua ugonvi na mwanamke mwingine kama vile wanagombania bwana mpaka mdogo wake akaniomba samahanai na kuniambia kuwa anaona aibu kwa jinsi dada yake anavyofanya. Demu akawa anatamba kuwa "...bwana mwenyewe wengine tulishachezea sana!". Nikashtuka, baada ya kinywaji nikamrudisha nyumbani kwake kule Victoria mambo yakaishia hapo. Baada ya miezi sita nikakutana na mdogo wake akaniambia kuwa demu huyo aliugua ukimwi akafariki ghafla sana; akanipeleka kunionyesha kaburi lake pale Kinondoni Makaburini..
Gridi ya taifa ya pale ilikuwa ni 🔥...Mudy traffic 🚦 yeye alisurvive miaka miwili tukaenda kumzika Lushoto 😢
 
Macheni bar, macheni dangulo daah enzi hizo watu walikuwa na mbumba hatari
Nimeingia jijini siku nyingi sana lakini Kwa Macheni sikubahatika kunywa. Nilikuwa napita asubuhi asubuhi nakuta watu ndiyo wanafunga funga. Nakubaliana na wewe ilivuma sana hasa ukizingatia kipindi hicho hakukuwa na bar kubwa nyingi kama sasa.
 
Kama gridi ya taifa ya Chipukizi na Kahumba Morogoro ilinikosa+ basi hata ya kwa macheni isingenipata
Makabuli mengi ya kinondoni ni zao la macheni.
Ukimwi ulikua nje nje pale hauepukiki. Njemba za posta , check bob wanaotafuta njia za storoway, pass na visa , madini, pale ndio palikia penywe. Awe waziri wa ardhi, awe waziri wa sijui wanyama pori enzi hizo unawkuta pale.
 
WAtu wamekula sana udongo kwa macheni, inavyoonekana...bora sikua town..ningekua na mm, ni mmojawapo tu labda rehema za Mungu
Kipindi hicho maambukizi ya ukimwi yalikuwa yako juu sana halafu watu walikuwa hawajaujulia kama sasa. Hata hizi dawa za kurefusha maisha hazikuwepo hivyo kila aliyeugua alifariki.
 
Hahahhaa mkuu, karibu sanaaa panawaka sanaa walihama Greal Lonasco ya zamanii..ni maisha mpaka meneja wa bar kama ile anakujua, ujana huu acha tu niende zangu 40's..miaka 9 nisogee humo nafikiri fujo zitapungua..
Mm nilikuwa nafanya fujo zangu nolasko ile ya mikadi then alipohamishia pale mjimwema. Sasa hivi napaona pale papya grand nolasko kwa mbali tu nikipitaga kwenda saiti, ila napaona pana bamba sana. Fujo nimepunguza sana kwa kweli.

Maana kipindi changu miaka ya 2013 ilikuwa nolasko mwenyewe ndio anadhamini show kama sina cash na makaunta woote wananielewa hahaa.
 
Mm nilikuwa nafanya fujo zangu nolasko ile ya mikadi then alipohamishia pale mjimwema. Sasa hivi napaona pale papya grand nolasko kwa mbali tu nikipitaga kwenda saiti, ila napaona pana bamba sana. Fujo nimepunguza sana kwa kweli.

Maana kipindi changu miaka ya 2013 ilikuwa nolasko mwenyewe ndio anadhamini show kama sina cash na makaunta woote wananielewa hahaa.
Naijua nolasco ya mikadi vyema, nimefika pale mara kadhaa kupiga vyombooo kisha Naenda Ngamiaa, namalizia Grand Nolasco..

Kila kitu kina muda wake, na ndio maisha yanapata maana...muda mwngne unasema mm nilikua nakesha bar, unacheeka tu.

Umri, Majukumu, muda mwngne unachoka tu kuhangaika usiku kwenye mabar.
 
Mm nilikuwa nafanya fujo zangu nolasko ile ya mikadi then alipohamishia pale mjimwema. Sasa hivi napaona pale papya grand nolasko kwa mbali tu nikipitaga kwenda saiti, ila napaona pana bamba sana. Fujo nimepunguza sana kwa kweli.

Maana kipindi changu miaka ya 2013 ilikuwa nolasko mwenyewe ndio anadhamini show kama sina cash na makaunta woote wananielewa hahaa.
2013, tupo chuo wengine...hahaha
 
Habari zenu wana JF wenzangu.

Hivi ni Bar au maeneo gani ya starehe yanaweza kufikia sifa ilizokuwa nazo Bar ya Macheni enzi zake.

Hii Bar enzi za Prime Time yake iliweza kujibebea umaarufu hadi nje ya mipaka ya nchi yetu achilia mbali maeneo na mikoa mbali mbali ya Tanzania.

Mwaka 2003 wakati nipo ndani ya basi kutoka Lusaka kuelekea Harare nilikutana na mzambia fulani ambae tuliongea mengi kati ya tulioongea nilishangaa kuona jamaa aliifahamu hadi macheni Baa na alisema kwamba siku atakayofanikiwa kukanyaga Tanzania atajitahidi kufika katika Bar hiyo ili kujionea mwenyewe kwa macho yake yale yote aliyokuwa anahadithiwa na wazambia wenzake waliobahatika kukanyaga Dar na kwenda kula bata katika Bar hiyo.

Lakini pia nishakutana na watu kutoka katika nchi zingine za Congo, Burundi, Namibia na Kenya wakiizungumzia Bar hiyo kwa jinsi ilivyokuwa na mvuto kwa watu mbali mbali kutoka mataifa mbali mbali.

Sasa toka Bar hiyo ya macheni ilipoanguka sijawahi kusikia Bar zingine zenye sifa kubwa kama hiyo.

Je wewe ushawahi kuisikia nyingine yenye sifa zinazofanana na zile zile za kwa macheni? Kama ipo ni ipi? Najua kuna Bar na maeneo mengi yenye sifa na mvuto wa kiwango fulani ila sio kufikia viwango vya Bar ya Macheni.

Nyinyi au wewe unaonaje?

Karibuni tujadili.
Tunafikiria vya maana
 
Back
Top Bottom