Dar es Salaam nzima haijawahi kutokea Baa yenye sifa na mvuto kama Kwa Macheni

Hahahah, na enzi hizo...alooooh mlienjoy maisha...buku tu, je aftatu??

Kila zama na kitabu chake. Kipindi hicho mziki wa dansi upo juu, pedeshee kibao mitaa hiyo. Pesa ilikuwa na thamani kiasi kipindi hicho cha Mkapa. Ila Waya ulikuwa mkali sana dawa ARV zilikuwa bado wanazipata matajiri, ndio miaka hii mtu anakufa kilo mbili😁
 
Ila maisha haya, starehe hizi zimeumiza sana watu weengi..mm kuna bar zipo kigamboni, Ngamia..unalewa mpaka saa kumi na moja mnabebana kipombe mpaka nolasco, saa mbili asbh utahisi ni saa sita usiku watu nyomiii ni kubebaba tu, kusaka lodge.
Nolasco sijsibuka siku nyingi. Day moja nikiwa pale nitaku dm tugonge chiaz
 
Nimekunywa sana kwa Macheni, Magomeni na Kinondoni hakukua na miujiza wowote. Ni bar tu za Kiswahili
Mkuu hapa nimezungumzia zaidi umaarufu wa baa yenyewe. Sikatai kwamba kulikuwa na baa kali nyingi zaidi ya macheni ila hazikuwahi kujulikana kama ilivyojulikana macheni.

Nasema hivi kwa sababu nina ushahidi wa watu wengi wa nje kuifahamu baa ya macheni kuliko baa nyingine yoyote iliyokuwepo nchini.
 
Gridi Gridi ya taifa ya pale ilikuwa ni 🔥...Mudy traffic 🚦 yeye alisurvive miaka miwili tukaenda kumzika Lushoto 😢
 
Macheni bar, macheni dangulo daah enzi hizo watu walikuwa na mbumba hatari
Nimeingia jijini siku nyingi sana lakini Kwa Macheni sikubahatika kunywa. Nilikuwa napita asubuhi asubuhi nakuta watu ndiyo wanafunga funga. Nakubaliana na wewe ilivuma sana hasa ukizingatia kipindi hicho hakukuwa na bar kubwa nyingi kama sasa.
 
Kama gridi ya taifa ya Chipukizi na Kahumba Morogoro ilinikosa+ basi hata ya kwa macheni isingenipata
Makabuli mengi ya kinondoni ni zao la macheni.
Ukimwi ulikua nje nje pale hauepukiki. Njemba za posta , check bob wanaotafuta njia za storoway, pass na visa , madini, pale ndio palikia penywe. Awe waziri wa ardhi, awe waziri wa sijui wanyama pori enzi hizo unawkuta pale.
 
WAtu wamekula sana udongo kwa macheni, inavyoonekana...bora sikua town..ningekua na mm, ni mmojawapo tu labda rehema za Mungu
Kipindi hicho maambukizi ya ukimwi yalikuwa yako juu sana halafu watu walikuwa hawajaujulia kama sasa. Hata hizi dawa za kurefusha maisha hazikuwepo hivyo kila aliyeugua alifariki.
 
Hahahhaa mkuu, karibu sanaaa panawaka sanaa walihama Greal Lonasco ya zamanii..ni maisha mpaka meneja wa bar kama ile anakujua, ujana huu acha tu niende zangu 40's..miaka 9 nisogee humo nafikiri fujo zitapungua..
Mm nilikuwa nafanya fujo zangu nolasko ile ya mikadi then alipohamishia pale mjimwema. Sasa hivi napaona pale papya grand nolasko kwa mbali tu nikipitaga kwenda saiti, ila napaona pana bamba sana. Fujo nimepunguza sana kwa kweli.

Maana kipindi changu miaka ya 2013 ilikuwa nolasko mwenyewe ndio anadhamini show kama sina cash na makaunta woote wananielewa hahaa.
 
Naijua nolasco ya mikadi vyema, nimefika pale mara kadhaa kupiga vyombooo kisha Naenda Ngamiaa, namalizia Grand Nolasco..

Kila kitu kina muda wake, na ndio maisha yanapata maana...muda mwngne unasema mm nilikua nakesha bar, unacheeka tu.

Umri, Majukumu, muda mwngne unachoka tu kuhangaika usiku kwenye mabar.
 
2013, tupo chuo wengine...hahaha
 
Tunafikiria vya maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…