zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Wakti namsikiliza Mheshimiwa mgeni wetu adhyim, Rais wa Muungano wa Mataifa ya Kimerekani (USA), Barack Hussein Obama, nilimsikia alipoitaja Dar Es Salaam, aliitafsiri kuwa ni "Habour of Peace" (labda iwe ung'eng'e ulinipiga chenga). Mheshimiwa kama ulitafsiriwa hivyo, wamekosea watafsiri wako, kama ni wewe mwenyewe, kwani naelewa kuwa unakijuwa Kiswahili kwa kiasi fulani, basi umekosea.
Maana halisi ya Dar Es Salaam, ni ngumu sana kuitafsiri ikiwa huupendi Uislaam na umeaminishwa na wabaguzi wa ujinga, kwani Dar Es Salaam inapatikana ndani ya Qur'an ikimaanisha ni moja kati ya pepo au kwa maulamaa wengine, moja kati ya milango ya kuingilia peponi "Baab Dar as Salaam", kwa maana moja au nyingine inamaanisha "haven of Peace" au "Nyumba" ya amani au kwa maana halisi "Pepo" ya amani.
Aliyekufunda kuwa Dar Es Salaam ni "Habour of Peace" hakukutendea haki wewe wala hakututendea haki sisi wa Dar Es Salaam.
Kwa kusherehesha; Dar Es Salaam si jina geni kwa miji ya duniani na haikuanzia hapa kwetu, kuna nchi nyingi ambazo zina majina ya majiji au miji iitwayo hivyo kwa lafdhi tofauti, maarufu ni Jerusalem, ina maanisha hivyo-hivyo. Nyingine ni Darussalaam, iliyopo Brunei, Ni hiyo hiyo, kama yetu tu.
Mnhhh mnhhh!
Karibu mgeni wetu.