Tetesi: Dar es Salaam SGR Terminus kupewa jina la Rais Samia

Habari zenu wana JF wenzangu,

Hizi ni tetesi kutoka kwa mtu wa ndani ya kitengo fulani, ambapo amesema mpango huo wa kuipa Terminus hiyo jina la raisi Samia utafanyika siku ya ufunguzi wa safari za train hizo zinazotumia umeme.

Mdau huyo amesema kwamba lengo kuu la kuipa Terminus hiyo kubwa, nzuri na yenye kuvutia kuliko Terminus yoyote barabarani Africa ukiondoa tu ile ya Johannesburg nchini Afrika kusini, inatokana na mchango mkubwa wa raisi huyo katika kumalizia mradi huu mkubwa na wenye manufaa kwa Taifa, uliyoachwa na mtangulizi wake ambae ni baba wa pili wa taifa hili (baada ya Nyerere) na mzalendo namba mbili (baada ya Nyerere) hayati John Pombe Magufuli.

Inasemekana Terminus hiyo itaanza kuitwa rasmi kwa jina la "Samia SGR Terminus" siku hiyo ya ufunguzi wa Terminus hiyo, na bila shaka litapokekelewa kwa mikono miwili na viongozi wote wa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wizara inayohusika na maswala hayo ya kitaifa.

Sisi wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla tunasubiri kulipokea suala hili kwa mikono miwili. Tunajua haters huwa hawakosekani, lkn hilo halina shida kwani kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi mtamu.

Samia SGR Terminus imekamilika, tujiandae kwa ufunguzi wa safari mbalimbali.

View attachment 2593948
Napendekeza iitwe Akilihuru Terminus itapendeza sana.
 
Paitwe Mtemi Isike au hata Mangi Meza au Olaigwanani au washiili ila sio hivyo.

Amalizie kwanza ujenzi halafu apewe kile kituo cha mwisho yaani kule mwisho wa Reli.
 
Miradi,Shule zatakiwa zipewe majina ya maeneo husika na sio kupachika majina ya watu.
Siku ikitokea nikawa Rais nafuta kila jina la mtu yanabaki Nyerere,
 
Vipi hizi barabara zetu zilizopewa majina ya watu tusiwajua sijui kina Sam Nujoma, Kenyata, Kwame Nkuruma nk?
Au wao ni sahihi lkn wa kwetu sio sahihi?
 
Ufunguzi wa hii treni ya SGR ni lini?
Habari zenu wana JF wenzangu,

Hizi ni tetesi kutoka kwa mtu wa ndani ya kitengo fulani, ambapo amesema mpango huo wa kuipa Terminus hiyo jina la raisi Samia utafanyika siku ya ufunguzi wa safari za train hizo zinazotumia umeme.

Mdau huyo amesema kwamba lengo kuu la kuipa Terminus hiyo kubwa, nzuri na yenye kuvutia kuliko Terminus yoyote barabarani Africa ukiondoa tu ile ya Johannesburg nchini Afrika kusini, inatokana na mchango mkubwa wa raisi huyo katika kumalizia mradi huu mkubwa na wenye manufaa kwa Taifa, uliyoachwa na mtangulizi wake ambae ni baba wa pili wa taifa hili (baada ya Nyerere) na mzalendo namba mbili (baada ya Nyerere) hayati John Pombe Magufuli.

Inasemekana Terminus hiyo itaanza kuitwa rasmi kwa jina la "Samia SGR Terminus" siku hiyo ya ufunguzi wa Terminus hiyo, na bila shaka litapokekelewa kwa mikono miwili na viongozi wote wa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wizara inayohusika na maswala hayo ya kitaifa.

Sisi wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla tunasubiri kulipokea suala hili kwa mikono miwili. Tunajua haters huwa hawakosekani, lkn hilo halina shida kwani kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi mtamu.

Samia SGR Terminus imekamilika, tujiandae kwa ufunguzi wa safari mbalimbali.

View attachment 2593948
 
Majina ya viongozi kila kitu si poa, Mama Samia alitakiwa aanzishe na yeye mradi wake wa kuacha alama utakaopewa jina lake. Hii station napendekeza iitwe " Mount Kilimanjaro Central Station". Na hizo station zingine kuu za mikoa zipewe majina ya vivutio vyetu vya utalii.
Mimi nafikiri ingeitwa Tanzanite Terminus station kutokana na muonekano wake ni wa Tanzanite.

Afu lile daraja lingepewa jina lingine mfano hilo la mount kilimanjaro bridge nk.
 
Coco Beach Bridge inatosha.

Back
Top Bottom