Tetesi: Dar es Salaam SGR Terminus kupewa jina la Rais Samia

Kwani hata hayo si mazuri mkuu? Mbona kuna barabara zetu zimepewa majina hata ya watu tusiowajua. Ukiuliza unaambiwa sijui alikuwa mpigania uhuru wa Togo, Msumbiji au sehem fulani.
basi naye mpeni barabara, hii iitwe Dar terminal inapendeza zaidi
 
Vipi hizi barabara zetu zilizopewa majina ya watu tusiwajua sijui kina Sam Nujoma, Kenyata, Kwame Nkuruma nk?
Au wao ni sahihi lkn wa kwetu sio sahihi?
Hao ni sahihi ila hawa wa sasa imekuwa kero.

Hao kina Kenyatta huwezi kuta wamepewa jina la shule, mara stendi, mara mji, mara hospital
 
Almurad wasipewe viongozi!!..chuki dhidi ya viongozi wako inakusaidia nini!?
Ndo hapo na mimi nashangaa inakuaje watu hawalalamiki barabara zetu za umma kuitwa majina ya watu tusiowajua na wasio na mchango wowote wa maana kwa nchi yetu kama vile barabara ya Moi, Kenyata road, Kwame Nkurumah nk.

Lakini kwa viongozi wetu ndo wanakimbilia kulalamika.
 
Paitwe Mtemi Isike au hata Mangi Meza au Olaigwanani au washiili ila sio hivyo.

Amalizie kwanza ujenzi halafu apewe kile kituo cha mwisho yaani kule mwisho wa Reli.
😂😂😂
 
Kama Dar es Salaam SGR Terminus haitoshi iitwe Ilala au Temeke SGR Terminus.
Ok mkuu nafikiri wahusika wakipita humu wataangalia comment na kufanyia kazi ushauri mbali mbali.
 
What is the problem??
 
Ili ajengewe heshima reli ya SGR ipewe jina la SAMIA, itapendeza sana.
 
Bahati mbaya huenda ikawa white elephant project kama zilivyo nyingine nyingi chini ya serikali ya ccm.

Kwa kujenga hatuna mpinzani, usimamizi sasa, zero kabisa.
 
Wangeita Hashim Mbita sgr terminus. Huyu mtu major hashim mbita naona hajaenziwa inavyostahili hapa tanzania.
 
Paitwe Station kama ilivyo sasa. Tuachane na huu ujinga wa kuvipa vitu vya Taifa majina ya viongozi.

Mie naona bora iitwe Mandonga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…