Dar es Salaam ya mwaka 1975 ilikuwa nzuri sana!

Dar es Salaam ya mwaka 1975 ilikuwa nzuri sana!

Tangu mkoloni aondoke Tanzania, Mtanzania anaishi varuvaru tu bila mpangilio wowote ule.

Dar es salaam ni Slum, watu wanazaliana na kuishi kama mapanya.

Hovyo hovyo, vululu-valala.
Hayo majengo yalikua ni ya wazawa wala sio wakoloni, mlaumu Nyerere aliyoyataifisha, Waingereza hawaja invest chochote cha Maana Tanzania maana wao walikuwa ni kama caretaker tu.
 
Hakika mkoloni naye alikuwa na mema yake mengi, aliweza kutupanga
1724852605955.png
 
Mji kaujenga Mjerumani. Ndiyo maana makanisa yako posta mji ulikoanzia
Hapana Mjerumani kaukuta mji, mji umejengwa na Sultan wa Znz, Ujerumani hata hakua na Time na dar,

Mjerumani kaja Dar kakuta watu tayari. Kuna uzi humu unaelezea Historia ya kaburi pale mnara wa saa.

Hilo kaburi lilizua ugomvi baina ya wajerumani na local Soma kujua Ujerumani walikuta nini.

Ushahidi wa pili wakati hao wenye hizo nyumba wanajenga waliweka majina yao juu ya nyumba, zilikua ni kama fashion fulani wakati huo. Mpaka leo unakuta tarehe ya jengo iliojengwa na mmiliki kama hivi
Natwar_House_-_Colonial-Era_Facade_-_Dar_es_Salaam_-_Tanzania (1).jpg
 
Yeye sultan hakukuta watu hapo Dar?
Kakuta watu ila kama mashamba, yeye akaona potential ya eneo akalinunua na kuanzisha mji. Na yeye ndio alitoa hilo jina Daru Al salaam iki maanisha nyumba ya amani.

Sultan alikua na mahusiano mazuri na Iran na Pakistan ya sasa (India ya zamani) kuna wakati Sultan alipinduliwa Oman akakimbilia huko na kupewa eneo atawale na kupata kodi mpaka alipopata nguvu akarudi na wanajeshi wa Kibulushi na ku Conquer Oman tena, toka wakati huo wanajeshi wa Oman na hata watu wa karibu wa Sultan wa katoka India ya zamani.

Baada ya Sultan kutawala Huku akaja na wahindi wake ambao wengi walikua na tabia kama za leo, ana duka chini anaishi juu, ndio wakajenga Znz na huku dar.

Na sio tu kujenga mji kuna watu wakubwa wakubwa ambao wametoka maeneo hayo na kutikisa dunia kwa Ugunduzi wao na kazi zao ila hawasemwi leo sababu ya mambo yetu ya kipuuzi.
 
Na sio tu kujenga mji kuna watu wakubwa wakubwa ambao wametoka maeneo hayo na kutikisa dunia kwa Ugunduzi wao na kazi zao ila hawasemwi leo sababu ya mambo yetu ya kipuuzi
Watu gani hao mkuu hebu wataje hapa. Au ni siri na wewe hautaki kuwataja?
 
Back
Top Bottom