Maana walianza kwa appreciate namna alivyoruhusu uhuru wa kujieleza, utawala wa Sheria, kufuta makesi ya kubambikiza na kuweka mazingira ya kuvutia wawekezaji.
Tukaona mwisho wa kesi ya Mdude Chadema, kurudi kwa Yusuf Manji na wao akina Mbowe kushinda RUFAA ya kesi ya Akwilina.
Bahati mbaya wakaanza kumshurutisha Rais kuwa akutane nao. Ingawa Rais alikuwa amejipangia ratiba yake ya kukutana na makundi masilahi mbalimbali. Kwenye kundi la vyama vya Siasa walisikika wakisema kuwa Rais akutane na CDM peke yake wao hawatahudhuria akiita vyama vyote kwa pamoja.
Suala la Katiba. Rais alikwisha sema kuwa kwa sasa anashughulikia kupanga uchumi, Katiba isubiri. Wao CDM wanasema hapana tunataka Katiba mpya sasa.
Mikutano ya hadhara. Kimsingi ni halali kikatiba, lakini Rais SSH ameikuta executive order ya kuifungia iliyowekwa na Magufuli. Kwa busara yake akasema ngoja kwanza ajiridhishe kuhusu hiyo mikutano ya hadhara. Lakini CDM hawaja taka kujua Wana deal na Rais muungwana. Wakaamua kupuuza na kuendelea na hiyo mikutano. Kwenye mkutano wa Barccuda wakampandisha yule mtukana matusi maarufu aliyekuwa rumande kuanzia mwaka jana na akawa ametoka recently na akatoa matusi mapya dhidi ya Rais. Kuwa atamnyoa kwa wembe aliomnyolea mtangulizi wake.
Na akina Mbowe hawakumchukulia hatua kumkanya, wakaona ni sawa tu.
Huyu Rais mpole na muungwana, anakubalika sana na wananchi. Ukiweka mkakati wa Siasa za kumvuruga kama Mwendazake CDM mtapoteza kukubalika kwenu na wananchi.