Dar: Gari 35 zazuiliwa kuendelea na safari stendi ya Magufuli

Dar: Gari 35 zazuiliwa kuendelea na safari stendi ya Magufuli

Mimi ndiyo ningekuwa Vehicle inspector
Wa kukagua magari nakuapia 85%
Ya magari ya usafishaji yangepaki haki yangu magari mengi Ni mabovu sana

Ongea wewe Kingsharon92 sisi tukiongea tunaitwa wahujumu
Ila nimekapenda hako kautaratibu na nna uhakika saa hizi magari ya kesho yako garage
 
Ongea wewe Kingsharon92 sisi tukiongea tunaitwa wahujumu
Ila nimekapenda hako kautaratibu na nna uhakika saa hizi magari ya kesho yako garage
Naongea hivi nikiwa dereva mkongwe zaidi ya miaka 30 magari mengi Ni mabovu sana
 
Wazuie na gari chakavu za Dar Moro! Nimepanda basi la BM Coach likazimwa maeneo ya mlandizi kuwashwa mpaka tukashuka kusukuma! Starter mbovu!

Mwaka 2020 kutembea na gari starter mbovu ni msiba
Mlandizi wapi mbali hivyo mkuu.Princess Muro wakati huo mkitoka Ubungo mnafika Mbezi tairi imepata pancha[emoji3]
 
Kwa kawaida magari makubwa wenye Mali wanatakiwa gari likaguliwe garage kila baada ya wiki sita

Hii inafanya gari kuwa imara kwa muda mrefu na kujua dosari ndogo na kubwa zinazoweza kujitokeza

Ni muhimu pia kila mwaka magari yangekuwa yanapewa Cheti cha ukaguzi kutoka Garage kuwa inakidhi viwango vya kutembea barabarani

Hiyo itapunguza ajali nyingi ziaizokuwa na ulazima kwani haya yanaepukika sana kwa wenzetu wanaofuata sheria
Tatizo letu hata kama Dereva akimwambia mmliliki kuwa tairi zimeisha ataambiwa mbona bado sana ila likianguka na kuuwa hapo ni kosa la dereva
 
Unayo hoja ya msingi lakini wenye mabasi hapa hawawezi kukuelewa
Kabla ya kuwabeza labda tujue machache...

Kwani walikagua vitu gani haswa?
Na wamefanya ukaguzi kwa masaa mangapi?
Na wakaguzi walikua wangapi?
Walitumia macho peke yake bila vifaa vingine vya ukaguzi?
 
Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Ibrahim Samwix ameyazuia mabasi 35 kuendelea na safari kutokana na ubovu mbalimbali aliogundua kwenye magari hayo kabla ya safari

Magari hayo hayataruhusiwa hadi yataka tengenezwa kwa kuwa yalikuwa yanahatarisha maisha ya wasafiri

Wito umetolewa kwa wenye magari kuyakagua na kuyatengeneza magari yao mara kwa mara ili kuepuka usumbufu

View attachment 1767667
Hayo mabasi 35 hayana mwenyewe? Yataje majina na kampuni zao
 
Mlandizi wapi mbali hivyo mkuu.Princess Muro wakati huo mkitoka Ubungo mnafika Mbezi tairi imepata pancha[emoji3]
Hahahah hawa wajinga gari nzuri wameweka ruti za Arusha, Dom, Mbeya na Mwanza 😂😂😂 huku kwengine wanatuwekea mi ngara ngara tu!
 
Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Ibrahim Samwix ameyazuia mabasi 35 kuendelea na safari kutokana na ubovu mbalimbali aliogundua kwenye magari hayo kabla ya safari

Magari hayo hayataruhusiwa hadi yataka tengenezwa kwa kuwa yalikuwa yanahatarisha maisha ya wasafiri

Wito umetolewa kwa wenye magari kuyakagua na kuyatengeneza magari yao mara kwa mara ili kuepuka usumbufu

View attachment 1767667
Hivi hii stand hapakua na jina lingine mpaka iitwe jina kama hili?
 
Mkuu ungekosoa kwa hoja ungetusaidia sana hapa. "....kuna ukaguaje wake"... Huo ukaguaji wake ukoje?
"... Magari 35 ni mengi sana kukaguliwa kwa muda huo"....embu fafanua kidogo. Unamaanisha ni mengi kwa kuzingatia idadi ya wakaguzi vs muda?aina ya ukaguzi vs muda?
Soma hio tarifa, sikuwabeza nimesema kile ninachokijua! Magari yanatakiwa kukaguliwa na kuna ukaguaji wake! Narudia magari 35 ni mengi sana kukaguliwa kwa muda huo kama anavyoonekana kwenye picha.
 
Kama ameweza kuzuia magari 35 Ina maana walikagua magari mangapi kwa siku ya leo pale stendi?????

Polisi wanajulikana kwa hila, hapo ameendesha hiyo kampeni ili hao 35 wamfate pembeni watoe kitu awaachie, imagine kila gari akipewa laki kwa magari 35 ni kiasi gani ili awaruhusu waingie barabarani???

Hizi kampeni za dizaini hii kwa polisi huwa zinafanyika makusudi kabisa na unakuta boss mwenyewe anasimamia Ile ni pesa yake maana yeye anajua hasimami barabarani kila siku. Yeye anakuja Ile saa 11 alfajiri akiendesha kampeni ya ukamataji mpaka saa nne anarudi zake ofisini the waliokamatwa wanaambiwa aliyekamata ni boss so wamfate ofisini kwake.

Huko wanamalizana hammuoni stendi labda baada ya mwezi 😃
 
Magari ya leo siyo yale yenu ya nyundo.

Au ndiyo nyie mnaopona corona kwa nyungu?

Kama nyungu ni dili mbona haiwasaidii nazo India?

Ukaguzi wa magari by mburula? Si waseme tu ni kutengeneza mchongo wa rushwa?
Labda hauko TZ wewe mbona garage zote mafundi ni wazuri tu na hawana degree mkuu?? Ila uelewa wao ni mzuri tu gari zote za kisasa wanatengeneza? Tena za kisasa ni rahisi sana kutengeneza you just check problem through computer program.
 
Kuna Basi linaitwa Shambalai, kama limeponyoka labda kama leo halikua ubungo, lile likipita ni kama kichanja kinatembea...
Shunie bishaaaa....?????
Umekaa unashangaa kitu kinakugonga miguuni, ukiangalia kumbe kuna kuna aliyebeba kuku huko ametaga.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Asilimia 60% ya ajali za barabarani ni uzembe wa madereva..juzi natoka dsm to mwz..tupo na gari ya Allys tulipata ajali sherui..wakati dereva wa basi alipo kuwa anaovateki lori la mafuta..akakutana uso kwa uso na semi..trafk wasiishie kukagua ubovu tu..hata mwendo kazi wazidi kucontrol
IMG-20210424-WA0026.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda hauko TZ wewe mbona garage zote mafundi ni wazuri tu na hawana degree mkuu?? Ila uelewa wao ni mzuri tu gari zote za kisasa wanatengeneza? Tena za kisasa ni rahisi sana kutengeneza you just check problem through computer program.

Tanzania mambo kijima kijima tu. Kila mtu ana weledi katika kila jambo. No wonder hata magari yanaweza kupigishwa nyungu vile vile.

Hiiiiii bagosha!
 
Ubora wa magari wanaufanyia kituoni?

Ilipaswa kuwe na utaratibu labda wa kila wiki wahusika kupeleka magari yao kwenye vituo fulani vya ukaguzi pengine kila mkoa au wilaya
 
Back
Top Bottom