Uchaguzi 2020 Dar: Helkopta ya Kampeni ya Tundu Lissu, yanyimwa kibali cha kutumia anga, ni baada ya kuomba kibali hapo jana

Uchaguzi 2020 Dar: Helkopta ya Kampeni ya Tundu Lissu, yanyimwa kibali cha kutumia anga, ni baada ya kuomba kibali hapo jana

Kumbe kibali walikuwa nacho
 

Attachments

  • 2514840_20200910_200044.jpg
    2514840_20200910_200044.jpg
    200.1 KB · Views: 1
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Ratiba ya mikutano 5 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Tundu Lissu, iliyopangwa kufanyika leo mkoani Pwani, imevurugika baada ya helkopta aliyokuwa aitumie kufika katika maeneo hayo, kuzuiliwa kwa kunyimwa kibali na Mamlaka ya Anga nchini, muda mfupi kabla ya kuruka.

Taarifa za kukataliwa kwa helkopta hiyo kuruka zilitolewa kwa Ofisa Mnadhimu wa Kampeni, Amani Golugwa, wakati msafara wa Mhe. Lissu ukielekea kupanda ndege baada ya kumaliza taratibu zote za ukaguzi wa kiusalama Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) terminal I.

Ofisa wa Mamlaka ya Anga aliyewasilisha taarifa hiyo wakati msafara wa Mhe. Lissu umeshatoka nje ya jengo la abiria, ametoa sababu zisizoeleweka kuzuia helkopta hiyo kuruka kutoka Uwanja wa JNIA kuelekea Bagamoyo, Chalinze, Mlandizi na Kibaha, wakati kibali chake kiliombwa tangu jana.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema imelazimika kutafuta njia mbadala ili Mgombea Urais Mhe. Lissu na msafara wake, aweze kuendelea na ratiba ya mikutano kwa kadri inavyowezekana. Mbali ya Mhe. Lissu, abiria wengine waliokuwa watumie usafiri huo ni watu 3, akiwemo Ofisa Mnadhimu wa Msafara Amani Golugwa, Katibu wa Mgombea, David Jumbe, msaidizi wa masuala ya ulinzi pamoja na rubani wa ndege hiyo.

Imetolewa leo, Alhamis, Septemba 10, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano


Majibu
 

Attachments

  • 2514840_20200910_200044.jpg
    2514840_20200910_200044.jpg
    200.1 KB · Views: 1
Lakini Magufuli hii nchi anaitafuta nini? Amezuia wenzake wasibandike mabango yao kwenye miji mpaka kwenye vyoo yeye kabandika ya kwake, amezuia vyombo vya habari visitangaze habari za wenzake! Sasa anazuia hata wasitumie helicopter, tunakoelekea atazuia hata wasifanya kampeni! Dunia hii kuna majitu ni majibwa!
Sema saccos haina pesa bado wanasubiri ile 25% walioahidiwa na mabeberu ndiyo maana wameshindwa kuweka mabango!
 
Acheni usanii hauwasaidii, hakuna aliyekataza kidege chenu, tatizo hamtaki kufanya siasa mnataka itokee fujo ili mpate sababu ya kusema kwa mab...na zenu. Mwakaa huu haumizwi mtu mtashindwa mchana kweupe. Chuma kipo chato kinapata mirinda bariiiiiidi kwa siku mbili huku kikisindikiza na supu ya kamongo, kitakapoibuka kwa awamu nyingine mtapata habari yenu. Kwa sasa kila anachofanya JIWE na nyie mnaiga, kaamua kupumzika na nyie mnapumzika kwa kisingizio cha kukosa KIBALI, DUU PATHETIC GETE GETE
haki itendeke kwa wagombea wote , kama ambavyo mgombea wenu habughudhiwi , kwa chochote akifanyacho , mfano pishapu , kupiga ngoma za bendi, kucheza mziki , kuwa na wanamziki , na vyombo vya habari kumkava yeye ,hivyo na wagombea wengine waachwe wafanye kampeni kwa raha zao , hasa chadema ,mnaisumbua sana why, so kama anakunywa soda baridi huko chato bahada ya kazi ngum ya kampeni, ni vizuri na nimpe pole , ila chokochoko kwa upande wa wagombea weza kiti cha urais zikomeshwe mara moja ,
 
Swali ni Je siku zote hiyo helicopter ilikuwa inarushwa na rubani gani???? Kama ndo huyo huyo Kwa nini siku nyingine wanekuwa wakimruhusu???
Jaribu kuelewa hapa Tanzania Rubani haruhusiwi kuendesha ndege akizidi miaka 65 ndiyo TAA Regulation zinasema hivyo ndiyo maana hao wamiliki wa Helcopiter ilibidi waombe waiver hivyo haijawahi kuendeshwa na Rubani wa miaka zaidi ya 65. By the way TZ marubani wa kiraia ni wengi sana wasiozidi miaka 65 nasikia Saccos hawajalipa pesa ndiyo maana walimiki wa Helcopitet wameanza kupiga chenga!
 
haki itendeke kwa wagombea wote , kama ambavyo mgombea wenu habughudhiwi , kwa chochote akifanyacho , mfano pishapu , kupiga ngoma za bendi, kucheza mziki , kuwa na wanamziki , na vyombo vya habari kumkava yeye ,hivyo na wagombea wengine waachwe wafanye kampeni kwa raha zao , hasa chadema ,mnaisumbua sana why, so kama anakunywa soda baridi huko chato bahada ya kazi ngum ya kampeni, ni vizuri na nimpe pole , ila chokochoko kwa upande wa wagombea weza kiti cha urais zikomeshwe mara moja ,
Tatizo saccos hawajalipa advance ya kukodi Helcopiter ndiyo maana wamiliki wa ndege wanapiga chenga!
 
KWELI MTI WENYE MATUNDA NDIO HUPIGWA MAWE....
Tundu lissu anapigwa kotekote
huku magufuli
huku majaliwa
huku samia
huku kikwete
huku pinda
huku NEC
huku mamlaka ya anga sijui nini na nini
huku tbccm
huku policcm

Wote ni dhidi ya Tundu lissu tu

Mungu ndo amesimama na Lissu na watz wote wako pamoja naye

Watz wanatala mabadiriko hakuna kingine na tumechoka kuonewa mara hii hatutakubali tena
kimbunga lissu 2020 , ni mashine ya mjerumani , siku moja tu ikiwashwa , inasaga kila kitu kinakua unga , upepo wake ukipita tu usipo jifunga taulo vizuri utashutuka imekwapuliwa, na mtu katupwa kule , kikipuliza kinapangua first eleven yote
 
Back
Top Bottom