Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Dah nyie wa kishua, vipi unaeza nipa hata u house boy kwenu [emoji1][emoji849]
We nawe, hahahaha shida Sina emoj,

Siriaz kwetu viwanja ni bei Sana, imagine hapa tunapoishi 2009 mama alinunua kiwanja kwa elfu hamsini,lkn mwaka Jana bei yake ni mion 5,

Wanaosababisha bei kupanda ni wakinga/wachaga wanasifa kweli.
 
Hiko kiwanja kina ukubwa gani?
Maana hiko cha mil 8 ni cha futi 10 kwa 15.Tena rural area huko kama unaelekea Kisarawe 2 ama Pemba mnazi.
Aya hicho cha mil 8 kijijini kwenu heka ngapi na eneo la urban ama rural?
Hayo sijui,lkn kwetu viwanja ni bei juu.
 
Habari zenu,

Mjanja M1 nimeona maeneo mengi Dar vijana wenye umri mkubwa miaka 30 na kuendelea wakiishi kwa wazazi wao na wengine kuzalia makwao.

Kautafiti kangu kamegundua zaidi kuwa kuna wanaume waliooa pia ambao wanaishi na wake zao kwenye nyumba za wazazi wao.

Vijana wengi wa Dar wameshakata tamaa ya kujenga makazi yao binafsi, wengi wanategemea cha wazazi eg. Nyumba, Magari n.k

Utafiti wangu pia umegundua kuwa kuna vijana wanaojitegemea lakini maisha yao hayapo vizuri kwani kesho yao imekuwa ngumu kueleweka, na mara nyingi utakuta kijana anaishi kwenye nyumba za kupanga na bado kodi ya pango inamsumbua kulipia.

Vijana hawa wenye umri mkubwa hawana future iliyobora maana kuna uwezekano kwenye uzee wao wakawa wanaishi maisha ya tabu kwa kukosa makazi yao binafsi.

USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.

NB. HUU NI UTAFITI WANGU KAMA MJANJA M1, KAMA UTAUPINGA BASI UTAKUWA SAHIHI PIA.

Written by Mjanja M1.
Yaan essay nzima umejielezea wewe na umefika conclusion kwa kuniambia Serikalini ifanyaje? Unafikiri wao wanaangalia kuhusu hilo wewe ushaambiwa lea mtoto wako akikua kumuendeleza ni jukumu lako masuala ya Ajira wewe mzazi ndio muajiri Namba 1 mpe shughuli za kufanya mwanao mpe mtaji afanye Jambo analolipenda acha masuala ya kusubiria Serekali ikufanyie hadi kukupa Ajira ikufanyie wewe umekalisha tu hakuna Serekali inayokuletea Ugali nyumbani kwako kwa hio akili kwenye utosi watoto wako wasaidie mwenyewe utajua unawapeleka shule kusoma au unawafungulia mradi wa familia Ila Serekali haiwezi kunyanyuka ikaja kuwaajiri watoto wako uliowazaa mwenyewe wakati wenyewe wapo Serekalini wana watoto, ukiambiwa ongeza na za kwako

Idumu Mizimu!
 
Hawa vijana muwaonee huruma wana stress sana wengi hawapendi kubaki kwao wanalazimika

Kuna vijana tangu wamalize vyuo hawana mishe za maana hivyo hata kwenda kupanga anaona kodi zitamtesa na akizingatia kwao kuna vyumba/chumba

Wengi unakuta walisoma seko mpaka chuo ila hawana ujuzi wowote wa VETA wanategemea magamba yao ya vyuo. Mitaji ya biashara hawana familia maisha ya kuungaunga.

Wengine wamejiongeza kuwa boda au winga K/koo, udalali n.k

Wanaumia sana wanapoona wenzao waliosoma nao wakiwa wana mishe. Wao wakiamka asuhuhi hawajui waende wapi

Tusiwaseme sana vijana wa Dar ila wanachopitia Mungu mwenyewe anajua
Hiyo hali haipo Dar tu hata huku pembezoni.

Yote maisha tu....keep on hustling
 
Ni mkoa gani wanagawa viwanja bure ndugu? Naku hakikishia hakuna mkoa wenye viwanja Bei rahisi Kama dar
Unazingua wewe, huko mabush mzee ana hekari saba atashindwa vipi kumpa mwanae robo heka akajenga na kuoa
 
Kitu kilichonishangaza ni kua kuna watu wamezaliwa dar na kukua dar ila mwisho wao wa kutembea ni Morogoro na chole. Wengine hadi wanakua watu wazima hawajawahi fika chalinze/moro
Aise ila syo wote mkuu wengine tumezaliwa dar lakini nchi tumeitembea vijiji kwa vitongoji

Ova
 
Habari zenu,

Mjanja M1 nimeona maeneo mengi Dar vijana wenye umri mkubwa miaka 30 na kuendelea wakiishi kwa wazazi wao na wengine kuzalia makwao.

Kautafiti kangu kamegundua zaidi kuwa kuna wanaume waliooa pia ambao wanaishi na wake zao kwenye nyumba za wazazi wao.

Vijana wengi wa Dar wameshakata tamaa ya kujenga makazi yao binafsi, wengi wanategemea cha wazazi eg. Nyumba, Magari n.k

Utafiti wangu pia umegundua kuwa kuna vijana wanaojitegemea lakini maisha yao hayapo vizuri kwani kesho yao imekuwa ngumu kueleweka, na mara nyingi utakuta kijana anaishi kwenye nyumba za kupanga na bado kodi ya pango inamsumbua kulipia.

Vijana hawa wenye umri mkubwa hawana future iliyobora maana kuna uwezekano kwenye uzee wao wakawa wanaishi maisha ya tabu kwa kukosa makazi yao binafsi.

USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.

NB. HUU NI UTAFITI WANGU KAMA MJANJA M1, KAMA UTAUPINGA BASI UTAKUWA SAHIHI PIA.

Written by Mjanja M1.
Kumbuka hao unaowasema wametoka mikoani

Ushamba wa watu wa mikoani kudhania maisha ya DSM ni rahisi ndio linapelekea kuja kwa wingi na kuwa katika hali hiyo
 
Kama home unapata aman unakula fresh humtesi mzaz au mlez we Kaa tu HAPO at the end kinachomatter ni furaha ya MTU binafsi
 
Watu wa dar ndiyo wakija huko mikoani,vijijini wanawaletea mipango
Hebu waheshimuni watu wa dar
Ila kweli watoto vijana wengi wa dar sana sana wale wenye nyumba za urithi hawatakagi kujituma
Wao wanasikilizia kodi,au mzee wao angoke wagombe Mali wauzeee

Ova
 
Ulilolisema ni sahihi kabisa, 80% ya marafiki zangu, majirani zangu I mean age mates wangu wanaishi majumbani kwao. Home Kijitonyama washkaji wengi wanafanya kazi lakini hawajatoka kwenye nyumba za wazazi. Ila nilichogundua ni pamoja na kuwepo kwa space, na wengine wanaambiwa na wazazi wao wenyewe kwanini unataka kupanga wakati vyumba nyumbani vipo?
Hii ilinitokea hata mimi kabla sijahamishiwa kikazi mkoani, mama haukutaka nikapange kabisa maana madogo wote wapo mikoani kikazi.
Halafu pia bei za vyumba DSM sio kama pale Kibaigwa 😂😂
 
Niwatetee vijana wenzangu wa dar., kwanza dar ndio mji wa Tanzania.
Mbili Vijana wa mikoani ndio huja huku dar, wachache wa dar hupenda kwenda mikoani, ni kutojua tu system zinavyoenda ndio maana wanakua wagumu kuona fursa. Ukiishi sana kwenye hekalu lako kuna maeneo unaweza usifike.
Tatu. Sisi vijana wa dar, nyumba kujenga ni kuanzia miaka 40-45, ma brother wanalifahamu hili. Vitoto vya kinyakyusa na kihaya, ndio ndoa nyingi mnazoziona mjini, sijui kwa garab siijui doctor cheni au wale wengine.
Sisi wa dar ndoa ni from 30's hao dada zenu ndio wanaoana ndoa za kitoto, 23-27 binti ameolewa. Sisi wa dar hatupo hivo, sisi ndoa from 28-40. Na watoto tunazalia nyumbani.
Wengi wetu kazi tunapata mapema tu. Ila hawa wa mikoani ndio wamejaza unemployed kwa dar.
Jitafakari. Hii nimeongea kwa upande wangu na mahomebiy wangu wa dar. Sasa jiweke ww utajijua wa dar au wakuja.
 
Kitu kilichonishangaza ni kua kuna watu wamezaliwa dar na kukua dar ila mwisho wao wa kutembea ni Morogoro na chole. Wengine hadi wanakua watu wazima hawajawahi fika chalinze/moro
Chalinze tufuate nini ?
 
Back
Top Bottom