Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Dar inaongoza vijana watu wazima kuishi kwa wazazi wao

Kitu kilichonishangaza ni kua kuna watu wamezaliwa dar na kukua dar ila mwisho wao wa kutembea ni Morogoro na chole. Wengine hadi wanakua watu wazima hawajawahi fika chalinze/moro
Tatizo hapo lipo wapi mkuu,

Ni nchi gani dunia hii au eneo gani unatamani kulitembelea. Je eneo hilo au nchi hiyo unadhani kinacho kukwamisha kutembelea huko hivi sasa ni nini?
 
Yesu mpaka anafika miaka 30 alikiwa anakaa kwao na muda mwingi alikuwa anatembea na mama ake na kila anapoenda mama anamfata watu wa mikoani mko obsessed sana Dar sijui mna matatizo gani
Wee na Yesu nani mwenye akili
 
Habari zenu,

Mjanja M1 nimeona maeneo mengi Dar vijana wenye umri mkubwa miaka 30 na kuendelea wakiishi kwa wazazi wao na wengine kuzalia makwao.

Kautafiti kangu kamegundua zaidi kuwa kuna wanaume waliooa pia ambao wanaishi na wake zao kwenye nyumba za wazazi wao.

Vijana wengi wa Dar wameshakata tamaa ya kujenga makazi yao binafsi, wengi wanategemea cha wazazi eg. Nyumba, Magari n.k

Utafiti wangu pia umegundua kuwa kuna vijana wanaojitegemea lakini maisha yao hayapo vizuri kwani kesho yao imekuwa ngumu kueleweka, na mara nyingi utakuta kijana anaishi kwenye nyumba za kupanga na bado kodi ya pango inamsumbua kulipia.

Vijana hawa wenye umri mkubwa hawana future iliyobora maana kuna uwezekano kwenye uzee wao wakawa wanaishi maisha ya tabu kwa kukosa makazi yao binafsi.

USHAURI - NAOMBA SERIKALI IONGEZE NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA, NA PIA IONDOE VIKWAZO VINGI KWA WANAOFANYA BIASHARA.

NB. HUU NI UTAFITI WANGU KAMA MJANJA M1, KAMA UTAUPINGA BASI UTAKUWA SAHIHI PIA.

Written by Mjanja M1.
Mie hapo sioni cha ajabu cha msingi ni wazazi wenyewe wameridhia kijana azeekee kwao basi!
Kama Yesu mwenyewe mpaka leo bado yuko kwa babake iweje kwa kijana wa Dar?
 
Upo sahihi, lakini kama una familia au mtoto inakupasa uwe na kwako.
Inatagia hali ya familia ya kwenu. Waarabu, Wahindi na Wapemba wana utamaduni wa ndugu wengi kukaa pamoja katika nyumba au compound moja.
 
Back
Top Bottom