Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Siijui kesho yangu Ila naijua kesho ya taifa langu. Narudia.. Lissu hatakaa awe Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sio 2020 ni kamwe(NEVER), hatakaa awe Raisi wa nchi hii. Mkuu wabongo hampendi kuusikia ukweli Ila huo ndo ukweli. Tanzania haiwezi ongozwa na mtu type ya Lissu, system haiwezi kuruhusu amekosea sana kuhusisha wazungu kwenye mbio zake, nakuhakikishia hawezi kuwa Raisi wa nchi hii hata iweje. Kuna nyaraka zake za hatari zimeshanaswa tayari amekuwa declared threat kwa Jamhuri. Take it from me.
Kwahiyo akishinda kwenye sanduku la kura ni kupindua meza?Je,walioamua kumpa kura wakikataa na kuamua kufanya maamuzi ya nguvu ya umma,mtaweza kuzuia uamuzi wa wananchi?Libya system yao iliwaambiaje?Misri?Algeria?Kenya?Burundi?Leo wale waliokuwa madarakani na kutumia hizo systems wapo?
Kama mmeichoka amani basi zuieni sanduku la kura lisiongee!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ukiingia JF waweza kudhani Lissu atashinda kuwa Raisi. Ukweli ni kwamba Lissu hatakaa awe Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sio 2020 ni kamwe(NEVER), hatakaa awe Raisi wa nchi hii. Ila kikatiba mnaruhusiwa kujitekenya na kucheka wenyewe mitandaoni masaa 24(24/7). Tarehe moja mwezi ujao ndo mtaelewa ninachomaanisha hapa.
Na huo ndo ukweli. Tundu Antiphas Lissu ndo Raisi wako wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025
 
Mpaka sasa Lissu kawazidi akili mno na tunaanzisha vuguvugu la kumng'oa Sirro bila huruma yoyote , ametia aibu Jeshi la Polisi , IGP mzima huwezi kutumwa na mtu kama Polepole
Binafsi sina la nyongeza zaidi ya kukueleza kuwa ' Navalny ni binadamu pia Lissu ni mtu! '
 
"Kanda Maalum Ya Polisi Dar Es Salaam" inahusika vipi na uhalifu wa mkoa mwingine, swala la kosa aliloitiwa (Japo halijatajwa) Mh Tundu Lissu ni mkoa wa Mara na akatakiwa ku report Kilimanjaro. Mambosasa yanamhusu nini maswala ya mikoa mingine?.

Nchi yetu jeshi la polisi limekosa weredi kabisa, viongozi wanakurupuka na kujiamulia tu anachojisikia, hawajui "TERRITORIAL JURISDICTION/MAMLAKA YA KIENEO" yanakwenda vipi na yana nguvu gani kisheria na mipaka ya mamlaka hayo.

Mambosasa anatakiwa afanye kazi kulingana na "TERRITORIAL JURISDICTION" ya eneo lake, eneo lake na mamlaka aliopewa kisheria ni ya Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam, hana mamlaka kisheria ya kuingilia maswala ya kikazi ya mikoa mingine. Aache kukurupuka kwani atalinajisi jeshi la polisi kuonekana halifuati sheria na mamlaka. Anapaswa arudishwe darasani na apelekwe kusoma upya sheria.

Barua ingekua imetokea "MAKAO MAKUU YA POLISI" raia tusingekua na pingamizi, na tungeiheshimu, kwasababu makao makuu ya polisi wana mamlaka ya mikoa yote kisheria. Ila barua inatoka "KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM". Kwa hilo watuache.

Acha lissu awanyooshe hawa vibwengo wenye vyeo vikubwa bila ya kuwa na elimu ya kukidhi matakwa ya kazi yao. Nchi inaendeshwa na kikundi cha watu wachache wanaojiamulia mambo bila kufuata sheria, wanatumia mamlaka na mabavu, ila sio sheria wala haki.

Au lasivyo wakiachiwa, kesho tutasikia Mhalifu amefanya kosa la Kubaka Morogoro halafu Jeshi La Polisi Mkoa Wa Kigoma limetoa barua ya kuachiliwa mara moja mhalifu huyo.

#KUFICHA AIBU, kesho utasikia Mambosasa anaongea na vyombo vya habari na kusema barua hio inayozunguka mitandaoni imeandikwa na watu "WASIOJULIKANA", wananchi tunaombwa tuipuuze.[emoji38][emoji16]
Kongole mkuu
 
Nani katukana?

Sisi tunamsema huyu kibaraka anaetaka urais ambae wakati wenzake tunapigania kujitoa kwenye makucha yao yeye yuko busy kuturudisha nyuma.
Unapigana kujitoa kwenye makucha au kujenga uwanja wa ndege chato???
 
Kwa hio hata huyu anayesema anapinga mafisadi inawezekana hata yeye baadae ikagundulika ni bonge la fisadi sio?
Petro ata Tembea yake ilionekana ni 'mwanafunzi wa Yesu'. Mpime mtu kwa anachokisema na kwa anachokitenda...mwanzo mwisho! Usipime ukaishia katikati!
 
Polisi mmeonesha weledi wa hali ya juu...hatutaki mtu alete visingizio,uchaguzi huu Lisu ndio atajua CCM ndio Dingi wa siasa za nchi hii.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
Mwaka huu ndo mwisho wa Ccm kutawala Tanzania. Mark my words
 
Kumlinganisha Lissu na Navanly.
Uzuri siku hizi ni rahisi sana kuwatambua akina 'Navanly' popote walipo. Kwa sababu wanaotengeneza akina 'Navanly' wanatumia kitabu kile kile na sana sana zaidi huwa wanabadili rangi ya 'jarada' la kitabu hicho.
 
Aisee, Kama na kiunzi hiki Lisu amekiruka basi nadiriki kusema Jamaa ameshashindikana.
CCM kila kukicha inahangaika kujibu hoja za Lisu,
Tume imemshindwa kuhusu hoja ya kumuunga mkono mgombea wa chama kingine,
Polisi wametumia mabomu ya machozi lakini watu wanaonyesha kutoyaogopa wananawa maji kisha wanamsalimia Lisu na mgombea mwenza,
IGP anatoa amri kumbe haijakidhi mahitaji ya kisheria, nahisi kunakitu MUNGU amempangia huyu mtu.
 
Back
Top Bottom