beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Julius Mzava (26) Mkazi wa eneo la usalama Chang’ombe Wilaya ya Temeke kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Magdalena Peter (56) kwa kumchoma kisu sehemu ya mwili wake.
Tukio hili limetokea tarehe 08/10/2021 saa 1:05 usiku eneo la Sandali Chang’ombe wakati marehemu(Magdalena Peter) alipoiingia chumbani kwa mtoto wake Julius Masawe(mtuhumiwa) kwa nia ya kumpa chakula na hapo ndipo aliposhambuliwa kwa kisu eneo la mwili wake akapata majeraha makubwa yaliyopelekea kupoteza kwa maisha yake licha ya jitihada za kumpeleka hospitali kufanyika.
Mtuhumiwa Julius Masawe (mtoto wa marehemu) amekamatwa, anahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani kama sehemu ya hatua muhimu za kisheria.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata na linawashikilia watu watano(5) kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vifaa vya magari na kupokea vifaa/vipuri vya magari vya wizi.
Watuhumiwa hao walikamatwa na vifaa mbalimbali vya magari zikiwemo taa za magari aina ya Toyota IST na milango ya magari ya aina mbalimbali.
Aidha, vitu mbalimbali vilivyokuwa vimeibiwa na wahalifu kwenye matukio mbalimbali ya uvunjaji vimekamatwa katika kituo cha Polisi Goba yakiwemo majenereta zaidi ya 25,vifaa mbalimbali vya ujenzi na mitungi ya gesi 10.
MULIRO J. MULIRO
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM DAR ES SALAAM