Dar: Kijana mbaroni kwa kumuua mama yake mzazi

Labda wale wa Mama wa kutype ndiyo wamekosea, maana wanakuwaga ni watu wazima kidogo,hasa wengi utawakuta kwenye office za Serekali,na wengi wao ndiyo vitengo vyao,hapo unakuta Mmama watu kawekewa mabarua karibu hamsini ya kutype,hapo ni mwendo wa kubuuluza tu!!
Boss nae hakukagua, kaipitisha tu
 
Miaka 26 bado mzazi anamlisha n kumpelekea chakula chumbani,umri huo ni kulelewa wazazi ndio wanajitakia na kuleta matatizo kwenye jamii zetu...mimi 22 tu nko napambana n hom nlishahama
 
Wamama wengi ndiyo huwa wanaharibu mitoto yao mingi ya kiume, tena ukilikuta ndiyo last born ndiyo shida kabisa jinsi linavyodekezwa na Mama yake hadi linazeeka Kama Mama yake yupo hai sau,Mara nyingi mitoto ya aina hii akili zao huwarudi baada ya Mama kufa, maana wanabaki na Jamii ambayo haiwezi kubaliana na Ujinga wake,kwa hiyo anajua lazima atanyooshwa hata Kama ikibidi kwa mkono wa Chuma, atanyooshwa tu!!
 
hapa pia polisi watakuwa wamembambika wapate hela.
Sure dogo hatakuwa na hela akienda December kwao anasemwa Sana. Akadanganywa na mganga atatoka polisi pasipo kukusudia.
Afu ndani ya mwaka atakuwa bilionea atakuja kujisifu kuwa sie ni watafutaji ni matajiri.
Bila hata kujisemea tunajua ni matajiri na Wana wasomi wengi,shule ni nyingi huko kuliko kwingineko tz Ila bado ushirikina wananunua kwa gharama zozote zile.
 
Miaka 26 bado mzazi anamlisha n kumpelekea chakula chumbani,umri huo ni kulelewa wazazi ndio wanajitakia na kuleta matatizo kwenye jamii zetu...mimi 22 tu nko napambana n hom nlishahama
22 ulichelewa Sana mkuu.
Kuna huyu tajiri mwenye magari ya bestline alitoka kwao akiwa na 12yrs old.alipofikisha miaka 16 tayari anamiliki gari lake la kwanza.
Wenzako wanaanza kutoka home wakiwa around 17-19 akichelewa Sana ni 20.
Ulidekezwa Sana mkuu
 
Habari yako inaulakini.....au sijui Hawa ma journalists Wana soma vyuo gani?mwanzo jina Julias mzava....katikati ya story Ni julias masawe,majina mawili tofauti?story haijajibu maswali ya 5w and 1h.....
 
Mbona mwanzoni umesema Julias Mzava....afu katkat ya mada unasema Julias Masawe
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Julius Mzava (26) Mkazi wa eneo la usalama Chang’ombe Wilaya ya Temeke kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Magdalena Peter (56) kwa kumchoma kisu sehemu ya mwili wake.
Tukio hili limetokea tarehe 08/10/2021 saa 1:05 usiku eneo la Sandali Chang’ombe wakati marehemu(Magdalena Peter) alipoiingia chumbani kwa mtoto wake Julius Masawe(mtuhumiwa) kwa nia ya kumpa chakula na hapo ndipo aliposhambuliwa kwa kisu eneo la mwili wake akapata majeraha makubwa yaliyopelekea kupoteza kwa maisha yake licha ya jitihada za kumpeleka hospitali kufanyika.

Mtuhumiwa Julius Masawe (mtoto wa marehemu) amekamatwa, anahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani kama sehemu ya hatua muhimu za kisheria.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata na linawashikilia watu watano(5) kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vifaa vya magari na kupokea vifaa/vipuri vya magari vya wizi.
Watuhumiwa hao walikamatwa na vifaa mbalimbali vya magari zikiwemo taa za magari aina ya Toyota IST na milango ya magari ya aina mbalimbali.
Aidha, vitu mbalimbali vilivyokuwa vimeibiwa na wahalifu kwenye matukio mbalimbali ya uvunjaji vimekamatwa katika kituo cha Polisi Goba yakiwemo majenereta zaidi ya 25,vifaa mbalimbali vya ujenzi na mitungi ya gesi 10.
MULIRO J. MULIRO
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM DAR ES SALAAM
 
wafuasi wa kibwetele wamechachamaa, kama ukifanikiwa kuuona ujumbe huu basi nakuomba kibwetele wa genk uje ubadili mitazamo ya wafuasi wako,kijana 26 years bado anagonga nguna kwa mama ,kwa kweli mawazo yako yamepelekea kinywa chako kitulishe maneno ya ovyo yaliyotukaa vichwani mwetu
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Julius Mzava (26) Mkazi wa eneo la usalama Chang’ombe Wilaya ya Temeke kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Magdalena Peter (56) kwa kumchoma kisu sehemu ya mwili wake.

Tukio hili limetokea tarehe 08/10/2021 saa 1:05 usiku eneo la Sandali Chang’ombe wakati marehemu(Magdalena Peter) alipoiingia chumbani kwa mtoto wake Julius Masawe(mtuhumiwa) kwa nia ya kumpa chakula na hapo ndipo aliposhambuliwa kwa kisu eneo la mwili wake akapata majeraha makubwa yaliyopelekea kupoteza kwa maisha yake licha ya jitihada za kumpeleka hospitali kufanyika.

Mtuhumiwa Julius Masawe (mtoto wa marehemu) amekamatwa, anahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani kama sehemu ya hatua muhimu za kisheria.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata na linawashikilia watu watano(5) kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vifaa vya magari na kupokea vifaa/vipuri vya magari vya wizi.

Watuhumiwa hao walikamatwa na vifaa mbalimbali vya magari zikiwemo taa za magari aina ya Toyota IST na milango ya magari ya aina mbalimbali.

Aidha, vitu mbalimbali vilivyokuwa vimeibiwa na wahalifu kwenye matukio mbalimbali ya uvunjaji vimekamatwa katika kituo cha Polisi Goba yakiwemo majenereta zaidi ya 25,vifaa mbalimbali vya ujenzi na mitungi ya gesi 10.

MULIRO J. MULIRO
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM DAR ES SALAAM
mara Julius mzava ,mara Julius masawe
 
Back
Top Bottom