DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Nimeeleza hapojuukwamba sina tatizo na Waziri kutimiza wajibu wakekwa kufuata sheria.

Magufuli alimpongeza trafiki aliyemzodoa mke wa Balozi Dr. Waziri Mahiga, kwa minajili ya kwamba serikalihii haijali wewe mkubwa, mke wa mkubwa wala nani, hapa kazi tu. That was debatable given the proctacted circumstances,na yule mama alijaribu kujirudi na ku contain ile situation lakini ikawa too late.

Kwa hiyo, kama suala ni "hapa kazi tu" na Waziri anafanya kazi yake, nimeshasema hapo juu Makonda kakosea.

Ila mimi ni mtu wa kutaka uongozi wa old school decorum, Mzee Mwinyi anakwambia enzi zao wanasoma, mwanafunzi ukionekana unatembea barabarani huku unakula, mwalimu wako akakuona "unakula majiani", ukifika shule ni fimbo.

Kwa nini unakosa ustaarabu wa kukaa kitako ukiwa unakula?

Labda hii old schooldecorum iko out of touch na reality, lakini sisi tuliokua enzi za serikali ya Mwalimu Nyerere, tunakumbuka enzi ambayo serikali ya Tanzania viongozi walifanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, angalau machonipetu.

Kama walikuwa na beef zao, tunakuja kuzisikia wakati washatangulia mbeleya haki,kutoka kwa insiders huko.

Enzi hizo huwezi kusikia Mkuu wa Mkoa anabishana na Waziri kwenye vyombo vya habari,regardless ya nani kakosea na nani kapatia, viongozi wa serikali moja kukozana kupitia vyombo vya habari ni utovu wa nidhamu.

Serikali inaendeshwa kwa imani.

Mizozo ya viongozi wa serikali moja kati yao, ina ondoa imani ya wananchi kwenye serikali kiujumla bila kujali nani kakosea na nani kapatia.

Jay-Z aliimba katika "Takeover"

"A wise man once told me, don't argue with a fool. Cause people from a distance, can't tell who is who".

Mpango angepiga mnada tu hayo makontena bila kuzozana, tuone hiyo laana ingeanzia wapi.
 
mi naamini kama sheria za kodi haziruhusu kutoa izo mali bila kodi pia sheria izo izo zimemruhusu raisi kutoa msamaha wa kodi kwa bidhaa yoyote ile so kwanini haoni sakata hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laana imrudie mwenyewe anaedanganya mara sio makontena yake mara diaspora wamempa[emoji849]
Diaspora ipi ya kumpa vitu vya bil 10 ..
Na Bado
 
Hii ni poul Makonda not RC against wizara ya fedha sio mamlaka mbili za uteuzi kulumbana ni mamlaka v/s mtu binafsi ambaye alishapewa utaratibu lkn hajafata

Sent using Jamii Forums mobile app
That's even worse.

Waziri angemdharau na kunadi tu vitu bila majibizano mengi, kwa sababu wananchi wakiona viongozi wanajibizana, bila kujali ni mtu na taasisi au taasisi na taasisis, na nani kapatia na nani kakosea, ule mzozanotu ni negative energy inayoondoa imani ya wananchi katika serikali.

Sasa hawa watu washatengeneza uadui, kesho wakitakiwa kukaa pamoja kwa manufaa ya umma, badala ya kuanza kazi, itabidi wanze usuluhishi kwanza.

Some schoolyard mentality, sio national leadership.

Natambua Makonda ana makosa, ila nafadhaika sana viongozikuzozana regardless ya nani kakosea.

Viongozi hawatakosa kukosea, ila wakishindwa kumaliza mizozo yao kwenye vikao wakajibizana kwenye vyombo vya habari, hilo linaonesha mapungufu makubwa sana katiak uongozi wetu.
 
Msamaha wa kodi hautolewi na Rais. Japo ana uwezo huo lakini akifanya hivyo atakuwa anapeleka ujumbe mbaya kwa wasaidizi wake na wananchi pia.

Bashite alifanya kosa kuamua kuingiza hayo makonteina bila ya kufanya mawasiliano kwanza ili kujia ni kitu gani kinaweza kupata msamaha wa kodi na kipi hakiwezekani.

Ni mbaya sana kwa kipngozi yeyote au mwananchi wa kawaidia kujiaminisha kuwa Rais ni rafiki yake kiasi kwamba anaweza kufanya chochote eti kwa vile tu kitu hicho kina manufaa kwa umma.

Kuna siku watu wwtakuja kujua kuwa Magufuli hana rafiki wa kudumu bali huangalia zaidi kama unaendana naye katika mipango yake au la.

Nahisi Bashite alienda mbali mno katika kumzoea Rais. Nilishangaa siku moja rafiki yangu aliponiambia kuwa amepigiwa simu na Baba mzazi wa Bashite akitaka ampe hela na kwamba yeye ana uwezo kwa kupitia mwanae kuhakikisha biashara za rafiki yangu zinaenda vizuri. Nilimwambia rafiki yangu kuwa ampuuze, jambo la muhimu ahakikishe anaendana na sheria. Ni aheri kutengeneza faida ndogo ndani ya sheria kuliko kutajirika nje ya sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima yako boss!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwisho wa siku Philipo will be the loser. Subirini mtaona. Keep watching.. If you do not know how does double standards work, keep watching.
 
Inasemekana dab hawaivi na mzazi wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibuni tutajua nani ni kipenzi Baba
 
Dab kapoteza credibility kwa mzazi wake...ndio maana husikii zile mbwembwe zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…