Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Nimeeleza hapojuukwamba sina tatizo na Waziri kutimiza wajibu wakekwa kufuata sheria.Mkuu kwa jambo hili ipo wazi Makonda kakosea.
Anaweka vitisho kujaribu kuzuia kutekelezwa kwa sheria halali sio tamko binafsi la kiongozi flani.
Alichofanya Dk. Philip Mpango ni kwenda kuondoa wasiwasi kwa umma ili sheria ikitekelezwa basi mali ziuzike bila shida.
Hapo waziri kaenda kufanya kazi ya mawasiliano kwa umma. Angeweza kumuagiza afisa alie chini yake lakini huyo anaweza kuwa chini kiitifaki kumpinga mkubwa wake kiitifaki.
Magufuli alimpongeza trafiki aliyemzodoa mke wa Balozi Dr. Waziri Mahiga, kwa minajili ya kwamba serikalihii haijali wewe mkubwa, mke wa mkubwa wala nani, hapa kazi tu. That was debatable given the proctacted circumstances,na yule mama alijaribu kujirudi na ku contain ile situation lakini ikawa too late.
Kwa hiyo, kama suala ni "hapa kazi tu" na Waziri anafanya kazi yake, nimeshasema hapo juu Makonda kakosea.
Ila mimi ni mtu wa kutaka uongozi wa old school decorum, Mzee Mwinyi anakwambia enzi zao wanasoma, mwanafunzi ukionekana unatembea barabarani huku unakula, mwalimu wako akakuona "unakula majiani", ukifika shule ni fimbo.
Kwa nini unakosa ustaarabu wa kukaa kitako ukiwa unakula?
Labda hii old schooldecorum iko out of touch na reality, lakini sisi tuliokua enzi za serikali ya Mwalimu Nyerere, tunakumbuka enzi ambayo serikali ya Tanzania viongozi walifanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, angalau machonipetu.
Kama walikuwa na beef zao, tunakuja kuzisikia wakati washatangulia mbeleya haki,kutoka kwa insiders huko.
Enzi hizo huwezi kusikia Mkuu wa Mkoa anabishana na Waziri kwenye vyombo vya habari,regardless ya nani kakosea na nani kapatia, viongozi wa serikali moja kukozana kupitia vyombo vya habari ni utovu wa nidhamu.
Serikali inaendeshwa kwa imani.
Mizozo ya viongozi wa serikali moja kati yao, ina ondoa imani ya wananchi kwenye serikali kiujumla bila kujali nani kakosea na nani kapatia.
Jay-Z aliimba katika "Takeover"
"A wise man once told me, don't argue with a fool. Cause people from a distance, can't tell who is who".
Mpango angepiga mnada tu hayo makontena bila kuzozana, tuone hiyo laana ingeanzia wapi.