DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Nakubaliana kabisa na Wewe! Haiwezekani Mhe. Waziri uende hadharani ukapingane na RC kwa kurejerea magazeti. Hii ni laana! RC yeye kaongea na anayemwamini Kanisani na kaomba kwa atakayenunua alaaniwe na sio Serikali ilaaniwe. Sasa nini kilichomtuma Waziri kulumbana? Ama kweli naamini Vita ya Dawa za kulevya alivyoanzisha RC ni vikubwa.
 

Toka dunia iumbwe hakujawahi kuonekana mpando wa bangi ukitoa maembe.CCM,haya ndio matunda ya ku-recruit vijana waliowekeza katika ujuzi wa kusema na kupayuka hovyo hovyo.Haya ndio mapato ya kununua watu toka popote pale, iwe upinzani au toka ndani ya CCM yenyewe, ili eti waende wakakabiliane na upinzani.Kazi ya kuusambaratisha upinzani ikiisha kumalizika,kazi inayokuwa imesalia ni kama hiyo ya Makonda kudhania kwamba hapa duniani kuna kitu kinaitwa laana.
'

Na kwa kuwa Pole pole na genge lao bado hawajaelewa vizuri kuwa kuna mapato mabaya zaidi ya hili, kufikiria kwamba Mungu ana hazina ya laana anazozigawa kadri apendavyo,basi ngoja endelee kuvutia vijana wasema hovyo katika chama chao.Anavutia vijana kwenye chama wasio kuwa na meno ya kuchuja maneno bali wenye makoo ya kutapika lolote na popote!
 
Hivi mwadhani DAB alitishia "Nyau"?? Huyo Mpango ajaribu kununua limojawapo tu hata kwa pesa ya mkopo kwani akiviuza vilivyomo ndani yake atarudisha alichonunulia fasta. Hayanunuliki hata kwa robo bei. Labda wamwombe mwenye nayo ayatoe sadaka
 

Kwa hiyo,na wewe unaaamini Mungu ana hazina ya Laana ambazo Makonda kama alivyomuomba, basi atazielekeza kule Makonda anakotaka ziende? Huyo Mungu anapatikana wapi? Ni yule aliyeumba Jua linazama katika dimbwi la matope meusi au ni yupi huyo hasa?
 
Umempamba Mpango maana ni mnafiki sana! Nadhani kapewa kibali kutoka kwa boss wake au siyo Hazina? ila aache kuonea walio chini yake maana ni wengi kawachinjia baharini
 
Apige mnada kimya kimya kwa kumuogopa nani? Embu acheni kumtukuza huyu yy amekuwa nani kwenye nchi hii? Kama amekosea aambiwe live tu hakuna kumuonea haya mtu hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja Nile popcorns

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok. Naona picha linaanza.
Lakini muda mwingine tutumie busara zaidi kuliko nguvu na sheria. Kodi ya serikali inayodaiwa ni 1.2bn, ina maana hayo makontena yanathamani zaidi ya hiyo let say 3bn. Serikali inauza kontena moja kwa 60mn ili ipate pesa yake. Katika hiyo 1.2bn zitatumika katika bajeti kununulia tena hivyo vifaa vya ofisi za walimu, ambavyo vinaweza visifike wingi huo. So, nionavyo mimi, serikali ndio itakayo poteza kwa kuingia gharama kwa vitu ambavyo wamepewa bure. Pili, inawavunja nguvu hata jamaa waliochangia wakiombwa tena. Ndio maana naona inahitajika busara coz wote tunajenga nyumba moja kasoro njia tunazo tumia. Na upuuzi kama huu nilishawahi kuuona pale MOI, walitangaza mnada wa kuuza vitanda vya wagonjwa wakati palepale muhimbili kuna watu wanalala chini sababu ni taasisi tofauti japo zipo chini ya wizara moja.
Tanzania kichwa cha mwendawazimu hadi kwenye uongozi sio mpira tu.
 
Apige mnada kimya kimya kwa kumuogopa nani? Embu acheni kumtukuza huyu yy amekuwa nani kwenye nchi hii? Kama amekosea aambiwe live tu hakuna kumuonea haya mtu hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna niliposemaapige mnadakimyakimya.

Nimegundua uzi huu umetawaliwa na siasa zaidi,habari za nani amuogope nani, focus kwenye personalities.

Wakati miminaongelea collective responsibility, serikalikufanya kazi kwa sauti moja.

Naongelea vitu fulani hivi vya old schoolprinciple katika zamaambazo kuanzia wananchi mpakaviongozi wameridhika na uongozi wa vikatuni na mielekamieleka tu.

Hatuwezi kuelewana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…