DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Tena mwambie collective responsibility ktk level ya waziri ni ya cabinet ambako m/kiti ni rais, na huko RC haingii, na ndo serikali na ndo mamlaka ya juu na chombo cha juu cha maamuzi ktk serikali,who is DAB
Watu bado wanajikomba kwa DAB naona akili zao ni zile za kina LEMUTUZ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda ana genge la wafanyabiashara wanaocheza sana faulo na kufaidi matunda ya nchi hii. Wakiishapiga mipigo yao ndo wanatoa 10% ya kuzugia ambayo wanaenda kununua mifuko ya cement wanajifanya wamesaidia maendeleo ya Dar.

Siku atakayotumbuliwa Makonda ndipo ntakapochukua kadi ya CCM kuunga mkono jitihada za JPM kuleta maendeleo
 
Sijawahi kuona taifa la kipuuzi kama tz..!! Mataifa makubwa kama marekani ..uingereza...spain huwa hawapapasi macho kwenye swala la kodi awe rais hata nani...nimeshuhudia wachezaji wakubwa akina messi neymar pamoja na majina yao kidunia lakini wanapofikiwa na kesi ya kukwepa kodi huwa wanaogopa sana na kifungo kinaweza kuwapata... Sasa hapa kwetu taifa changa masikini...mkuu wa mkoa tu anawekeana misuri na waziri tena wote viongozi wa serikali..yaani makonda ambaye anatakiwa kusimamia sheria yeye ndiye anataka zipindishwe....kama anaweza kufanya hivi katika kodi tutawezaji kumuamini katika sekta nyingine..akiwa mkuu wa mkoa...
Poor tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_2018-08-27-21-24-10.jpg


Ndicho kinachoendelea!

Waziri Vs RC

- KANA -
 
Wanasema kuna maajabu ya dunia yanayopatikana katika nchi mbali mbali, ila Tanzania yenyewe ni ajabu miongoni Mwa maajabu,

Watu wanajitolea kukusanya vifaa kuwasaidia watanzania walioko katika shule zisizo na vifaa Alafu inafika bandarini eti viuzwe,??

Kama wanajali sana hela basi vinunuliwe na wizara ya elimu,

Tanzania ilivyonikatisha Tamaa mimi kuhusu michango ya kujitolea kuokoa majanga nadhani hata wengine wamekata tamaa,

Kuna rafiki yangu mtoto wa mtu mkubwa wa zamani anakaa Norwich nilipomtembelea juma lilee akanambia kuna vifaa vya hospital tuvikusanye tutume visaidie hospital za Tanzania, nisiwe mnafiki nilimjibu Tokea serikali imeleta zuruzunga kwenye Hela ya Tetemeko niliyochangia USD 400 nikidhani zitamfikia yule mama ambaye alitumika kukusanya Hela Mara matembezi masaki Mara changia bukoba, kumbe picha yake inatumika tu, sitakuja kuchangia Janga lolote Tanzania, acha wenye za kuchezea wachange,

Sasa Leo huyo jamaa yangu baada ya kusikia makontena ya makonda ya msaada yamezuiliwa ili yauzwe kanipigia moja kwa moja kwamba ulisema kweli, nami sivikusanyi

Mnakatisha wanaojitolea tamaa,
Ni bora ukatumia hela yako kuinua familia yako kuliko kuchangia Majanga ambayo serikali haithamini mchango wako,

Britanica
 
Vitendo vya Zero brain vinamchafua rais wetu.Nyerere angeshamtimua huyu RC mpenda vijizawadi
 
Muda c mrefu tutaona barua kutoka ikulu ya utenguzi WA mtu na itakuwa usiku
 
Hivi mnajua kuwa makonda ni msanii nyie? vifaa vya shule vinahitaji kutoka USA? kwani hao Diaspora wangenunua hivyo vifaa hapa hapa bongo ilikuwa inatosha kabisa tena wangekuwa wametoa ajira kwa vijana wetu wanaotengeneza hao maviti , makonda ni mpiga dili tu hata tukimsema vizuri kiasi gani, yeye ni mkuu wa mkoa misaada kama ile hata angeuliza TRA kwamba kuna mzigo wa msaada kutoka Diaspora hebu nipeni utaratibu wa kodi kabla hajawaambia kuwa leteni, futa taratibu na sharia za nchi hicho ndo Dk Mpango amesema. Eti Mpango na Makonda hata kama nikitoka usingizini siwezi hata kufikiria mara mbili kumtoa Dk mpango over Makonda ,kwa lipi amablo makonda kalifanyia hili Taifa? hakuna mtu anaeumia kama Dk Mpango, analala na kuwaza jinsi ya kukuza uchumi wa taifa hili, kila kitu unachokigusa hapo Tanzania kuanzia elimu, miundo mbinu , umeme, Dream LINER, kilimo, viwanda yanahitaji pesa, Mpango ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi yule ni mtalaam sio mpiga domo, anahitaji utulivu wa akili sio hawa kina makonda ambao wameinvest kwenye kuongea ,yaani mpango kwa hili yuko sahihi over 100%.
 
Back
Top Bottom