Hivi mnajua kuwa makonda ni msanii nyie? vifaa vya shule vinahitaji kutoka USA? kwani hao Diaspora wangenunua hivyo vifaa hapa hapa bongo ilikuwa inatosha kabisa tena wangekuwa wametoa ajira kwa vijana wetu wanaotengeneza hao maviti , makonda ni mpiga dili tu hata tukimsema vizuri kiasi gani, yeye ni mkuu wa mkoa misaada kama ile hata angeuliza TRA kwamba kuna mzigo wa msaada kutoka Diaspora hebu nipeni utaratibu wa kodi kabla hajawaambia kuwa leteni, futa taratibu na sharia za nchi hicho ndo Dk Mpango amesema. Eti Mpango na Makonda hata kama nikitoka usingizini siwezi hata kufikiria mara mbili kumtoa Dk mpango over Makonda ,kwa lipi amablo makonda kalifanyia hili Taifa? hakuna mtu anaeumia kama Dk Mpango, analala na kuwaza jinsi ya kukuza uchumi wa taifa hili, kila kitu unachokigusa hapo Tanzania kuanzia elimu, miundo mbinu , umeme, Dream LINER, kilimo, viwanda yanahitaji pesa, Mpango ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi yule ni mtalaam sio mpiga domo, anahitaji utulivu wa akili sio hawa kina makonda ambao wameinvest kwenye kuongea ,yaani mpango kwa hili yuko sahihi over 100%.