DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Kwa kauli ya RC Makonda ilipaswa afukuzwe,ameifitinisha serikali.Tukizingatie sheria sote nchi itaenda vizuri.
 
pole sana daudi bashite
 
Tueipende kuandika vitu tusivyokuwa na uhakika! Kila mtu anjua Mizigo ya nani!
 
Kunajambo limefichika ndani ya huo msaada wajuzi wanajua.
 
Hata tusingejua kama si makonda kutangaza anapigiwa mnada, unafikiri kila mnada wa makontena wanakutangazia kama ya makonda?
Hata mahakamani tunajua kesi za watu maarufu tu zinaendaje lakin za chokambaya hatujui lolote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kontena 36 za samani zitolewe hivihivi kama msaada?tena na diaspora aliyeko marekani?jamani tuache masihara.hapo kontena za msaada ni moja au mbili tu nyingine zote zingepelekwa showrooms tu.wangechukuliwa baadhi wa walimu na waandishi wa habari wapigwe picha wakigaiwa baadhi ya viti na meza mchezo uishe.sasa wanalazimisha mzigo utoke bila kulipa kodi kinyume na sheria kwa kisingizio cha msaada kwenye mashule.wanataka kuichakachua serekali mchana kweupeee
 
Hizo samani ni za nani au zinalengwa kupelekwa wapi?Msaada au?(Kuuliza si ujinga)
 
Ulitaka aagize tu anavyotaka kisa ni vifaa vya kugawa mashuleni?
Kama ni vifaa vya kugawa kwenye mashule kwanini aandike majina yake?
Alafu watu wanaongea vitu wasivyovijua ukiagiza mzigo au ukituma mzigo kwenda nje ya nchi kuna namba agency wako atajaza kuwa huu ni mzigo Wa aina gani na CPC ipi mfano kama ni mradi Wa serikali mfano kampani ya bam inayojenga jengo pale airport hawezi kuleta mavyuma tu bila kujaza CPC TRA wanakadiria kodi kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na serikali kuna hsc code za bidhaa zote sasa makonda ameagiza kwa CPC gani kwenye mzigo wake ili TRA waupitishe kama ni msaada Wa shule na je vinamsamaha Wa kodi?kwa sheria hizi na kama umeshaingizwa kwenye systems ya tancis ningumu KWA ushauri wangu kwakuwa yeye ni MTU mkubwa aombe wahisani wamchangie alipe kodi kama utaratibu ulivyo KWA maana kila siku storage inaongezeka na siku nyingine kabla hajaagiza aonane na wahusika wampe maelekezo kabla
 
Hivi hata viti, meza na kabati tunaagiza toka nje wakati humu Nchni kuna samani nzuri na imara zinatengenezwa na vijana wetu mitaani, Hao diaspora wangekupa Fedha ungenunua hapa nchini kuliko kununua mabox toka ng'ambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mimi nilijuwa mkiwa nje mnakuwa na akili lakini kumbe hovyo tu, ukiwa unachangia lazima ujue unachangia kwenye Taasisi gani . Unamchangia Bashite then unakuja kusema vifaa vya watoto mashuleni. TRA kazia humo humo
 
Hicho kisa cha kula barabarani umenikumbusha mbali.

Nikiwa shule ya bweni kidato cha tano mwalimu wangu mmoja alitukuta njiani tunakula 'pears' alitusimamisha kwa hasira karibu atupe adhabu.

BTW, Nakubaliana na busara uliyo shauri kuhusu mgogoro wa Makonda na Waziri. Kama ulivyosema ilikuwa njia mbaya iliyotumiwa na waziri.

Nadhani ilichochewa na historia ya Makonda kuhusishwa na minong'ono ya kuwa anaogopwa na mawaziri na analindwa na mamlaka zilizo mteua na kwamba yeye huamua chochote bila hofu ya kutumbuliwa.
Sasa wahusika wakaona kuzima kelele haraka bora waziri awahi kumkosoa.

Tukio lilisha trend kwenye vyombo vya habari tayari. Hii ndio athari ya siasa zetu za kibongo zinaamua mambo mangi ndivyo sivyo kuogopa wanasiasa au kuwapatia umaarufu wanasiasa usio wa faida kwa taifa.
 
Haiwezekani mtu mmoja atumie mgongo wa madaraka kukwepa kulipa Kodi kisa ukuu wa Nkoaaa tuone sasa Jiwee atamtetea kwa hilii...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jiongeze badala ya kukurupuka kuandika thread. Makontena yalikuwa 36 kwa jina binafsi. Yote yaliombewa kufutiwa kodi. Iliposhindikana, akayalipia makontena 16 kwa fedha binafsi. Mpaka Leo hayajulikani yapo wapi. Yaliyobaki, 20, ndiyo tunapigiana kelele zisizo na msingi humu ndani. Achana na jambazi huyu. Kama mlichangia mliingizwa choo cha kike. Mlipaswa mjiulize kwanini michango yenu inasafirishwa kwa jina binafsi. Na kwanini kwanza aliyakataa hayajui?!?! Mlitumika kama mradi binafsi bila hata Wizara ya Elimu kujua au mamlaka za mkoa kutaarifiwa. Sasa kaeni kimya mkijutia uzumbukuku mlioufanya kwa kuzidiwa akili na Form Four Failure.
 
Tumesikia hivi karibuni sakata la makontena ya Mh Makonda.

Sakata lilianza mnamo Februari mwaka huu kwa kuyapokea makontena hayo mbele ya vyombo vya habari kule bandarini.

Lilipokuja swala la kodi mnamo mwezi wa nne au tano hivi, Makonda aliyakana MBELE YA VYOMBO VYA HABARI kuwa na yeye nado kwanza anayasikia!

Tukumbuke mapema, Mkuu wa nchi alimhimiza apige kazi kwenda mbele!

TRA wakakomaa na mnada, makontena bei ikawa juu ya viwango, hivyo hayakununulika.
Jumapili hii Makonda kaenda Kanisani( na siyo TRA) kuyaombea laana kwa atakayeyanunua!
~Mbele ya vyombo vya habari!

Hapa nikachoka!
Uongo ukawa dhahiri, makontena sasa ni yake na Makonda alitaka kukwepa kodi.

Na sasa anatumia ushirikina(sijui kanisa linalotoa laana kwa utendaji wa Serikali).

Haya ndo matokeo ya kuweka mtu kwenye madaraka makubwa huku kichwani ni patupu.
 
Huyu kiumbe alitakiwa awe makini sana ili kuprove wrong kuwa si kweli kuwa ana vyeti vya kufoji na hatumii jina lake

Lakini kila siku zinavyosonga anaonyesha ni kweli kichwani hamna kitu alafu alitakiwa awe mtulivu sana pia alitakiwa kusoma alama za nyakati mapema wakati anajua kabisa anaishi kwa kubebwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mi naamini kama sheria za kodi haziruhusu kutoa izo mali bila kodi pia sheria izo izo zimemruhusu raisi kutoa msamaha wa kodi kwa bidhaa yoyote ile so kwanini haoni sakata hili

Sent using Jamii Forums mobile app
Pengine wakubwa wamehisi hizo samani sio zote zinaenda kusaidia kwenye elimu.

Inaweza kuwa wafanyabiashara flani wanapitisha vitu kwa mgongo wa makonda.

Kwanini havikuletwa kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam badala ya jina binafsi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…