DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Watanzania wengi ni vichaa kweli haiwezekani mtu atumie cheo chake vibaya afu anajitokeza mtu kupongeza hivi kila kiongozi akisema aingize makontena labda ya computer nchini kugawa shuleni na TRA isimtoze kodi nchi itaenda kweli tuache upimbi tusisingizie misaada ili tujinufaishe.
 
Alisema atawashitaki TRA kwa baba yake kumbe bado.
Ni baba gani anaye entertain wakwepa kodi? Makontena yamekuja kwa jina la mwana mpendwa wa baba, alipe tu. Yangekuja kwa jina la WALIMU nadhani serikali ingeelewa!
 
Mkuu usiwe na akili ya Makonda.ushirikina siyo dili, na serikali ina taratibu zake.

Kwanza HAKUNA KANISA LINALOTOA LAANA!
Hilo uelewe.
Pili, fuata sheria maana hata dawa za wagonjwa zina kodi zake.
Mtunusitake kugundua uchochoro wa kuingiza bidhaa bila kulipa kodi.
Ujanja uliotaka kutumika na Makonda ni ujanja wa kizamani sana, na uchochoro huo ulisha zibwa.
Hiyo mizigo wala si ya Makonda maana kwanza akiwa kijana mdogo wa kuanza kazi juzi , hana mtaji wa marafiki wa kumtolea makontena 20, na vile vile hana mtaji wa fedha za hizo kontena.
Rushwa si lazima iandikwe usoni, haya ya Makonda ndo dalili zake.
 
Mwaka 1997 Tanzania iliamua kukua kufikia uchumi wa kati kwa kutengeneza dira ya maendeleo ya Taifa 2025. Mpaka sasa tuna takribani miaka 7 tu imebakia ili kuona realization ya njozi ikiwa dhahiri katika maisha ya Watanzania.

Binafsi natambua mara kwa mara tunahimazana kuwa wazalendo. Na uzalendo tafsiri yake imekuwa na mkanganyiko kwelikweli. Ila ukikaa na wanajeshi ukawauliza, utaelewa tafsiri ya uzalendo kwa vitendo. Wamarekani au Wa-Israel hali kadhalika, unawaelewa, ila sisi… huenda tunahitaji kuwekewa mikono… Mungu tusaidie.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kaja na mpango mahsusi wa kuhakikisha anatoa mchango wake kwa vitendo ile kuboresha elimu mkoani Dar es Salaam. Amejenga madarasa, nyumba za walimu, ofisi za walimu na kupata uhakika wa madawati ya kutosha. Wasamalia wema wamempatia madawati na viti vya walimu mara vitu vimekwama toka Januari, leo hii ni tunakaribia kabisa kufika September, baadooo havijatoka.

Waziri Mpango kwa nia njema na vijana wake wa mamlaka ya mapato nao wanataka kodi. Toka Januari mpaka leo kama hela hajalipwa tafsiri rahisi bajeti ya kulipia haikuwepo ndiyo maana Paulo Makonda aliomba msamaha wa kodi. Waziri na vijana wake wanazingatia sheria na taratibu za ki-kodi.

Kuna sheria duniani nzuri na mbaya, ila zote zinabaki kuwa sheria katika dunia hii hii. Kuna bilioni 133 ya EPA zilitoka BOT 2005 kwa mujibu wa taratibu. Baadae ikaonekana ni wizi ulifanyika. Ila mpaka zinatoka, hakuna polisi aliekama mtu, “huenda sheria ilizingatiwa”. Sote pia tunakumbuka mabilioni ya ESCROW yalitoka BOT, hapo napo bila shaka kuna sheria na taratibu zilifuatwa mpaka yakalipwa.

Leo walimu wanahitaji viti na meza kama vitendea kazi. Kwa kuwa sheria hajafuatwa (maana furniture sheria hajatamka zinapaa msamaha wa kodi) pamoja na nia njema ya aliefanya initiatives, yet, kuna kukwama. Je tunaijenga Tanzania kuelekea dira ya maendeleo ya Taifa 2025?

Kodi kama italipwa, sehemu ya kodi hiyo hiyo mbona ndiyo itanunua viti na meza hizo hizo. Tunajenga nyumba moja Tanzania yet tunagombania fito.

Hii yanikumbusha habari ya taasisi moja ilianza mwaka 2009 na mtaji wa USD 100 mil nchi zaUlaya mashariki. Mwaka huu (miaka 9 baadae) hao jamaa wamekwenda nchi nyingine na uwekezaji kama huo huo kwa mtaji wa zaidi ya USD 2 bilion.

Kuna Mtanzania namfahamu ana model ya mradi kama hao jamaa wa Ulaya Mashariki, anataka kuleta uwekezaji wa mradi na technology ili kutengeza bidhaa katika ubora kwa soko la ndani na nje. Kwa projection, mradi huo utaanza na ajira za Watanzania 100+ na kwa mwaka malipo ya kodi yakawa kati ya billion 15 na kuendelea. Achilia mbali manunuzi ya huduma mbalimbali za kiwanda hicho kama vile maji, umeme na tozo za huduma kama TFDA, TBS, GS1 na ambazo zitaingia serikalini.

Mradi huu utakuwa mchango pia kwa vituo vya utafiti Ukiriguru na vituo vingine vinavyojihusisha na kilimo achilia mbali ku-replicate out-growers scheme.

Mradi huu wa uwekezaji ukiuza mauzo ya nje ya bidhaa kwa kuwa unatumia technology ya kisasa kwenye soko la mazao ya Kilimo AGOA Marekani, kuna fursa za hela ya kigeni kuingia nchini pia.

Sheria na taratibu ambazo zaweza kufanyiwa kazi kujenga ushirikiano kufanikisha lengo, unachelewesha jambo zuri kufanyika.

Jana Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji amewataka “wakubwa” kushirikiana na wawekezaji kuijenga Tanzania. Imeonekana kuna “wakubwa” kuwabalasa baadhi ya wawakezaji Tanzania hii hii.

JPM amejipambanua anataka twende mbele, ila wasaidizi wake ndiyo hivyooo kama tulivyoona Waziri na Mkuu wa Mkoa, Director wa TIC na baadhi ya wakuu wa Wilaya na Mikoa.

Adui yetu Tanzania ni Ujinga, umasikini na maradhi.Kama sheria, sera na taratibu zinatuchelewesha, hizo sheria, sera na taratibu zinatufaa kweli.

JPM alinunua ndege mpya kwa cash, baadhi wakamzodoa, oohhh, Rais kanunua ndege bila kuzingatia sheria za manunuzi ya umma. Je, lengo ni kunua ndege au sheria ya manunuzi ambayo inaweza kuchelewesha mambo na wakati mwingine kuongeza gharama kwa jina la “mchakato”.

Nazipenda sheria na taratibu. Ila sheria zingine ni mbaaaya. Badala ya kututumikia twende mbele zinatuchelewesha.

Tunaipenda Tanzania. Tukiwa wazalendo kweli, tutashirikiana kwa nia njema kwenda mbele kuijenga Tanzania badala ya kukwamishana kwa jina la sheria na taratibu.Tunawajibika moja kwa moja kulenga kumtumikia Mtanzania kwa kushindana na maaduni Umasikini, ujinga na maradi. Wazalendo huwa wana-eliminate maadua with it take. Sisi hivi tunatumia strategy ipi
 
Ni vizuri wangezikabizi wizara ya Elimu.
Okay badala ya kuuza.....nadhani hata yeye alizungumzia hivyo though yeye lengo la kwanza ni kodi then ikishindikana ndo wanagawa kwa mujibu wa taratibu watazoziweka....ila nimeona vitu vingi ni viti vile vya kuzunguuka au macho yangu?
 
Okay badala ya kuuza.....nadhani hata yeye alizungumzia hivyo though yeye lengo la kwanza ni kodi then ikishindikana ndo wanagawa kwa mujibu wa taratibu watazoziweka....ila nimeona vitu vingi ni viti vile vya kuzunguuka au macho yangu?
Sasa hapo ni vizuri tukamuambia Mkuu wa mkoa aiondoe laana kwenye bidhaa.
 

Sina hakika kama tatizo hapa ni elimu duni...nadhani inawezekana ni arrogance ya mtu...arrogance huwa haina elimu --unaweza ukawa na elimu lakini mtu akabaki kuwa ni arrogant...mwenye elimu duni naye anaweza kuwa arrogant kwa namna yake...sitaki kwenda kwa undani zaidi zaidi kuhusu suaka hili la makontena, lakini niwazi nadhani JPM anapata taabu sana katika teuzi zake mbalimbali...Kama sakata hili la makontena ni la kweli kumhusu huyu anayetajwa then ipo shida kubwa katika baadhi ya watendaji wa serikali.....
 
Either you are missing a point or intentionally trying to fool folks. Hivi nyie wazushi wachache ndo wa kulalamika mnavunjwa moyo? Umetaja Norwich kwahiyo I'm assuming una affiliation na UK. Hivi hukumwona Penny Mourdant akikabidhi mabilioni kwa Magufuli couple of weeks ago? Yes, kama nchi wahisani hazitafsiri ukwepakodi wa Bashite ni kuwaamgusha, who the hell are you vibaraka wa Makonda kutuzuga?

Makonda ni mkwepa kodi. Period. Na kama ambavyo charities UK zinapaswa kuijulisha HMRC kwa minajili ya tax exemption, so was huyo mtu aliyefoji jina na cheti cha kidato cha nne.

Anayevunjwa moyo ni Waziri Mpango, kwa sababu hata asingetolea ufafanuzi kuhusu suala hilo, Bashite alishayakana makontena hayo kisha sijui akawashwa na nini, akadai hakuna wa kuyazuwia, yet sasa yanapigwa mnada.

Huu ni mwanzo wa mwisho wa Bashite, na nyie wapambe wake mjiandae kisaikolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mpango is going to calm.. Bashite ana nyota ya kuhurumiwa. Nachukua nafasi hii kumtaka mpango akae mbali na suala hili... Hakuna mwanadamu anaetafuta laana maadam alert ishatolewa nakwambia no body will dear to buy..Mpango achana na hilo suala maana kama kupga mnada tu watu hawajafka bei kabla ya kiapo cha laana then what do you expect.... "kama shetani anaweza kulaani kwanini mnabeza laana ya makonda?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…