Mwaka 1997 Tanzania iliamua kukua kufikia uchumi wa kati kwa kutengeneza dira ya maendeleo ya Taifa 2025. Mpaka sasa tuna takribani miaka 7 tu imebakia ili kuona realization ya njozi ikiwa dhahiri katika maisha ya Watanzania.
Binafsi natambua mara kwa mara tunahimazana kuwa wazalendo. Na uzalendo tafsiri yake imekuwa na mkanganyiko kwelikweli. Ila ukikaa na wanajeshi ukawauliza, utaelewa tafsiri ya uzalendo kwa vitendo. Wamarekani au Wa-Israel hali kadhalika, unawaelewa, ila sisi… huenda tunahitaji kuwekewa mikono… Mungu tusaidie.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kaja na mpango mahsusi wa kuhakikisha anatoa mchango wake kwa vitendo ile kuboresha elimu mkoani Dar es Salaam. Amejenga madarasa, nyumba za walimu, ofisi za walimu na kupata uhakika wa madawati ya kutosha. Wasamalia wema wamempatia madawati na viti vya walimu mara vitu vimekwama toka Januari, leo hii ni tunakaribia kabisa kufika September, baadooo havijatoka.
Waziri Mpango kwa nia njema na vijana wake wa mamlaka ya mapato nao wanataka kodi. Toka Januari mpaka leo kama hela hajalipwa tafsiri rahisi bajeti ya kulipia haikuwepo ndiyo maana Paulo Makonda aliomba msamaha wa kodi. Waziri na vijana wake wanazingatia sheria na taratibu za ki-kodi.
Kuna sheria duniani nzuri na mbaya, ila zote zinabaki kuwa sheria katika dunia hii hii. Kuna bilioni 133 ya EPA zilitoka BOT 2005 kwa mujibu wa taratibu. Baadae ikaonekana ni wizi ulifanyika. Ila mpaka zinatoka, hakuna polisi aliekama mtu, “huenda sheria ilizingatiwa”. Sote pia tunakumbuka mabilioni ya ESCROW yalitoka BOT, hapo napo bila shaka kuna sheria na taratibu zilifuatwa mpaka yakalipwa.
Leo walimu wanahitaji viti na meza kama vitendea kazi. Kwa kuwa sheria hajafuatwa (maana furniture sheria hajatamka zinapaa msamaha wa kodi) pamoja na nia njema ya aliefanya initiatives, yet, kuna kukwama. Je tunaijenga Tanzania kuelekea dira ya maendeleo ya Taifa 2025?
Kodi kama italipwa, sehemu ya kodi hiyo hiyo mbona ndiyo itanunua viti na meza hizo hizo. Tunajenga nyumba moja Tanzania yet tunagombania fito.
Hii yanikumbusha habari ya taasisi moja ilianza mwaka 2009 na mtaji wa USD 100 mil nchi zaUlaya mashariki. Mwaka huu (miaka 9 baadae) hao jamaa wamekwenda nchi nyingine na uwekezaji kama huo huo kwa mtaji wa zaidi ya USD 2 bilion.
Kuna Mtanzania namfahamu ana model ya mradi kama hao jamaa wa Ulaya Mashariki, anataka kuleta uwekezaji wa mradi na technology ili kutengeza bidhaa katika ubora kwa soko la ndani na nje. Kwa projection, mradi huo utaanza na ajira za Watanzania 100+ na kwa mwaka malipo ya kodi yakawa kati ya billion 15 na kuendelea. Achilia mbali manunuzi ya huduma mbalimbali za kiwanda hicho kama vile maji, umeme na tozo za huduma kama TFDA, TBS, GS1 na ambazo zitaingia serikalini.
Mradi huu utakuwa mchango pia kwa vituo vya utafiti Ukiriguru na vituo vingine vinavyojihusisha na kilimo achilia mbali ku-replicate out-growers scheme.
Mradi huu wa uwekezaji ukiuza mauzo ya nje ya bidhaa kwa kuwa unatumia technology ya kisasa kwenye soko la mazao ya Kilimo AGOA Marekani, kuna fursa za hela ya kigeni kuingia nchini pia.
Sheria na taratibu ambazo zaweza kufanyiwa kazi kujenga ushirikiano kufanikisha lengo, unachelewesha jambo zuri kufanyika.
Jana Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji amewataka “wakubwa” kushirikiana na wawekezaji kuijenga Tanzania. Imeonekana kuna “wakubwa” kuwabalasa baadhi ya wawakezaji Tanzania hii hii.
JPM amejipambanua anataka twende mbele, ila wasaidizi wake ndiyo hivyooo kama tulivyoona Waziri na Mkuu wa Mkoa, Director wa TIC na baadhi ya wakuu wa Wilaya na Mikoa.
Adui yetu Tanzania ni Ujinga, umasikini na maradhi.Kama sheria, sera na taratibu zinatuchelewesha, hizo sheria, sera na taratibu zinatufaa kweli.
JPM alinunua ndege mpya kwa cash, baadhi wakamzodoa, oohhh, Rais kanunua ndege bila kuzingatia sheria za manunuzi ya umma. Je, lengo ni kunua ndege au sheria ya manunuzi ambayo inaweza kuchelewesha mambo na wakati mwingine kuongeza gharama kwa jina la “mchakato”.
Nazipenda sheria na taratibu. Ila sheria zingine ni mbaaaya. Badala ya kututumikia twende mbele zinatuchelewesha.
Tunaipenda Tanzania. Tukiwa wazalendo kweli, tutashirikiana kwa nia njema kwenda mbele kuijenga Tanzania badala ya kukwamishana kwa jina la sheria na taratibu.Tunawajibika moja kwa moja kulenga kumtumikia Mtanzania kwa kushindana na maaduni Umasikini, ujinga na maradi. Wazalendo huwa wana-eliminate maadua with it take. Sisi hivi tunatumia strategy ipi