DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Mkuu tumekuwepo nchini muda mrefu sana na tunaweza kumtambua mwanasiasa mwizi kwa mbali sana.
Njia ya kijinga na ya kwanza ni mwanasiasa kujidai ana uchungu sana na kada fulani ya watu masikini, wakati hasa ni kupiga cha juu.
Hiyo huruma ni changa la macho.
Makonda huyu huyu ambaye majuzi(less than 10 years) alikuwa hana kitu, leo ana ma VX, BMW na mali za kutisha, na baadaye anawaagizia wananchi wake makontena zaidi ya 20 ,samani za shule?

Mtu ukipumbazika na hilo, basi una matatizo ya kimsingi.

Hela isiyopatikana kihalali daima kama jipu, linajitokeza ili lipasuke.
 
Ile ni Misaada Tu kapewa na watz waisio marekani sio hela yake. Walichukua used furniture na kumsaidia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wenye matatizo ya msingi ni aina yako ya watu. Kwa hiyo hata lile suala la matibabu ya wachina pale bandarini ilikuwa ni siasa ya kudanganyia umma?.

Kwa hiyo hata suala la kutetea haki za kinamama waliotelekezewa watoto na lenyewe ni jambo la kisiasa?.

Hakuna wa kukulazimisha kwamba lile ninalowaza mimi ni lazima liwe ndio hilo hilo kichwani mwako.
 
Ile ni Misaada Tu kapewa na watz waisio marekani sio hela yake. Walichukua used furniture na kumsaidia

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa asingeiagiza km paul, angetumia mashirika yasiyo ya kiserikali kuingiza mizigo ambayo ni misaada, sheria inabana na imeainisha waziwazi hamna msaada wa kodi kwa watu binafsi iwe au isiwe kwa manufaa ya jamii, ndo kosa lilipofanyika hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unamuonea bure Makonda,serikali ya Magufuli ina ma professor kibao wanaofanya madudu
 
Nenda nchi za walizoendelea ambako sheria ni msumeno uone kama utafanya usanii aliofanya makonda halafu upewe makontena bila kulipa kodi.
Kudaiwa kwake means hakufata sheria za msamaha yeye ni nani asilipe kama wengine wanalipa? On top of that it doesn’t seems hayo makontena yana vifaa vya shule tu, kuna zaidi, plus uongo kuwa diaspora wamempa, diaspora ipi? Hii mnayosema wanabeba mabox watoe msaada wa vitu vinavyo worth kodi bil 21?? Gerarahia!
 
Ile clip ya gwajima kuwa anmdelete! Ndio imekuwa kweli?
 
Yeah ..... wALIZIOKOTA, HALAFU ZIKASAFIRI KWA KUTUMIA UNGO AU UFAGIO WA CHELEWA ZA MNAZI?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] cha muhimu aitishe "harambee" aanzishe namba ya simu labda 155484 tutume buku au jero au mia mia, ili mwisho wa siku tupate kodi yetu, huku aombe nyongeza na kusitisha mnada wakati tunakusanya hizo pesa, easy, sasa kulialia kama vile tunaonewa.

Mbona watu wanacheza sana bahati nasibu, aanzishe namba ya kampuni watu wachangie buku au jero au hata sh mia. Fasta,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unaelewa mchakato mzima uliotumika kuzipata hizo samani?
 
Bora fenicha za watanzania,, tungepata hela za mbao, misumali, nyundo, gundi pamoja na kodi hela za kigeni tumezikosa na kodi tena tuzikose aah! Makonda Hakuna laana hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…