DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Tusiangalie nani sababu ya huo msaada.bali tuangalie msaada una faida gani.
kuna watanzania wengi wapo huko ughaibuni wanapenda kuisaidia nchi yao.ila haya masuala ya kodi ndo yanawaumiza.
Haiwezekani MTU atoe msaada alaf umwambie alipe kodi.kwani ni Mali yake?au anakwenda kuuza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria iko wazi. Ameagiza kama makonda anatakiwa alipe kodi km makonda, angeagiza km shirika lisilo la kiserikali au shirika la kiserikali linalohusiana na kutoa misaada kwa jamii lisingetokea swala la kudaiana kodi. So anatakiwa awe mbunifu km alivyokuja watz wamchangie kodi, au lasivyo Diaspora na sisi tuchange ipatikane ila kutoka bila kulipwa pale nadhani itaamsha hisia nyingi kwa wanaolipa kodi bandarini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili la Makontena ya Makonda , sidhani kama waziri mpango kajichukulia hatua, ni lazima alishauriana na Raisi na akapewa GO AHEAD.

Sasa hawa vibaraka wa Makonda wanajisumbua nini, na wao na Makonda wajue kuwa kila wanvyozidi kupinga na kuropoka ovyo, wanapinga na kukejeli amri ya Raisi Magufuli .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sheria, fata tu sheria. Usiipige teke sheria ili ujifanyie mambo yako afu ulalamike baadae, sheria inakuelekeza jinsi ya kuingiza misaada nchini, ukienda tofauti usilie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao watanzania waliopo nje wanaopenda ķusaidia wafuate sheria kama hawataki lipa kodi.

Hili tukio liwe funzo kwao
 
Utakuwa mwizi tu, kwani hukufuata taratibu wa kisheria wewe ni ndani kwanza week tatu ndo mahakamani, baadae utawekewa dhamana ya hao uliotaka kuwapa hiyo nia njema yako, kwa kifupi ni kufuata sheria zilizopo Kama hazifai tuombe bunge lizibadilisha ili nia njema ziende kisheria. Makonda hoye, shule hoye, Jodi hoye, Mpango hour.
 
Naona kiza kinene! Mgongano wa sheria na kiu ya maendeleo. Katika hali yoyote ile sheria lazima ichukue mkondo wake. Vinginevyo itafika wakati tutafanya mambo kila mtu atatushangaa. KUMBUKA; hivi juzi wakati Mhe. Rais akisifia ukusanyaji wa mapato kwa Jiji la Dodoma alisema Dar imeshindwa na Dodoma sijui nimchukulie hatua RC au kwa namna yoyote ya matamko aliyotumia alikuwa haridhishwi na kasi ya ukusanyaji wa kodi Dar. Sasa limekuja hili la vifaa vya shule Vs kulipiwa kodi. Mbona tunaangalia upande mmoja tu wa sarafu? Jamani sarafu inazo pande mbili. Lazima zitazamwe zote kwa wakati mmoja. Kila mtu sasa anaogopa kutumbuliwa. Sio MAKONDA wala sio MPANGO. Tuwaangalie wote wawili kwa jicho linaloona sawa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…