DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

ya apa inatakiwa ufikirie mbal ndio utatoa jibu sahihi ..first ujue sheria inasemaje ya ushuru. alichokifanya waziri alimuliza kamisha wa TRA sheria inasemaje,akafanunua kuwa iwe selikari ya mitaa au selikari kuu ikiagiza vitu inatakiwa ilipe ushuru, kwa hyo ata kipindi anagiza hivi vifaa ilibid atoe taarifa selikarin kuwa kuna amepata ufadhiri wa vifaa vya shule lkn itakuwaje kuhusu ushuru? kwa hyo selikari kupitia wizara ya elimu ingejadili hyo jins gan ya kufanya. Lkn ye akafanya yeye kama yeye wakat anajua kabisa nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria alafu ww unakuwa wa kwanza kuvunja sheria ..hii n sawa na kusema kwa vile ile ni hospital ya selikari bas isilipe bil za umeme kwa shirika la tanesco sasa mbona nchi itakuwa inaendeshwa kienyeji...na wazili kasema hivi vi2 vitauzwa na ela itaenda selikarin itafanya kaz ile ile ya huduma za jamii au wakishindwa watazigawa sehem tofaut tofaut sio 2 dsm wanafunzi na walim ni wa watanzania wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani umemaliza kabisa mkuu! Elimu ikiwa kwa kiwango kidogo kuliko hitaji husika haya ndo matatizo yake; nimejifunza kuwa siku zote elimu ya kutosha inakufanya ujue kuwa kuna mengi mno ya kujua na hivyo kukufanya uwe mnyenyekevu na makini katika kuweka akiba, ikiwemo ya maneno.

Kwa bahati mvaya sana DAB, akuzingatia mashauri ya Sulemani katika Mithali 4:13 na kama kubadilisha jina kumeshindwa kumhekimisha hakuna kanisa litakalomsaidia kufikia malengo yake kwa mbinu dhalimu.

Kilichokaki ni kurudi na kubembeleza mamlaka ya uteuzi; labda kuna maajabu yatakayowezekana.

Pole nyingi kwa DAB lakini uzuri ni kwamba anaendelea kujifunza, japo kwa njia ngumu kuwa mara nyingine mbeleko inaweza kuwa ngumu sana kupatikana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilivyokuwa Makonda alienda kwenye nyombo vya habari akaomba watu wa nje tutume vifaa alisema kwenye media sio hata siri na akasema lini vitafika watu wa pale Washington state walijua vifaa vinaenda kusaidia watoto na mkuu wa mkoa aliomba viwe kwa jina lake ili asaidie sehemu ambayo haina vifaa lakini kosa lake lisije ku cost watoto wangemtafuta mtumaji ambaye ni Mtanzania ! Kabla ya mnada na angeweza kubadilisha jina

Ficha ujinga wako, vifaa vya walimu na watoto vije kwa jina lake ili iweje? Kama kuna waliochanga ili hali wanajua kuwa vinakuja kwa jina la bashite jua hao ni mazwazwa zaidi ya bashite mwenyewe
 
watu tu hawampendi makonda.. ila kuuza meza za walimu ni wehu
Wapi ziimeandikwa "Meza za Walimu?" sisi tunajua ule mzigo ni wa GSM! Walimhonga vigari,wakamuhonga hisa kwenye kampuni yao,wakamkarabatia ofisi na kumweka samani kama hizo zilizoko kwenye ma container bandarini! Kwa hiyo zile Container ni za GSM na yeye ni mmoja wa wamiliki wa GSM! Alipe kodi aache kutuma vibaka kuja kutetea huku!
 
Hivi kwani kodi anayotakiwa kulipa mh RC kwa hayo makontena ni shilingi ngapi kwanza ?
Si tuliambiwa ana hela sana huyu mtu...!
Yeye si ana marafiki kibao wenye uwezo....!
Pengine alistahili kuandika barua ya kuomba msamaha Wa kodi kweli, lakini baada ya kukataliwa sidhani kama alipaswa "kulialia" namna hii....
wanalaumu bure wafanyabiashara kwenye suala ka kodi; kumbe hata wanaoimba tulipe kodi nao hawataki kulipa!

lakin la pili; furniture za nje kod yake juu sana!
ukinunua mnadan kodi yake ni 77%
yaan kama ulinunu kwa 10 milion, TRA wanakudai ulipe 7.7milion ziada
 
Huyu mzee hana akili , kwahiyo anamaanisha serikali itajenga madarasa na ofisi za walimu .mbona haijajenga mpaka makonda ndiye kajenga

Sent using Jamii Forums mobile app
order ya serikali imetoka, anatokea mtu anaipinga hadharani, nani yuko juu kati ya mkuu wa mkoa na waziri, what if kila mkuu wa mkoa apate msaada wa kontainer 36 za samani! baadae magari ya shule, baadae simenti za kujengea madarasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM oyeee
400-08055661en_Masterfile.jpg
 
Ilivyokuwa Makonda alienda kwenye nyombo vya habari akaomba watu wa nje tutume vifaa alisema kwenye media sio hata siri na akasema lini vitafika watu wa pale Washington state walijua vifaa vinaenda kusaidia watoto na mkuu wa mkoa aliomba viwe kwa jina lake ili asaidie sehemu ambayo haina vifaa lakini kosa lake lisije ku cost watoto wangemtafuta mtumaji ambaye ni Mtanzania ! Kabla ya mnada na angeweza kubadilisha jina
Mwanzoni si alivikana? Una kipi cha kusema kuhusu hili?
 
Wanasema kuna maajabu ya dunia yanayopatikana katika nchi mbali mbali, ila Tanzania yenyewe ni ajabu miongoni Mwa maajabu,

Watu wanajitolea kukusanya vifaa kuwasaidia watanzania walioko katika shule zisizo na vifaa Alafu inafika bandarini eti viuzwe,??

Kama wanajali sana hela basi vinunuliwe na wizara ya elimu,

Tanzania ilivyonikatisha Tamaa mimi kuhusu michango ya kujitolea kuokoa majanga nadhani hata wengine wamekata tamaa,

Kuna rafiki yangu mtoto wa mtu mkubwa wa zamani anakaa Norwich nilipomtembelea juma lilee akanambia kuna vifaa vya hospital tuvikusanye tutume visaidie hospital za Tanzania, nisiwe mnafiki nilimjibu Tokea serikali imeleta zuruzunga kwenye Hela ya Tetemeko niliyochangia USD 400 nikidhani zitamfikia yule mama ambaye alitumika kukusanya Hela Mara matembezi masaki Mara changia bukoba, kumbe picha yake inatumika tu, sitakuja kuchangia Janga lolote Tanzania, acha wenye za kuchezea wachange,

Sasa Leo huyo jamaa yangu baada ya kusikia makontena ya makonda ya msaada yamezuiliwa ili yauzwe kanipigia moja kwa moja kwamba ulisema kweli, nami sivikusanyi

Mnakatisha wanaojitolea tamaa,
Ni bora ukatumia hela yako kuinua familia yako kuliko kuchangia Majanga ambayo serikali haithamini mchango wako,

Britanica
hivyo vifaa angevileta kwa jina la wizara ya elimu au kwa jina la ofisi ya mkuu wa mkoa na si jina lake shida ndo inaanzia hapo ,mwambie alipe ushuru tu !
 
Mimi ni mpenzi wa somo la sheria,sishabikii sheria kupindishwa
Sheria ya kodi imempa waziri wa fedha maguvu ya kusamehe kodi bila hata kuliarifu bunge,ndio maana kuna mawaziri waliwahi kudondoka kwa kuitumia sheria hiyo vibaya
Hapa huwezi kumuona mtu kama Zitto,yeye anasubiri magufuli tu ,aweze kutweet
Mkuu nina shaka na upenzi wako wa somo la sheria, kuna kifungu kipi kinampa waziri nguvu za kusamehe kodi kwenye samani? Nimesikia waziri akisema samani inabidi zilipiwe kodi kwa mujibu wa sheria.
 
Huuu ni mchezo tu wananchi tunachezewa akili hapo hamna lolote.Sema wanatataka kutufanya tukae attention kusikiliza kitachompata makonda tuache kujadili mambo ya msingi.Huyu ni mkuu wa Mkoa na Huyu ni Waziri na wote wanaishi Dar na Boss wao ni mmoja hapo kuna ABLAKADABLA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom