DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Wanasema kuna maajabu ya dunia yanayopatikana katika nchi mbali mbali, ila Tanzania yenyewe ni ajabu miongoni Mwa maajabu,

Watu wanajitolea kukusanya vifaa kuwasaidia watanzania walioko katika shule zisizo na vifaa Alafu inafika bandarini eti viuzwe,??

Kama wanajali sana hela basi vinunuliwe na wizara ya elimu,

Tanzania ilivyonikatisha Tamaa mimi kuhusu michango ya kujitolea kuokoa majanga nadhani hata wengine wamekata tamaa,

Kuna rafiki yangu mtoto wa mtu mkubwa wa zamani anakaa Norwich nilipomtembelea juma lilee akanambia kuna vifaa vya hospital tuvikusanye tutume visaidie hospital za Tanzania, nisiwe mnafiki nilimjibu Tokea serikali imeleta zuruzunga kwenye Hela ya Tetemeko niliyochangia USD 400 nikidhani zitamfikia yule mama ambaye alitumika kukusanya Hela Mara matembezi masaki Mara changia bukoba, kumbe picha yake inatumika tu, sitakuja kuchangia Janga lolote Tanzania, acha wenye za kuchezea wachange,

Sasa Leo huyo jamaa yangu baada ya kusikia makontena ya makonda ya msaada yamezuiliwa ili yauzwe kanipigia moja kwa moja kwamba ulisema kweli, nami sivikusanyi

Mnakatisha wanaojitolea tamaa,
Ni bora ukatumia hela yako kuinua familia yako kuliko kuchangia Majanga ambayo serikali haithamini mchango wako,

Britanica
Tupe evidence inayo justify kwamba ni kweli hivyo vifaa vimechangwa na Diasporas na twende mbali Zaidi unipe ushahidi kama ni kweli ndani ya makontena hayo ni furniture tuu peke yake ziko huko.TRA na Dr Philip Mpango sio wtu wa mzaha mzaha wewe.Ukiyafungulia yale makontena kilichopo ndani yake utashangaa mkuu.Acha serikali iuze tupate kodi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kurekebisha maslahi mbalimbli ya watumishi wetu waliosahaulika kama sio kutupwa kabisa
 
Dua za wanyonge zinaanza fanya kazi.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Mkuu huyu mkuu wetu wa mkoa si tu hana hekima, bali anataka kufungua uchochoro wa ukwepaji kodi.
Wakuu wa mikoa wote wakiagiza "vifaa kwa ajili ya mikoa yao", unaweza kupima ukwepaji kodi utakaofuata.

Naenda mbali zaidi, Makonda katumiwa tu, hizo samani kwenye makontena nahisi zina wenyewe.
Yaani tunasema Tanzania ya viwanda yeye anaagiza nje! Ndo maana mafundi seremala hawana kazi! Alipe kodi.
 
apo ndo napokumbukaga kua ya kaisari mpe kaisari....!!!!
 
Laana kwa watu watakaonunua makontena? Je laana za watu aliowaumiza yeye je? Mie naona laana za watu aliowaumiza ndizo zimeanza kufanya kazi na bado!
 
Sasa kumekuchaaaaaaaaaa, sasa kumekuchaaaaa, jogoo limekwisha wika Chimwagaaaaa..... (kwa sauti ya hayati John Komba)...
 
20180828_092856.png
 
Kuna maelekezo public na maelekezo ya chini kwa chini,haya ya chini kwa chini ndio huwa na nguvu,kama haya makontena yatauzwa basi tuombe uzima,tutakuja kuona Kati ya mpango na makonda ni Nani mwenye nguvu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huyu mkuu wetu wa mkoa si tu hana hekima, bali anataka kufungua uchochoro wa ukwepaji kodi.
Wakuu wa mikoa wote wakiagiza "vifaa kwa ajili ya mikoa yao", unaweza kupima ukwepaji kodi utakaofuata.

Naenda mbali zaidi, Makonda katumiwa tu, hizo samani kwenye makontena nahisi zina wenyewe.
Kuuumbeee!
Sasa naanza kukonekiti doti!
Huyu kaleta samani!
Huyu kajenga shule!
Huyu kasema samani zipigwe mnada!
Huyu kalaani!
Huyu kanunua madiwani!
Mwenyenguvu mpisheni jamani!
 
#MwananchiNukuu Wengine hugawa watu katika mafungu. Mtu fulani akifanya kosa hata liwe kubwa, hasemwi lakini mwingine akifanya kosa japo dogo hukuzwa likawa kama Mlima Kilimanjaro" Hayati Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere #MwananchiLeo

Sasa huyu bashite kafanya bonge la kosa lakini baba yake anamlinda tu hapo ndo utajua jiwe alivyombaguzi.
hujui anampa nini mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mk
Hii series hii inaonyesha magu kashamchoka Bashite na ndio maana wateuliwa wa magu hawatishiki kwa sasa, na napata uhakika sasa kuwa ni kweli Bashite akili zake hazipo sawasawa maana mara ya kwanza aliyakana hayo makontena kuwa sio yake akaja tena akisema kuwa ni yake na anaomba msamaha wa kodi na sasa anawalaani wanaoyapiga mnada wakati ni yeye mwenyewe mwazo aliyakana kuwa sio yake

Alafu ukimkuta kule insta anavyopost mambo ya kilokole huwezi mshtukia kuwa ni shetani mkubwa huyu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu usicheze na mwana Wa mungu, muda si mrefu mungu baba yake bashite ata mshughulikia huyo mpango,
 
Back
Top Bottom