Dar: Lori lililopakia saruji limeyagonga magari mawili madogo katika eneo la Tegeta Wazo

Dar: Lori lililopakia saruji limeyagonga magari mawili madogo katika eneo la Tegeta Wazo

Lori lililokuwa limebeba saruji limeyagonga magari mawili madogo katika eneo la Tegeta wazo, Dar es Salaam ambapo zoezi la uokoaji linaendelea.

---
Lori lililokuwa limebeba Saruji limeyagonga Magari mawili madogo katika eneo la Tegeta wazo, Dar es Salaam

Zoezi la Uokoaji linaendelea huku Taarifa za awali zikisema Watu 3 wamepoteza Maisha

View attachment 2413063
Nchi imekuwa ya majanga kila kukicha.
 
Kuna taarifa za Ajali mbaya ya Lori lililobeba Cement kuparamia gari ndogo kadhaa na Kuna taarifa ya vifo. Poleni kwa wahanga
IMG-20221111-WA0019.jpg
 
Haya malori ya kiwanda Cha Wazo ni hatari sana Kwa wakazi wa Madale na Wazo,mara nyingi yanakata break na kuserereka,kipande Cha barabara Toka wazo to kibaoni ni chembamba sana na kibaya zaidi ndo inatumika na mabasi yanayoenda kaskazini .hao watu wamekufa asubuhi wakiwa wanaelekea kibaruani,so sad😭
 
Tegeta-Wazo Road ni nyembamba sana, serikali ilipe fidia itanue hiyo barabara ingawa nasikia walioijenga ni wazo(kiwanda) wenyewe.
Moja wapo ya barabara hatarishi ndani ya JMT ni pamoja na hicho kipande cha kutoka Tegeta Kibaoni hadi pale kiwandani (Twiga Cement). Jumla ya ajali zilizotokea katika hicho kipande na kusababisha vifo ni nyingi sana. Ile barabara kwa namna yoyote ile inahitaji kujengwa upya kusudi iendani na hali halisi ya mazingira ya sasa na yajayo. Kwa bahati nzuri siyo ndefu sana, kama sijakosea itakuwa na urefu husiozidi 2Km.

Kwa sasa ile barabara siyo tu inakidhi mahitaji ya pale kiwandani kama ilivyokusudiwa hapo awali, la hasha! Ile barabara kwa sasa inahudimia wadau wengi sana. Mabasi yote yaendayo kaskazini (i.e. Arusha, Kilimanjaro na Tanga) yanapita pale pale, idadi ya wakazi wanaotumia ile barabara ni wengi sana na kwa asilimia kubwa pia wana uwezo wa kati yaani wanamiliki magari, mabasi ya shule pia ni mengi sana. Sasa jaribu kutafakari kwa kina....serikali itawaambia nini wananchi pale itakapotokea ajali inayohusisha mabasi ya watoto wa shule au hata mabasi ya abiria?

Wananchi inatupasa tupaze sauti la sivyo tutazidi kuangamia kwa kukosa maarifa!
 
Hizi accidents za Wazo , cement, Tegeta ni kila "siku", nobody cares! Makalla, sema neno basi au ndiyo hivyo kidumu chama kile kile cha mapinduzi
 
Mteremko wa wazo kuja huku kibaoni ni shida sana. Ni eneo la ajali nyingi, siku moja basi imetupita kitopeni bagomoyo nafika hapo Kibaoni nakuta imeliwa na lori la cement

Pole kwa waathirika wa ajali hii
R.I.P Waliotangulia
 
Binadamu muda wowote utakufa, jitahidi kula na kufurahia maisha.
Ni kweli lakini kwa nchi kama Tanzania hasa jiji la Dar, uzembe unasababisha vifo vya ajali za magari vingi sana. Haya yote yanaweza kabisa kupunguzwa kabisa. Hayo malori mengi ni mabovu lakini bado utashangaa yako barabarani na yanakwenda mwendo wa kasi sana.
 
Lori lililokuwa limebeba saruji limeyagonga magari mawili madogo katika eneo la Tegeta wazo, Dar es Salaam ambapo zoezi la uokoaji linaendelea.

---
Lori lililokuwa limebeba Saruji limeyagonga Magari mawili madogo katika eneo la Tegeta wazo, Dar es Salaam

Zoezi la Uokoaji linaendelea huku Taarifa za awali zikisema Watu 3 wamepoteza Maisha

Hili ni tatizo la miaka mingi sana.
Hayo malori ni chakvu na hayanaga breki.
 
Ni kweli lakini kwa nchi kama Tanzania hasa jiji la Dar, uzembe unasababisha vifo vya ajali za magari vingi sana. Haya yote yanaweza kabisa kupunguzwa kabisa. Hayo malori mengi ni mabovu lakini bado utashangaa yako barabarani na yanakwenda mwendo wa kasi sana.
Nini kifanyike? Na askari hawakagui magari wao wanaangalia uwezekano wa kupata pesa na faini.

Mambo kama haya yanahitaji mipango ya muda mrefu ambayo haina siasa.
 
Nini kifanyike? Na askari hawakagui magari wao wanaangalia uwezekano wa kupata pesa na faini.

Mambo kama haya yanahitaji mipango ya muda mrefu ambayo haina siasa.
Wanasiasa wa Tanzania hasa chama tawala wamekuwa matapeli kiasi cha wananchi kudhani kuwa siasa ni utapeli. Huwezi kukwepa siasa kwenye mipango ya nchi. Viongozi wanaochaguliwa na wananchi ndiyo huweka mazingira ya wataalam kupanga mipango. Bila kuwa na viongozi wenye vision na wachapakazi huwezi kupanga mpango wowote. Unaweka na eg mkuu wa wilaya changudoa, aliyepata ukuu wa wilaya kwa sababu ya kuwa nyumba ndogo ya kiongozi halafu unategea miujiza ya ''mipango ya muda mrefu''?
 
Back
Top Bottom