Dar: Maandamano ya ACT Wazalendo kuelekea Ikulu kushinikiza waliotajwa wizi kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua

Dar: Maandamano ya ACT Wazalendo kuelekea Ikulu kushinikiza waliotajwa wizi kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua

Hakuna chama Cha upinzani nchi hii kwa sasa chenye uwezo wakukusanya hata raia mia mbili. Wote wezi tu km mama zao ccm
 
ACT Ni CCM (b) Ushawahi kuona maandamano ya CCM yakawa na mvuto?
Ukiona RPC Kanda maalum hajaongea chochote kuhusu maandamano hayo, endelea na shughuli zako.
 
RIPORT NYINGI ZA UKAGUZI , HUWA NI HOJA NA ZIKIJIBIWA ZINAFUTWA. JAMII INAWEZA KUJAWA PUMZI KUWA KIASI KILACHOTAJWA NI WIZI KUMBE WAKATI MWINGINE NI PROCEDURE TU AU KUNA KITU HAKUPATA UFAFANUZI WAKATI WA UKAGUZI. LIKIFIKA KWA WABUNGE KWA SABABU WAO WANATAFUTA MILEAGE ZA KISIASA ILI WANAPORUDI KWENYE KAMPENI WAONEKANE WALIKUWA WANACHAPA KAZI WANAANZA KUCHOCHEA KUNI. WANANCHI WAELIMISHWE KUHUSU UKAGUZI WA C.AG NA REPORT ZAO LA SIVYO WANAHARAKATI UCHWARA WALIOFULIA WATAIGOMBANISHA SERIKALI NA WANANCHI WASIOELEWA CHOCHOTE

Kwa maelezo yako Hakuna wizi wowote?. Tuache kutetea ufisadi kwa kulaaumu wabunge au wapinzani. Report imeonesha upigaji mwingi serikalini halafu unakuja kutetea. Siku nyingine hiyo report muisome huko vyumbani msitutangazie wanananchi.
 
Tanzania haiwezi kuwa na Upinzani wa Kweli nje ya CCM .
Baba wa Taifa ni Mwasisi wa Taifa hili . Ni mshika maono wa Taifa hili .
Kuna baadhi ya Wapumbavu wanatumia vibaya Jina la Mwalimu Nyerere na kumtukana wakidhani kuwa watafanya Mageuzi kwenye nchi hii. Nonsense!
Mfano Mwalimu alitabiri kuwa Chadema kitakua Chama kitakachoisumbua CCM wakati huo chama kilichokua na nguvu kilikua ni NCCR Mageuzi. Mwalimu akawaambia kuwa mpinzani atakayeiangusha CCM atatokea ndani ya CCM.
Lakini Cha ajabu Kuna watu Bado wanataka Katiba mpya huku wakimponda Mwalimu Nyerere na kutaka Katiba yenye Serikali Tatu na majimbo . Ni upuuzi tuu. Hakuna mtu atakayeitaoa Tanzania kwenye misingi ya Mbeba maono wake aliyeapewa na Mungu Kwa ajili ya Watanzania na Afrika nzima ingekua ni zama za vitabu vya dini Nyerere angeitwa Nabii wa Tanzania na Afrika.

ACT ni Chama Cha Kijamaa . Sawa ndiyo misingi ya Taifa letu lakini kimejaa chuki Kwa baadhi ya makabila , kina harufu ya udini, Kuna siasa za kinafiki, kina siasa za kupenda ukubwa na viongozi wake kujilimbikizia Mali Kwa mgongo wa siasa. ACT kinapigania mabadiliko ya mfumo wa kisiasa ,kiuchumi , maendeleo ya watu na mabadiliko ya Katiba kama ilivyo Kwa vyama vingine vyote vya siasa na hata baadhi ya wanaCCM. Sasa Cha ajabu ACT kimekua kikijitenga sana na vyama vya Upinzani vyenye nguvu kama Chadema.

Ni wazi kabisa kuwa Chadema ni Chama chenye nguvu ukilinganisha na vyama vingine vya Upinzani. Sasa Zito kabwa alipaswa kutumia Muda Mwingi kutafuta maridhiano na Chadema na CUF kuliko kujitafutia umaarufu wa ACT peke yake jambo ambalo kamwe halitawezekana labda wabaki TU kuwa na wawakilishi kule Zanzibar ambao bila shaka yoyote 2025 watabaki wachache sana kwani Hussein ni Rais Sahihi sana Kwa Wazanzibar na hata Tanzania. Labda Mwinyi aje Bara.

Wito wangu Kwa Zito na wapinzani Kwa ujumla . Ni wakati Sasa wa kuwa na maridhiano kabla ya kuwa na maridhiano na CCM ambayo ni Chama Dola. CCM haioni shida kutoa hata pesa zote zilizoko hazina na kuwahonga akina Mbowe na wengineo wote endapo itagundua kuwa kufanya hivyo kutawafanya wabaki madarakani. Ikumbukwe kuwa CCM ni Jina la Chama ambacho kina watu waliojitajirusha Sana kupitia madaraka na wanaendelea kujimilikisha kila kilicho kizuri kwao na familia zao na marafiki zao na wale watakaowatumia kulinda madaraka na Mali zao.

Kama wapinzani wanaamini kuwa wana watu nyuma yao basi waungane Kwa dhamira Moja ya kuisambaratisha kwanza CCM. Bila Jina CCM kuondoka kwenye masikio na mioyo ya Watanzania mabwana na watwana maskini kamwe hakuna mabadiliko chanya.
Yaani bila kule Vijiji kupoteza kabisa bendera za kijani na vikofia na tishsti za kijani, aloo sahauni kabisa wezi wa Mali za umma kuondoka kwenye ofisi za umma.

Kuna Connection kubwa sana kati ya wizi wa Mali za umma,rushwa kubwa, matumizi mabaya ya Mali za umma na Kukiweka CCM madarakani. Kawaulizeni Walimu na CWT yao na Benki ya Walimu. Yaani Wakishachaguliwa kuwa viongozi wa CWT wanageuka kuwa makada kindakindaki wa CCM ili waibe na kuharibu kila mpango wa kuwakomboa walimu baada ya uozo mkubwa wanapata uteuzi wa kuwa Kwa heshima kubwa huku wakiwa wameacha kilio kwa walimu na ubadhirifu mkubwa. Chama kinabaki kuwa Chama Cha kutetea wabakaji na walimu wanaotuhumiwa kulawiti wanafunzi na kuwatia mimba . Kumbafu kabisa !!
Hali kadhalika ndani ya wanausalama wetu ni hivyo hivyo. Wanapewa madaraka kama shukrani ya kuwaweka wezi madarakani na kulinda uhalifu wao .Matokeo yake Wizara ya Mambo ya Ndani ni kati ya wizara zilizomsumbua sana JPM na Mwalimu Nyerere kutokana na kuwa na ubadhirifu mkubwa na kutumia Muda Mwingi kuharibiana kazi na kufitiniana ili tu wapate nafasi ya kujipendekeza kwenye Chama na kupata uteuzi ili kuendelea kulindana na kulinda wezi . Mzunguko unaendelea na CCM inaendekea kutawala kupitia udhaifu na tamaa walio nao wanaotakiwa kuwakosoa na wakuu wa Idara kwa manufaa yao na kakundi ka watu wachache.

Asante Sana kwa analysis nzuri.
 
Umeongea ukweli Mchungu

CHADEMA msingi yake ni confrontation politics. Sasa tunapelekwa kwenye mediation politics. Huu ndio muda wa kurudi kwenye asili yetu tupambane mpaka wanannchi waelewe kuwa tunawapigania. Tuanze na Dodoma tufanye maandamano yasiyo na kikomo.
 
Wanajisumbua kwa raisi huyu 🤣🤣🤣hataki stress anaiendesha nchi kizungu,ambapo machinery za uwajibikaj ziko open na zinafanya kazi🤔tuwe wapole apparatus zetu ziko vizuri kufanyia kazi ripoti ya cag 🤣🤣🤔
 
Maandamano 😁

images - 2023-04-18T103527.049.jpeg
 
Maandamano makubwa yameanza eneo la Fire Kariakoo yakiwa yameandaliwa na ACT-Wazalendo kushinikiza wezi wote walionaswa na Ripoti ya CAG waondolke maofisini kwenda magerezani.

Maandamano yanaongozwa na viongozi waandamizi wa chama hicho Cha upinzani na yataishia lango Kuu la Ikulu ya Magogoni ili yapokelewe na Rais Samia Suluhu Hassan.

Binafsi Niko mbele na bango langu. Hali ya hewa si rafiki sana hata kuandika ni taabu lakini umma unazidi kujitokeza kuwataja wezi wakamatwe. Karibuni.
ACT ni CUF iliyochangamka kwa hiyo hamna jipya hapo labda rangi ya jezi zao tu
 
Hakuna chama Cha upinzani nchi hii kwa sasa chenye uwezo wakukusanya hata raia mia mbili. Wote wezi tu km mama zao ccm
Wamekuibia nini?. Report ya CAG imeipatia CHADEMA hati Safi. Wewe unadai ni wezi. Tatizo tunaitetea CCM kwa kujificha kwenye mgongo wa upinzani, wakati upinzani hawapo bungeni wala halmashauri. Sasa wanaomuibia serikalini, bungeni na halmashauri unawaona wa maana. Tuna safari ndefu.
 
Back
Top Bottom