Dar: Maandamano ya ACT Wazalendo kuelekea Ikulu kushinikiza waliotajwa wizi kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua

Dar: Maandamano ya ACT Wazalendo kuelekea Ikulu kushinikiza waliotajwa wizi kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua

CCM nao lini wanaandamana ili kumshinikiza Mwenyekiti wao amfukuze CAG kwa kuibua "Ulaji" wao?
 
Kupitia thread hii ndipo utajifunza udhaifu wa wanasiasa wa upinzani Tanzania.
ACT wataanza kushambuliwa na wafuasi na shabiki wa vyama vingine vya upinzani kuhusu haya maandamano kuliko watakavyo shambuliwa na wafuasi wa chama tawala (CCM).

Hiyo yote ni kuwakatisha tamaa wasifanikiwe kupata umaarufu kuliko wao. Kwao bora CCM iendelee kukaa madarakani na kuvurunda vitu kuliko wenzao wawe juu yao kisiasa.

Kwa mshangao kesi kama hii hadi watu maarufu na wajuaji wakubwa wa JF utawakuta wanashangilia kukwamishana wapinzani.

Ufuasi wa vyama kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda husababisha tatizo hili.
Wapinzani wa Tz hawana ushirikiano baina yao.

econonist zitto junior JokaKuu Bams
 
CHADEMA tunalemazwa na Mbowe. Niwe mkweli. Ilitakiwa maandamano yaitishwe na CHADEMA baada ya siku tatu kupita. Ila wapo kimya.
Wewe na Tindo ni miongoni mwa wahafidhina msioridhishwa na uongozi wa Mbowe hapo Cdm, ila kumbukeni mchango wa Mbowe kwa Cdm unahusika pakubwa kwenye kukifanya hichi chama kuwa chama kikuu cha upinzani.
Bams zitto junior
 
ACT kinapambana sana kuwa chama kikuu cha upinzani. Wakiendelea hivi chini ya miaka mitatu ijayo watakuwa wameshaipiku CHADEMA hasa hii ya sasa.

Maandamano yana nia nzuri sana sema mwamko wa Watanzania ndiyo zero....

View attachment 2591675
ACT na CUF ya Lipumba mko kwenye kapu moja la takataka za ccm.
Mnabebwa kuikomoa chadema lkn hata nyie wenyewe mnaujua mziki chadema ikitangaza maandamano.
 
Kwa jinsi watanzania tulivyo, hapo uko kitandani umejifunika na duvet, unaandamana Kwa simu🤣🤣
Watanzania labda tutaandamana siku mafuriko yakiingia kwenye nyumba zetu, manake tutakuwa hatuna Kwa kujificha.
Hivi duveti ni nini?!..
 
Kwa mchoro huu naona wamesahau kuweka point namba 10 itakua ni lock-up..[emoji1787]
Mama ni mpole hawezi kuwaweka lock-up bana. Sana sana atawapokea ikulu na kuwapongeza kwa kutimiza takwa lao la kikatiba. Na wakimzingua wataishia tu kuitwa stupid basi [emoji16][emoji16]
 
Wewe na Tindo ni miongoni mwa wahafidhina msioridhishwa na uongozi wa Mbowe hapo Cdm, ila kumbukeni mchango wa Mbowe kwa Cdm unahusika pakubwa kwenye kukifanya hichi chama kuwa chama kikuu cha upinzani.
Bams zitto junior

Hatubezi mchango wake, ila wakati ukuta. Angekufa na chama kingekufa? Hakuna succession plan huko CDM?
 
Maandamano makubwa yameanza eneo la Fire Kariakoo yakiwa yameandaliwa na ACT-Wazalendo kushinikiza wezi wote walionaswa na Ripoti ya CAG waondolke maofisini kwenda magerezani.

Maandamano yanaongozwa na viongozi waandamizi wa chama hicho Cha upinzani na yataishia lango Kuu la Ikulu ya Magogoni ili yapokelewe na Rais Samia Suluhu Hassan.

Binafsi Niko mbele na bango langu. Hali ya hewa si rafiki sana hata kuandika ni taabu lakini umma unazidi kujitokeza kuwataja wezi wakamatwe. Karibuni.
Kimenuka !
 
Back
Top Bottom