Desalination ni process aghali sana duniani.
Mkuu mimi nimeitumia hizo RO tukiita fresh water maker,au desalination plants,kwa zaidi ya miaka 15 huko offshore bahari ya Pacific.Tukitengeneza kati ya tani 150 hadi 200 kwa siku.
Kwanza hiyo initial cost ni aghali mno.
Operating cost na maintenance cost ni kubwa mno,kubadirisha filters weekly.
Hayo maji ni pure water hayana ingredients, hivyo kuyatumia yalivyo yana upungufu wa madini unless huongeze hizo ingredients.
Inatumia umeme mwingi mno kwa sababu ya pumps zake kusukuma maji chumvi kupitisha fresh water kwenye vipenyo vidogo mno vya membrane ni big issue.
Kitu kilicho ghali ni hizo membranes,zinataka usimamizi na matumizi sahii sana.Bei za membrane spare part ni zaidi ya nusu bei ya mtambo mpya.
Kibaya ni coastal waters si salama kwa kupata maji safi sababu ya pollution tokea viwandani na vinyesi vya binadamu , ina maana itabidi kusukuma maji kuyahifadhi kwanza kwenye setting tanks inaongeza initial cost na maintenance cost.
Lakini kama tukichimba visima hivi vyetu tukapata maji yenye chumvi kidogo inaweza kutumia RO kuzalisha maji safi kwa gharama pungufu zaidi kuliko maji ya bahari.