Dar: Maji ya Bahari yafanyiwe Desalination tuyanywe

Dar: Maji ya Bahari yafanyiwe Desalination tuyanywe

Asante kwa mchango wako. Mwisho wa siku Wananchi wa kawaida ndo wanataabika. Unashauri nini kifanyike ili kujiondoa tulipo kwama?
Nimesema kwenye maoni yangu hapo juu...

Kwamba;

1. Short term solution ni hiyo uliyopendekeza wewe, utafutwe uwezekano kuyabadili maji ya bahari yatumike kwa matumizi ya binadamu na viwandani kwa kutumia teknolojia ya Salinization bila kujali gharama..

2. Long term solution ni watanzania tukubali na tuhamasike kusukuma mabadiliko ya mfumo wa kiutawala na kisiasa wa nchi yetu kwa kuandika Katiba mpya ya wananchi ili kuleta uwajibikaji serious wa kila kiongozi anayepewa dhamana ya ku-serve wananchi...
 
Kwa jinsi mambo yalivyo hilo wazo likitekelezwa hatuchelewi kuambiwa kina cha bahari kimeshuka halafu meli zimeshindwa kuja na kupunguza mapato ya bandari...janja janja iko nyingi sana🐒
 
Kama kuna mtu anafahamu inavyotengenezwa gongo basi huu mradi aliousema mkuu hapo ni rahisi wachukulie yale yale matilio ya mtambo wa gongo coz pale unavunwa mvuke then unabadilishwa kuwa kimiminika na hapo utachukuliwa mvuke wa maji ya bahari utabadilishwa kuwa kimiminika kwanza watapata faida mbili
1.watapata maji safi na salama yalio chemshwa hayahitaji hada dawa ya kuuwa vijidudu
2.watapata chumvi safi ya kupikia
nawasilisha
 
Nyie si ikifika msimu wa uchaguzi mnapewa vijora na kanzu mnaanza kuimba "wacha waandamane, wataisoma namba"
Saivi kwenye namba tunaisoma wote.
Mi nnaona wacha maji yakosekane kwani Kuna shida gani,?Kuna mijitu mikubwa humu miaka inazidi kusonga na Bado linainjoy na linaionea huruma rangi ya kijani utadhani lilizalliwa garden kwenye majani
Haya ndio yametuletea huu umasikini
Lisa limepewa buiu kumi ligawane na mwenzake kesho yanaenda kuwarudisha madarakani
Ujinga
 
Nimesema kwenye maoni yangu hapo juu...

Kwamba;

1. Short term solution ni hiyo uliyopendekeza wewe, utafutwe uwezekano kuyabadili maji ya bahari yatumike kwa matumizi ya binadamu na viwandani kwa kutumia teknolojia ya Salinization bila kujali gharama..

2. Long term solution ni watanzania tukubali na tuhamasike kusukuma mabadiliko ya mfumo wa kiutawala na kisiasa wa nchi yetu kwa kuandika Katiba mpya ya wananchi ili kuleta uwajibikaji serious wa kila kiongozi anayepewa dhamana ya ku-serve wananchi...
Upo sahihi
 
Kuota ndoto sio jambo baya, ila uhalisia wa mambo ndio swala muhimu. Sidhani kama Sisi watu wa kuota ndoto za Desalination au hata Recycling wakati tuna mvua, mito inayotirisha maji mwaka mzima na maziwa ya kutosha tu. Kwanini tusifikirie kujenga mabwawa kila mahali ikiwa ni pamoja na Wami, ambapo jiografia inaruhusu. Maji mengi ya mvua zinazonyesha nchini yanaishia baharini baada ya kusababisha mafuriko. Mvua zikiisha tunakuwa na tatizo la ukame na shida ya maji.
Tumelala
 
Sala Wakuu,

Ni aibu kwa Dar, Tanga na Zanzibar kuwa na Mgao wa Maji Wakati kuna Bahari.

Nashauri Serikali itengeneze Maji ya Bahari ili kuondoa tatizo la maji Dar.

Maji ya Ruvu hayatoshi. Pwani peke yake kwa Takwimu za Serikali ina Viwanda 1036 na vyote vinatumia hayo Maji. Achinjilia mbali Hoteli za Dar.

Ni aibu kwa Nchi kiwanda kuzimwa kwa kukosa maji, au hoteli kukosa Maji.

Tanzania ni Tajiri. Itengeneze mtambo wa seawater reverse osmosis systems SWRO. Maji tutauza hadi Nchi jirani.

seawater reverse osmosis systems SWRO ni teknolojia ya kutengeneza maji ya bahari yaweze kutumika kunyweka.

Viwanda wapewe maji ya Bahari theni Dawasa ibaki na wananchi.

Uzuri, Mtambo hautumii umeme mwingi, hivyo tunaweza kutengeneza umeme wa upepeo baharini ukaendesha mtambo usiku na mchana.

Dar ndo Nchi, Dar kutegemea maji ya Chanzo kimoja ni shida. Anakuja adui anaangusha pale Missile moja, dar nzima inakosa maji.

Nchi kibao hazina vyanzo vya maji na maji hayakatiki kwa kutegemea Maji ya bahari tu.

Sehemu kama Kuwait, Saudi Arabia, Marekani, Carlsbad, San Diego, Singapore, Canary Islands, Caribbean, China, Japan wanategemea maji ya bahari na hautasikia uhaba wa maji.

Mungu atupe nini. Achana na Bandari ya Bagamoyo. Wape maji Dar. Au tuuze ndege moja tununue mtambo. Kupanga ni kuchagua
View attachment 2399355
CC: Wizara ya maji
kuna kampuni XX ya kuuza maji leo nmeenda dukani kununua maji nmepata kama lita na nusu kwa jelo ila hyo ladha ya maji unajua kabisa haya ni maji ya bahari
 
kuna kampuni XX ya kuuza maji leo nmeenda dukani kununua maji nmepata kama lita na nusu kwa jelo ila hyo ladha ya maji unajua kabisa haya ni maji ya bahari
Hyo itakuwa AZAM maana bakhresa yeye anasema anauza chupa na sio maji maana ni haram kuuza maji ndio maana anauzia watu maji ya chumvi
 
Hii siyo ishu ya DAWASCO bali ni swala la nchi kwa ujumla likihusisha SERA na MIPANGO...

DAWASCO ni kibarua tu wa serikali. Ni watendaji na watekelezaji wa SERA na MIPANGO ambayo tayari serikali inayo...

Chombo kinachoweza kusukuma agenda hii na serikali kufanya ni BUNGE. Hiki ndicho chombo na sauti ya wananchi...

Bunge likisema, wananchi wamesema na serikali inatii. Bahati mbaya tu ni kuwa, Tanzania kwa sasa HATUNA BUNGE. Nchi hii ni yatima. Tuendelee kuomba Mungu aingilie kati na kutunusuru na anguko kuu lijalo..

Ndo kusema kubwa, mambo ya nchi hii kwa sasa hayawezi kwenda unless kufanyike mabadiliko makubwa ya mfumo wa kisiasa na kiutawala wa nchi yetu kupitia mabadiliko ya kikatiba...

Kuwaambia watu hawahawa walio kwenye mfumo huu mbovu wa kiutawala na kisiasa ulioshindwa kutatua matatizo ya nchi hii kwa muda wote huu wa miaka 60 tangu uhuru ni kumpigia mbuzi gitaa ili acheze...

Nchi hii kwa sasa kila kitu ni shida. Umeme ni shida. Maji ni shida. Elimu ni shida. Siasa zetu ni shida tu. Kila kitu ni shida. Hakuna sekta ya huduma ya kijamii ambayo utasema ingalau ni afadhali...

Hii ni ishara ya wazi kuwa, watawala wa sasa chini ya CCM wameshafikia ukomo wa kufikiri kwa ajili ya nchi na wananchi....

Badala yake kwa kuwa wao hawakatikiwi na umeme, maji kwao yanatiririka usiku na mchana, hawawezi kujua shida na adha wanazopata wananchi sisi...

figganigga
Bunge la wakina Babu tale [emoji1]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom