Dar: Maji ya Bahari yafanyiwe Desalination tuyanywe

Kuna mgeni alikuwepo leo radio one sijui ni Boss kutoka Wizara ya maji,naye anasema kutumia maji ya bahari ni ghali lakini hasemi ni ghali ukilinganisha na nini? Na ni ghali kiasi gani? Tunaambiwa tu ghali.

Hii nchi ina watu wa hovyo sana, unaweza kukuta huyo boss kutoka wizara ya maji wala hajui ni bei gani huo mtambo, bali na yeye kasikia tu watu mitaani wanasema huo mtambo ni bei ghali!
 
Kuyafanyia Desertation ndiyo kufanyaje?
 
Kweli ndugu yangu, 'Desalination mara nyingi wanaweza nchi zilizo financially stable, na sio nchi kama sie hohehahe............
Kama waganda wanajenga bomba la mafuta kwa $3.5b kutoka Uganda hadi Tanga, huo mtambo wa maji hapa baharini ndio utakuwa ghali zaidi ya huo?
 
Kuota ndoto sio jambo baya, ila uhalisia wa mambo ndio swala muhimu. Sidhani kama Sisi watu wa kuota ndoto za Desalination au hata Recycling wakati tuna mvua, mito inayotirisha maji mwaka mzima na maziwa ya kutosha tu. Kwanini tusifikirie kujenga mabwawa kila mahali ikiwa ni pamoja na Wami, ambapo jiografia inaruhusu. Maji mengi ya mvua zinazonyesha nchini yanaishia baharini baada ya kusababisha mafuriko. Mvua zikiisha tunakuwa na tatizo la ukame na shida ya maji.
 
Kujenga desalination plant serikali inaweza kujipinda kwa msaada wa wahisani ikajenga.

Shida inakuja kwenye gharama za kuiendesha na kuitunza hiyo desalination plant

Na ili huo mradi udumu lazima ujiendeshe je, wananchi wataweza kumudu gharama za kununua maji hayo ili mradi ujiendeshe au ndio serikali itajikuta inaingia hasara ya kutoa ruzuku ili kuuhudumia??
 
Opportunity Cost...

Desalination ni expensive labda baadae technology inavyozidi kubadilika..., tuwaachie waarabu wenye nishati ya kumwaga wafanye desalination Bongo tuna cheaper alternatives..., Pili Wastes factor mabaki ya desalination ni more salt concentrated sasa kuyarudisha baharini kuna environmental unpredictability ya madhara ya hii kitu
 
Mwaka 2016 tulipataga majaa walitaka kuja funga hii system pale karibu na Sea Clif Hotel au pale baada ya Police mess! Na Bei kwa Gallon ilikuwa so Cheap kuliko kutoa maji Ruvu kuja Dar....Siasa zetu zikawa nyingii tukashindwa kuendelea nao.Mwaka Jana nilipata hawa wanazalisha maji ya kunywa kutokana na Hewa. Nao wapo Tayari kuja wekeza Hapa Tanzania So kama kuna member wa JF anaweza push ani PM tupige kazi
 
Hapana kwa sasa Zipo system cheap za kuzalisha maji safi toka bahari kwa garama nafuu kama vile unayavuna mtoni- tuliwai fanya tafiti hii hapa Tanzania na wa Israel. Garama la Galoni moja la Dawasa cost yake na garama ya Galoni inayozalishwa na Desalination plant , Desalination ipo Cheap
 
Rufiji siyo mbali. Kwa nini wasichukue maji ya mto Rufiji walete kwa watu wa Dar?
 
Unadhani ingekuwa hivyo dunia ingehangaika na kwamba fresh water ni only 2% wakati tumezungwa na maji / bahari kuliko hata ardhi ?

ofcourse its getting cheaper by the day and what about disposing the remain concentrated water (Umeiweka pia hii under consideration)?

Sijafanya utafiti zaidi but if this was the case common sense inaniambia issue za maji zisingekuwa tabu duniani
 
Mkuu umejibu vyema sana.
 
Mungu wa mbinguni tumekukosea nini sisi watanzania? Mpaka leo hatujapata viongozi wanao weza kuondoa tatizo la maji?
Hadi kwanza wananchi tutakapo kuwa na akili,yaani leo hii anaibuka kiongozi anasema eti tusilaumiane kuwa ni mipango ya Mungu!!kweli yaani kila mwaka matatizo ni yale yale,yanapotokea mbinu zinazotumika ni za kidharura utadhania ,ni janga wakati ni kitu kinachofahamika.
 
Kujenga mabwawa ya kukinga maji ya mvua Ili kutumia wakati wa kiangazi ni gharama rahisi kuliko kusafisha maji ya bahari.
Kila teknolojia hutumika mahali fulani kulingana na kinachopatikana hapo.
Kwa nini tuhangaike kusafisha maji ya bahari wakati tuna vipindi vya mvua vya kutosha?
Elimu zetu zinatakiwa zitumike kulingana na hali na mazingira halisi badala ya kukariri.
 
Tatizo la Watanzania wengi kama wewe mnapenda dandia vitu na kujifanya mnajua kila kitu! Mnabishana bila kutoa majibu ya kisayansi unapayuka payuka tu! Israel wana zaidi ya miaka 30 wanazalisha maji ya kunywa kutokana na maji ya bahari. Na wana all it takes kudeal na waste baada ya kuzalisha haya maji- kwa kukusaidia hapa Tanzania mji karibia yote yanayouzwa kwenye Chupa yanapitia same system isipokuwa tu settings za maji ya visima na ya bahari zina tofautiana ila ata wazalishaji wa maji kama Uhai Wanaweza wakabadilisha settings za mitambo yao ya RO wakaweza kuzalisha pure drinking water from the sea water
Tafuta hii plant kubwa ya Israel inayozalisha mamilioni ya lita za maji safi toka kwenye maji bahari

Sorek Desalination Plant​

 

Attachments

  • 006E28F7-DCED-4232-89E7-05DB8A7DA270.jpeg
    58.7 KB · Views: 4
Tatizo la Watanzania wengi kama wewe mnapenda dandia vitu na kujifanya mnajua kila kitu! Mnabishana bila kutoa majibu ya kisayansi unapayuka payuka tu! Israel wana zaidi ya miaka 30
Kwahio Israel wakifanya ndio the cheapest model ya kuzalisha maji kuliko nyingine ambazo zipo ? Kwao wanaweza kufanya na ni cheaper kutokana na their opportunity cost je sisi hatuna mbadala wa cheaper means..., haya mambo ya fulani kafanya na mimi nifanye nadhani ni myopic thinking....
wanazalisha maji ya kunywa kutokana na maji ya bahari. Na wana all it takes kudeal na waste
Its still debatable scientifically effect ya wide range desalination wakifanya mataifa matatu manne sawa ila kila mtu akifanya let alone cost ya nishati Je pockets za concentrated salt water zinaweza / zitaleta madhara gani ya kimazingira wewe unajua ?
baada ya kuzalisha haya maji- kwa kukusaidia hapa Tanzania mji karibia yote yanayouzwa kwenye Chupa yanapitia same system
Na hayo maji ya chupa ni bei gani na ya haya tunayouziwa kutumia nyumbani na sio kunywa tu mpaka kumwaga chooni na kumwagilizia bustani na kuoshea magari ni bei gani ? Ushafanya hizo hesabu ?

Na je ni cheaper kuliko labda uvunaji wa mvua kujenga mabwawa au pumping ya maji kwa nchi yenye vyanzo vya kutosha vya fresh water na mvua za above average ?

Haya yote umeweka katika consideration au tu sababu Israel anafanya basi na sisi tufanye ?
And howmuch will a bottle cost? Is it cheaper now with what they are doing or will it be cheaper then ? Na kwanini hawafanyi au hizi information ulizonazo wewe wenyewe hawana ?
 
Hii siyo ishu ya DAWASCO bali ni swala la nchi kwa ujumla likihusisha SERA na MIPANGO...

DAWASCO ni kibarua tu wa serikali. Ni watendaji na watekelezaji wa SERA na MIPANGO ambayo tayari serikali inayo...

Chombo kinachoweza kusukuma agenda hii na serikali kufanya ni BUNGE. Hiki ndicho chombo na sauti ya wananchi...

Bunge likisema, wananchi wamesema na serikali inatii. Bahati mbaya tu ni kuwa, Tanzania kwa sasa HATUNA BUNGE. Nchi hii ni yatima. Tuendelee kuomba Mungu aingilie kati na kutunusuru na anguko kuu lijalo..

Ndo kusema kubwa, mambo ya nchi hii kwa sasa hayawezi kwenda unless kufanyike mabadiliko makubwa ya mfumo wa kisiasa na kiutawala wa nchi yetu kupitia mabadiliko ya kikatiba...

Kuwaambia watu hawahawa walio kwenye mfumo huu mbovu wa kiutawala na kisiasa ulioshindwa kutatua matatizo ya nchi hii kwa muda wote huu wa miaka 60 tangu uhuru ni kumpigia mbuzi gitaa ili acheze...

Nchi hii kwa sasa kila kitu ni shida. Umeme ni shida. Maji ni shida. Elimu ni shida. Siasa zetu ni shida tu. Kila kitu ni shida. Hakuna sekta ya huduma ya kijamii ambayo utasema ingalau ni afadhali...

Hii ni ishara ya wazi kuwa, watawala wa sasa chini ya CCM wameshafikia ukomo wa kufikiri kwa ajili ya nchi na wananchi....

Badala yake kwa kuwa wao hawakatikiwi na umeme, maji kwao yanatiririka usiku na mchana, hawawezi kujua shida na adha wanazopata wananchi sisi...

figganigga
 
Asante kwa mchango wako. Mwisho wa siku Wananchi wa kawaida ndo wanataabika. Unashauri nini kifanyike ili kujiondoa tulipo kwama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…