Huyo Roho wa Kweli anayezungumziwa ha Yesu hapa tunajua ni Roho Mtakatifu na sio SWW. Na alikwisha kuja siku ile mitume waliposhukiwa na Roho Mtakatifu ndio siku ya Pentekoste kama iliyoandikwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume 2:1-47.
Natulichungue hili neno lililofasiriwa Msaidizi katika Bibilia ya Kiswahili, na ambalo limeitwa "
Comforter" yaani Mliwazi katika Biblia ya Kiingereza ya zamani ya
King James, na likaitwa "
Counsellor", yaani Mshauri katika Biblia ya Kiingereza ya
Revised Standard Version, na likaitwa "
Helper" yaani Msaidizi katika Biblia za Kiingereza mpya mpya kama
New World Translation na
Good News Bible, na "
Mu'azzi", yaani Mliwazi katika Biblia ya Kiarabu ya
Darul Kitabul Muqaddas ya Cairo
Maneno aliyoyasema Yesu tunayapata kwa tafsiri tu, kwani Yesu hakusema kwa Kigiriki wala Kilatini, bali alisema kwa lugha ya kawaida ya Palastina wakati ule ilikuwa ni Kiaramiya na lugha yao ya dini ni Kiebrania.
Zote mbili hizo zina asili moja na Kiarabu.
Injili ya Yohana ndio hiyo iliyotaja hiyo bishara ya Yesu kuwa atakuja huyo aitwae Msaidizi.
Katika utangulizi wa nakla ya Biblia ya Revised Standard Version imeelezwa kuwa hata hiyo matini ya Kigiriki ilioko "imeharibiwa na makosa yaliyojumlika kwa kukosoea kosea kwa walionukulu muda wa karne kumi na nne."
Wataalamu wa Biblia wakubwa kama Rudolf Bultmann (Mprotestanti) na Father John Lawrence Mackenzie (Mkatoliki) wanakubali kuwa sehemu nyengine za Injili si kweli kihistoria, na ya kwamba maneno fulani ya Yesu kwa hakika yamebuniwa na Kanisa la kale.
Ni makosa kusema kuwa huyo
Periklitos (Msifiwa) aliyefasiriwa kwa kukosea Msaidizi, ni Roho Mtakatifu, ambaye Wakristo wanasema ni nafsi ya Mungu. Ushahidi wa makosa hayo umo humo humo katika Injili ya Yohana.
Kama huyo Msaidizi ni Roho Mtakatifu kwanini Yesu alisema "yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo (
Periklitos) hatakuja kwenu.???
Roho Mtakatifu twaambiwa ni Mungu wa milele. Je, kwani Mungu hatokuwepo maadamu Yesu yupo?
Je, yeye Yesu na Manabii wote waliomtangulia na watakatifu wengine hawakuteremkiwa na Roho Mtakatifu?
Injili ya Mathayo, nayo inatueleza kuwa Yesu alibashiri kutokea kwa Muhammad, ambaye ni katika uzao wa Ismaili, anayefananishwa na jiwe liliokataliwa na wajenzi.
Pia Yesu alibashiri kuinuka kwa Umma wa Kiislamu utakaopewa Ufalme wa Mungu, nayo yote hayo yakatimia:
Yesu akwaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?
Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.
Mathayo 21.42-44