Naam ni jambo la afya kuwa na fikra huru za kufikiria juu ya jambo, kitu, ama mtu kadri Mungu anavyokuwezesha.
Hata hivyo, kwa kuanza kumkosoa Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli, aliyekuwa rais wa nchi yetu Tanzania, tena kwa kebehi huku ukijua kabisa hawezi kuja hapa kufafanua utofauti wa contracts na framework agreement, inatoa taswira ya ama kwa makusudi unataka kubadili mjadala ama kuna ukweli kuna nguvu za 'ziada' zinakuweka kwenye utetezi wa mradi (sentensi ndefu, nivumilie).
Binafsi, sikutilii shaka lakini unatengeza mazingira ya kunikatisha tamaa mimi mwanafunzi wako kindakidanki nisiendelee na somo.πππ
Ndugu yangu inakuwa hunitendei haki ukisema kwamba namkebehi Magu...
Btw, kwani wakati yupo hai alishawahi kuja JF kujibu chochote hadi ionekane kusema hivi sasa itakuwa ni kutomtendea haki?!! Halafu hili la Magu unatakiwa kulizoea...
Mwalimu amefariki zaidi ya miaka 20 iliyopita, lakini bado anasemwa, na ataendelea kusemwa!
Karume amefariki takribani miaka 50 iliyopita lakini bado anasemwa na ataendelea kusemwa!!!
Kwahiyo unatakiwa kuzoea na hilo la Magu....
Ndugu yangu TUJITEGEMEE hebu tafakari peke yako....
Ulishawahi kuona au kusikia pande mbili zinasaini mkataba, halafu hapo hapo wanatangaza wanaendelea na majadiliano kwa sababu hawajafikia makubaliano?! Hushawahi kusikia kitu kama hicho?!
Sina shaka wewe ni mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea nchini! Je, ipo siku yoyote uliyowahi kusikia kwamba SERIKALI IMEVUNJA MKATABA wa Ujenzi wa Bandari?
Ukitafakari kwa makini, utaona wazi kwamba hapakuwa na mkataba na ndo maana majadiliano yalikuwa yanaendelea!! Sasa kama hapakuwa na mkataba, ni mkataba upi ambao Magu na Serikali yake walikuwa wanatutangazia kwamba ni wa Kinyonyaji, ni upi?!
Sasa hapo uki-doubt credibility ya Magu sio kwamba ni kumkebehi bali ndo uhalisia wenyewe!!! Na ukizingatia kauli zingine kwenye mambo mengine, hapo inatoa nguvu zaidi ya ku-doubt credibility yake!!
Lakini tatizo lingine la Magu, inawezekana ni kama lile ambalo niliwahi kusema kuhusu Kakoko, kwamba Kakoko ni Engineer kwahiyo inawezekana hana uelewa mkubwa kuhusu mambo ya kodi!!
Matokeo yake, akaenda kwenye media na kutangaza "Mchina ametaka asamehewe kodi" bila kutaja ni kodi ipi! Ilikuwa ni muhimu kutaja kwa sababu, sheria zetu zinaruhusu kusamehe baadhi ya kodi ili kuvutia wawekezaji!!
Lakini unapotoka tu mbele na kusema "Mchina anataka asamehewe kodi" ni rahisi sana wananchi kuamini kwamba kumbe zile VAT, Import Tax, Excise Duty n.k zote hizo zinaenda kwa Mchina; jambo ambalo si kweli!!