Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata ingekuwa tupu wangeileta? Meli imeletwa na mzigo, wanalipwa na wenye mzigo.Walioleta meli wamesema huduma zimeboreka
Kweli mkuu hata mimi nilishawai kuiona miaka ya nyuma ikiwa inashusha magari hapohapo bandari ya DSM.hii nchi ngumu mno kwa uongo.Mbona hii meli imewahi kuja Bandari ya hapo hapo Dar es Salaam kipindi cha nyuma ?
Nini kimebadilika mpaka iwe habari ?
Naomba ufafanuzi tafadhali !
Meli hiyo iliyotengenezwa mwaka 2009 ina urefu wa mita 199.9 na upana mita 32.2 kwenda chini
Tabia nchiMbona hii meli imewahi kuja Bandari ya hapo hapo Dar es Salaam kipindi cha nyuma ?
Nini kimebadilika mpaka iwe habari ?
Naomba ufafanuzi tafadhali !
hapanaJe Bandari yetu inaweza kupokea meli zenye urefu wa 400m kama za Hmm algeciras?
Terms za uwepo wake ndiyo kikwazo. Hakuna asiyetaka mradi wenye maendeleo ya win win! Win loose ndiyo haikubaliki.I wish watu wengi zaidi na zaidi wangefahamu faida za Bandari ya Bagamoyo lakini, dah!
Leo hii habari haizungumzii ukubwa wa meli wala idadi ya makontena, inazungumzia idadi ya magari,Mbona hii meli imewahi kuja Bandari ya hapo hapo Dar es Salaam kipindi cha nyuma ?
Nini kimebadilika mpaka iwe habari ?
Naomba ufafanuzi tafadhali !
View attachment 1887764
View attachment 1887765
Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuzivutia kampuni kubwa za usafirishaji duniani, baada ya meli kubwa ya kisasa ikiwa na shehena kubwa zaidi ya magari kuwahi kutia nanga bandarini hapo.
Meli hiyo ya TRANQUAIL ACE (IMO: 9561253) inayomilikiwa na Kampuni ya Mitsui ikitokea moja kwa moja nchini Japan, imetia nanga ikiwa na magari 3,743 ambayo ni mengi zaidi kuwahi kusafirishwa kuja nchini kwa mara moja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi amesema kuwa meli hiyo imeandika historia mpya kutokana na kubeba shehena kubwa ya magari.
Meli hiyo iliyotengenezwa mwaka 2009 ina urefu wa mita 199.9 na upana mita 32.2 kwenda chini, ambapo imetia nanga chini ya nahodha, Diardado Garate.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 10, 2021 katika Bandari ya Dar es Salaam, Hamissi amesema kuwa meli hiyo imetia nanga Agosti 9, 2021 na kuanza shughuli ya ushushaji ambao unatarajiwa kumalizika kesho jioni.
Meli kubwa kuwahi kutia nanga nchini na ailiyokuwa imebeba shehena kubwa ya magari ilitia nanga bandarini hapo mwaka 2018 ikiwa na magari 2600.
"Leo ni siku nzuri sana katika historia ya TPA kwa kuweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa na iliyobeba shehena kubwa zaidi kuja nchini. Hii haijawahi kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kubwa zaidi meli hii imetoka moja kwa moja Japan kuja nchini bila kupitia bandari nyingine.
View attachment 1887766
"Kwa hiyo ni jambo jema dunia inakafahamu kwamba, Tanzania tuna bandari bora na ya kisasa yenye uwezo wa kupokea meli zote na ikazihudumia kwa wakati,” amesema Hamissi na kuongeza: “Katika inayoendelea kushushwa, magari yatasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda nchi jirani na mengine 798 yanabaki hapa nchini.
"Mtaona ni jinsi gani sasa nchi zetu za jirani zinazotuzunguuka zimeenza kutuamini, kati ya magari yaliyoingia asilimia 65 yanakwenda kwenye nchi hizo."
Meneja Kampuni ya Inchcape Shipping Services, John Massawe amesema meli hiyo ina uwezo wa kubeba magari 5,200 na kwamba imetumia siku 20 ikiwa safari hadi kuwasili.
"Tumekuwa tukihudumia kampuni ya magari kwa miaka zaidi ya 20, na hii ni meli ya kwanza hivyo tunatarajia huu ni mwanzo wa kuleta meli nyingine kubwa zaidi," amesema Massawe.
Terms za uwepo wake ndiyo kikwazo. Hakuna asiyetaka mradi wenye maendeleo ya win win! Win loose ndiyo haikubaliki.
Naona ni sawa tuu, kumbuka Si nchi moja wala mbili, yaweza kua 5 au zaidi, kuna uwezekano kati ya hizo nchi, bado idadi yetu ipo juu...65% ya magari yanaenda nchi nyingine ! -
sisi kwetu huku shida nini gharama za kodi au uchumi wakati?
Ndio nakwambia wenye mzigo wameileta kwa sababu huduma zimeboreshwa.Wailete tupu kwani wanafanya maonyesho ya meli?Hata ingekuwa tupu wangeileta? Meli imeletwa na mzigo, wanalipwa na wenye mzigo.
Alaa kwa hiyo magari ya Zambia na Malawi sio shehena ya mizigo? Kule Mombasa hawapitishi magari? Aisee wewe ni mburula wa kiwango cha vumbi kabisaaaTunajisifu kwa kupitisha magari ya Zambia na Malawi. Shehena za mizigo mizigo inapita Mombasa.
Shida ya maccm ni moja kama kundi Lililoko madarakani halikunufaika na 10% na mradi haujaanza huwa hawaendelezi na huwa wanaona sifa zitakwenda kwa mwingine.Huwa ni wapumbavu Sana hao.Hii win loose ilikua ni fikra potofu, kuamini kuwa kila jambo lina upigaji, jambo ambalo halikuakisi uhalisia. Hata kama kulikua na viashiria vya upigaji, si yangefanyika mabadiliko ya watendaji lakini mradi ukaendelea? Hii pia inagusa na mradi wa NLG kule Lindi ambao umesuasua mradi mkubwa kabisa, lakini pia imehusisha miradi ya Gesi kule Mtwara Makampuni kuondoka.
Ukubwa wa meli means high volume of cargo na hichi ndicho biashara ya bandari inataka kwamba volume kubwa ya mzigo inapita na Wana uwezo wa ku clear mzigo mkubwa kwa ufanisi na haraka.Bandari ya Dar es salaam imeendelea kuzivutia”
Sasa Mimi nauliza, bandari inahusikaje na Idadi ya magari na ukubwa wa meli?
Ni kwamba watu wameagiza magari mengi, Hakuna credit ya bandari wa siasa za Kifala
Magari hayawekwi kwenye containers lakini kwa ukubwa wa meli hii hata meli zingine za mizigo ya kwenye containers zinaweza leta meli zao Dar na mzigo ukawa cleared Dar ,ndio logic hapoLeo hii habari haizungumzii ukubwa wa meli wala idadi ya makontena, inazungumzia idadi ya magari,
Ni rekodi mbili tofauti...
Umaskini na gharama za kodi ziko juu ,Bongo gari ni anasa eti wanalinda mazingira kwa sababu sehemu kubwa magari yanayonunuliwa ni used.65% ya magari yanaenda nchi nyingine ! -
sisi kwetu huku shida nini gharama za kodi au uchumi wakati?