Dah! Unachekesha sana ndugu! Kwanza, nilichoandika ni hiki:Kabla ya kuzungumza fanya uchunguzi kwanza mkuu...
Kwa taarifa yako kama unamfahamu bilionea Jakob Juma wa kenya alitekwa na kuuawa mwaka 2016.
Marekani na ulaya matukio kama haya nanatokea sana. Hebu fuatilia matukio ya kutekwa hawa matajiri
BOBBY GREENLEASE
VIRGINIA PIPER
JOHN PAUL GETTY III
ALDO MORO na wengine wengi.
Umeona sasa?! Nimeuluzi richest person kwenye nchi husika! Nimeulizia Forbe's Billionnaire na sio wafanyabiashara ambao wamewahi kuwa kutekwa!Nitajie nchi moja tu, yoyote ile ambayo tajiri wake mkubwa kuliko wote aliwahi kutekwa na saa 24 kupita bila vyombo vya dola kuwa na clue!
Unaweza usiwe unatetea uhalifu lakini ukawa unatetea mfumo!! Aidha, unaweza usiwe wa kuvaa gwanda wala nguo za kijani lakini ukawa mtetezi ama wa serikali au mfumo!Halafu hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kutetea uhalifu...mimi sivai gwanda wala nguo za kijani mkuu.
Mimi ni mtanzania mzalendo nayefikiria kabla ya kuongea nmsilishwi na mtu najilisha.
Tena basi, hivi sasa Tanzania kuna tafsiri mpya ya uzalendo! Uzalendo si tena suala la kuipenda nchi yako bali suala la kuipenda na kuitetea kwa nguvu zote serikali yako! Tafsiri yetu mpya ni kwamba, uzalendo ni kutetea mfumo! Jambo la ziada! Mdogo wangu kabisa ambae ni tumbo moja! Huyu haipendi CCM hata nukta lakini humwambii lolote kuhusu Magu! Jambo lolote linaoelekea ku-downgrade utawala au mfumo wa Magu au Magu mwenyewe; mdogo wangu huyu atakuwa against nalo hata kama hoja hana!
Khaa! Kumbe unataka niwalaumu SUMATRA, TRA au Tume ya Haki za Binadamu kwa suala la kutekwa Mo na mamlaka kutokuwa na taarifa zozote hata baada ya saa 30 kupita?! Kama umenisoma vizuri, nimehusisha suala zima la mfumo wa ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya dola vyenyewe! Eneo husika ni high profile area wanakoishi high profile figures!Sasa unaoolaumu vyombo vya usalama kwa uzembe una maana gani?
Mkuu, unafahamu ilipo Colosseum?!
Kutokana na mazingira ya pale mtu angetarajia hata response time iwe ndani ya muda mfupi sana kwa sababu, pale walipo sio mbali sana na vituo vikubwa vifuatavyo: Oysterbay na Salendar Bridge! Si hivyo tu, kwa namna eneo lenyewe lilivyo, mtu angetarajia hata askari wa patrol wapo wa kutosha na sina shaka hata kidogo kwamba wapo wa kutosha sana!
Sasa ikiwa hadi sasa hakuna hata clue ya aina yoyote basi ina maana mfumo wa usalama upo duni! Na kama upo duni pande za Oysterbay, tena Oysterbay yenyewe along Haile Selassie, mtaa mkubwa kabisa Oyersterbay, vipi kuhusu mfumo wa kiusalama huku kwa Mtogole? NI nani wa kulaumiwa?
.Ndiyo nakumbuka yote hayo! Hivi kabisa unataka kulinganisha magaidi ambao wapo tayari kufa kazini na kidnapers ambao wanatarajia ujira baada ya kukamilisha kazi yao? Seriously?! Unalinganisha Magaidi walioingia sehemu kuua na wale walioenda sehemu kuteka ili hatimae watoroke?! Lakini yote kwa yote, pale Westgate Magaidi waliingia na kuweka kambi ndani kwa sababu tayari walishajiandaa kufa na hivyo hapakuwa na suala la manhunt! Hali hiyo ni tofauti kabisa na hili la Mo!Unakumbuka tukio la westgate attack?
Mamia ya watu waliuawa na watu kama watatu hivi...serikali ilituma polisi, wanajeshi, mpaka makomandooo lakini hawakukamata hata mhusika mmoja
Kuna kipi cha maana ulichosema cha kukufanya uhoji "kama sijui vizuri" niulize?! Kipi cha kujua vizuri hapo? Hilo la Westgate ambao lilikuwa linarushwa live au hilo la akina Mikel Obi?Kama hujui ni vizuri ukanyamaza kimya kuliko kuleta hisia zako kwenye mambo ya uhalisia.
Haijalishi ametekwa kwa sababu gani (kwa hoja yako kwamba kuna mengi tusiyoyajua)! Muhimu ni uwezo wa vyombo vya usalama kukabiliana na matukio kama haya! Saa 30 zimeshapita na kwa maana nyingine, kwa muda huo watekaji wameweza kufanya chochote walichokusudia! Chochote hicho kinaweza kuwa kumuua (God forbid), kuvuka nae boda hadi nje ya mipaka yetu, na kumfanyia lingine lolote lile watakalo!Mfanyabiashara mkubwa kama Mo kutekwa sio jambo la kitoto. K7na mengi tusiyojajua its better kuwa kimyaaa. Achia vyombo vya usalama kazi yao.
Hizo ni siasa za Bible na Quran ambazo zinashindwa kuwalinda hata Masheikh, Masharifu, Mapadri, Maaskofu, Maparoko, na siku hizi nasikia kuna mitume!!! Wote hao wanategemea ulinzi wa polisi na wala sio ulinzi wa maombi au dua!Kikumbwa ni kumuombea huko aliko atoke salama.
ASANTE
ASANTE!