Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Nimemuelewa sana Mambosasa anajaribu kumuweka pembeni kabisa Bashite anajaribu kusisitiza watu wamtafute yeye kwa taarifa na siyo Bashite na anasisitiza kuwa yeye ndiye anapata taarifa kutoka vyanzo mbalimbali hivyo ndiyo wa kuulizwa
 
Hawa siku ya kwanza alfajiri hawakufanya kazi zaidi ya kwenda kuweka utepe kwenye gari ya Mo na kumhoji yule Dereva wa uber mi nilidhani wangetoa zile chopa zao kuzunguka mji muda huo huo walipopata taharifa wao ndio kwanza wanakamata watu na kutangaza tumefunga mipaka kweli? kila siku kutueleza tuu vitu ambavyo havina logic kabisa na kuendelea kufanya kazi kizamani wakati mbinu za matukio ya kihalifu zikibadilika kila kukicha...
 
Bado tuna changamoto kama wageni wanakuja nchini na kumiliki silaha au wameingia Nazo hatujui ni veeepe.

Tuwaachie polisi wafanye kazi yao vizuri.
Umejuaje ni wageni .Tanzania aina watu weupe !!?? Tusubiri kwanza wakamatwe ndio tuanze kujadili
 
Hivi kwanza ni kwanini Polisi wame-conclude kwamba tukio limefanywa na raia wa kigeni..? Halafu kama hizo gari zimenaswa kwenye cctv, wameshindwa kuzisambaza picha in case kuna raia anaweza kuyatambua..?
Ndiyo maana kuna jamaa kasema hapo juu they are so stupid!
 
Wazee wenye hekima walipata kuandika "UTU BUSARA, UJINGA HASARA!" hawakukomea hapo wengine walipata kunena "UKIONA ZINDUNA, AMBARI ZAKARIBIA"
Basi na tumuombe sana Maulana hiki kikombe kituepuke. Tumuombee ndugu yetu Mo awe salama na abaki salama kutoka katika hiyo mikono isiyojulikana. Tuwaombee na wengine ambao pia ni wahanga katika matendo ovu hayo. Kuna maswali mengi kuliko majawabu lakini nani anathubutu kuhoji? Nani anaweza kuthubutu kutoa maoni yasihusishwe na siasa ama kiki? Aaaah ni heri kuendelea kunyamaza tu kama walivyopata kusema wale wakongwe "HERI MIMI SIJASEMA!!".
Mungu ibarikiTanzania. Dumisha uhuru na umoja.
 
Iddi Amin alideal na akawatimua, the rest is history, tatizo la Nduli hakuwa smart iliback fire

Putin alideal na Oligarchs, akawaweka ndani, akaextract concensions, Putin alikuwa smart, ana kura ya Veto kwenye baraza la Usalama, Ana Gesi inayotegemewa Ulaya ana Jeshi lenye Silaha za Nyukilia, Putin akafanikiwa

Mtoto wa Mfalme wa Saudia naye hakuwa nyuma, akadeal na wafanyabiashara wakubwa, akataka wampe share kwenye makampuni yao, akataka wailipe serikali ya Saudia pesa kwa madai ya kukwepa kodi, Mtoto wa mfalme hakuwaweka Jela hawa watu bali aliwaweka kwenye Five star hotels ila akalimit uhuru wao. Mtoto wa mfalme aliweza haya kwa sababu ana Mafuta, analindwa na Marekani n.k
 
Umejuaje ni wageni .Tanzania aina watu weupe !!?? Tusubiri kwanza wakamatwe ndio tuanze kujadili
Tusijitoe akili hiyo.
Hiyo sio kauli yangu ni kauli ya awali ya Jeshi la polisi kupitia Mambosasa na pia mkuu wa Mkoa .
Siwezi kunukuu wapita njia tu wasio rasmi.
Kwa hiyo tuwaulize wao kuwa walijuaje ?

Lakini pia tukio lolote la kihalifu linaweza kufanywa na mhalifu yeyote bila kujali rangi au jinsia. Mzungu anaweza akatumika kufanya uhalifu kama alivyo mwafrika tatizo ni kuwa sisi tumepuuza ulinzi shirikishi ndio maana wageni wanaweza wakaka popote bila kujulikana na kuwa na kumbukumbu zao mpaka pale wanapojihusisha na siasa hasa wakiwa ni wapinzani ndipo utasikia wanafuatiliwa uraia wao.
 
Habari nzito kama hii,abgekuwa nani ndo ingekuwa nyepesi?

Zakaria taarifa yake ilitolewa na polisi?

Ya Roma mkatoliki ilitolewa na Polisi?

Ya Masoud kipanya ilitolewa na Polisi?

Ya Ben saa nane ilitolewa na polisi?
Ya Tundu Lissu ilitolewa na polisi?

Ya Hussein Bashe na Msukuma Dodoma ilitolewa na Polisi???

Nguvu ya social networks ni kubwa sana,kama kila habari ingesubiriwa kutolewa na polisi,hasa habari kama hizi,basi yote hayo hapo juu,kamwe tusingeweza kuyajua!!!
Ilipofikia tusaidiwe tu na wenzetu wa nchi za nje walioendelea katika matukio aina hii ili wahusika wakome na kuchukuliwa hatua stahiki maana mficha maradhi... ama tusipoziba ufa... Hakuna hata mmoja atakayeishi milele, na tusome sana maandiko, dua na maombezi kwa wingi.
Hii ni Tanzania yetu sote kwa pamoja tunapaswa kuilinda amani na umoja wetu. Mengi yanaumiza na kukwaza heri kunyamaza tu. YATAPITA!
 
Hii nchi ishafananishwa na nchi ya wajinga tena watu wasio na akili ndio wamepewa madaraka makubwa kuongoza wenye akili.

Polisi wanasema tutoe ushirikiano kwa lipi labda?

1. Wametoa plate namba za magari wanayoyahisi?
2. Wametoa cctv footage kuomba msaada wa raia?
3. Hawana teknolojia ya satelite kufatilia mwenendo wa gari ilimbeba mo?
4. Hawana picha hata rangi ya gari inayohusishwa?
5. Hao wazungu wakoje? Nchi hii ina idadi kubwa ya wazungu kushindwa kuwatambua?
6. Waliomteka saa roma mpaka leo walishapatikana baada ya makonda kutoa mda je makonda alishawai kuhojiwa?

7. Hiyo risasi na ganda lake hazina usajili kujua ni nani kamilikishwa

Huo ni msaada gani wakati mnasema jeshi la kisasa au ni jeshi la kisiasa?

Bila shaka naamini wahusika ni serikali yenyewe wananchi tunazugwa tu
 
Back
Top Bottom