Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Hii nchi ishafananishwa na nchi ya wajinga tena watu wasio na akili ndio wamepewa madaraka makubwa kuongoza wenye akili.

Polisi wanasema tutoe ushirikiano kwa lipi labda?

1. Wametoa plate namba za magari wanayoyahisi?
2. Wametoa cctv footage kuomba msaada wa raia?
3. Hawana teknolojia ya satelite kufatilia mwenendo wa gari ilimbeba mo?
4. Hawana picha hata rangi ya gari inayohusishwa?
5. Hao wazungu wakoje? Nchi hii ina idadi kubwa ya wazungu kushindwa kuwatambua?
6. Waliomteka saa roma mpaka leo walishapatikana baada ya makonda kutoa mda je makonda alishawai kuhojiwa?

7. Hiyo risasi na ganda lake hazina usajili kujua ni nani kamilikishwa

Huo ni msaada gani wakati mnasema jeshi la kisasa au ni jeshi la kisiasa?

Bila shaka naamini wahusika ni serikali yenyewe wananchi tunazugwa tu
ishu ya kutafuta billionare haijawahi kuwa rahisi kama unavyo fikiria, isitoshe watu wameacha vitu vyte vya kum trace kwa simu na gari lake mkuu
 
ishu ya kutafuta billionare haijawahi kuwa rahisi kama unavyo fikiria, isitoshe watu wameacha vitu vyte vya kum trace kwa simu na gari lake mkuu
Tz hakuna issue ilishakua nyepesi....hao wengine wakina Ben Sa nane..kwani wamepatikana au nae ni billionaire....?
 
Ma-conder alisema mo atapatikana hv karibuni.. Hata kwa roma alisema hivyo ikawa kweli. Mpeni muda
 
Soko la mbaazi limeua sana uchumi wa wakulima hasa wa kwetu Ruvuma.
Kwa sasa
Gunia la mahindi linauzwa Tsh 20,000/
Dumla ya Mbaazi ilikuwa inauzwa Tsh 12,000/-
Hivyo Gunia la mbaazi liliuzwa zaidi ya Tsh 500,000/-
Kama ni ukweli Manji ndiye aliyekuwa ananunua Mbaazi basi jinsi alivyoshughulikiwa wakati ule ameathiri sana kipato cha wakulima wa kusini mwa Tanzania.
Leo Manji yupo huru, ina maana hakuwa na hatia.
Lakini wakulima wamekosa soko la mazao yao.
Hapo nani kapata hasara ?
Naiomba Serikali inapo washughurikia hawa matajiri wanao changia uchumi wa wa wananchi basi iwa shughulikie kwa STAHA.
Soko la mbaazi lilianza kuturudisha vijijini sisi tunao kwepa umasikini na kukimbilia mjini.
Tulianzisha mashamba vijijini, tukainua JEMBE, tena la mkono na tukanufaika.
Leo ni kilio kila mahali. Mbaazi inaozea mashambani, vijana wanakuja tena mjini kufafuta fulsa.
Jamani tunapo washugulikia hawa matajiri, basi tuwashughulike kwa staha.
Leo Manji yupo huru ila wakulima ndio wapo hoi.
Wakulima ndio wapo Jela Bosi yupo uraiani.
Jamani tunapo washughulikia hawa matajiri basi tuwashughulikie kwa staha.
Matajiri akina Manji, Bakhresa, Mengi, MO, Rostam Azizi na wengineo.
Naomba Radhi kama nimekosea mahali.
Usipokuwa makini unaweza kusema hivi "ni kama vile kuna mpango mkakati wa kutenganisha MATABAKA baina ya MATAJIRI, MASKINI, WATAWALA na WATAWALIWA.
NDIPO WALALA HAI NA WALALAHOI KILA MMOJA ATATAMBUA NAFASI YAKE
 
JAMAA KASEMA WALIOMTEKA NI WAZUNGU...... HAHAHAHAAHA.
IKO SIKU TUTAAMBIWA WALIOMTEKA KINGU NI WAGOGO!
 
wathungu weuthi wa MAMBISASA
Kwa hiyo ndani ya nchi tuna vikundi vya kigaidi vya kizungu ?
na wazuia mikutano a k a wapiga mabomu wameshindwa kuwabaini ?
Kama ni ushirikiano kwa nini hawakuwahi kumhoji ROMA juu ya waliomteka Roma na kama walimhoji mbona wazee wa media hawakuwahi kutujuza hatua za kuwasaka ?
MAGAIDI WANAOJIITA WATEULE.
 
Nimesoma soma articles za mauaji mbalimbali na katika kesi hata kama CCTV footage ipo askari kuileta kwa raia hua ni last resort ambapo hua wanaamua kufanya open investigation.

Kesi za abduction/ kidnapping hua zinafanyiwa sana mtindo huu kwakua abductors tupo nao mitaani. Mfano katika kesi ya Rostov Ripper Askari waliprofile wanahisije mhusika wao atakavyokua kutokana na matukio yalivyoonekana.
Same kwa kesi ya BTK, na watu walitoa tips, ingawa nyingi ni za hovyo il za msaada zinakuepo.

Kwa hizo articles nilizosoma zinasema kwamba, mtu aliyetekwa hua na window of opportunity la kumpata akiwa hai. Kadri muda unavyoenda dirisha linazidi kutanuka na inaanza kua ni kuhisi zaidi kuliko kuongozwa na facts. Mfano kwa sasa hivi askari wanaweza kua na theory hata mia za wapi watekaji watakua wameelekea, ila lingekua jeshi la kisasa ilibidi wajitahidi dirisha lisitanuke zaidi.

Pia ninachoamini ni kwamba kama waliomteka ni pros na wanachohitaji ni ransom watasema ila kama siyo pros wanaweza kureact savagely kwa namna serikali na nchi ilivyolipokea hili swala.

Nchi nyingi hua hazinegotiate na kidnappers, simply kwakua mkiwapa leo ransom kesho watakuja kumteka Samata, wakifanikiwa kila mtekaji atajua hili ni shamba la bibi. Sijui nchi yetu sera yake juu ya negotiation ikoje.

Ila askari wana eneo lao la kulaumiwa katika hili.
 
hayo ni mambo ya bussiness.
Mambo ya kuzungukana mbuyu.
Wale waliowateka akina roma ni mambo ya siasa.ujue utajiri na masuala ya biashara yana mambo mengi nyuma ya pazia.kama wanavyosema polisi watekaji ni wazungu.inawezekana ni kutofautiana katika mambo ya biashara.
 
Dah tunaletewa movie nyingine
.sijui itakuwa na part 2?
.sijui itachezwa kwa ustadi au itafanana na zile nyingine?
.sijui inataka kumpa kiki nani ?

Wakati utasema...stay tuned....!!!!

Nonsense unadhani watu wote ni wajinga? Nyie ndie wachezeshaji wa movies na huenda mkahusika ili kuchafua nchi
 
Mzungu wageni wawili ni kauli ziachazo ushahidi fikirishi,ccctv hawataki kuonyesha,maganda ya risasi je no ngapi Maana maganda tu wapewa Mossad au FBI hata yale ya lissu washapata muhusika kupitia no za maganda.Criminals yeyote lzm aache ushahidi wa kuanzia, ukipata maganda tu ushampata mwizi wako Kwa technology za kisasa
yah na hafanyi bahati kwa mbaya et ni mbinu flani ivi nzuri sana ktk kutuliza watu kwa namna ambayo hawatajua

izo kauli zao znaziirisha wazi kabisa wameusika
 
Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..

Mwenye habari kamili atujuze.

======

UPDATES:

Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.

RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini

UPDATE 1:

Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji

UPDATE 2:

RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

UPDATE 3:

RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji

UPDATE 4: 1100HRS
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekanusha taarifa za kupatikana kwa mfanyabishara Mohammed Dewji, na kwamba taarifa zilizosambaa kuwa amepatikana sio sahihi.

RC Makonda ametoa onyo kali kwa yeyote atakayeibuka na kuanza kusambaza taarifa za uongo kuhusiana na tukio hili au kuligeuza na kulifanya mtaji wa kisiasa.
View attachment 894040
View attachment 894102

MFAHAMU MOHAMMED GULAM ABBAS DEWJI "MO"

Mohammed Dewji ‘MO’ alizaliwa tarehe 8/05/1975 , mjini Singida kata ya Ipembe. Ni kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mo alizaliwa salama, kwani mama yake mzazi alijifungua akiwa nyumbani lakini alisaidiwa na nesi na daktari. Ni mtoto wa pili wa Mzee Gulam Dewji katika watoto sita wa familia hiyo. Ana dada mmoja Sabera na wadogo zake Ali, Hassan, Hussein na Fatema.

Baada ya kufikisha umri wa miaka mitano, alihama na kwenda mkoa wa Arusha kwa ajili ya elimu ya shule ya msingi. Aliishi Arusha na kusoma katika Shule ya msingi ya Arusha hadi mwaka 1986 alipohitimu elimu ya msingi.

Mwaka 1987 alihamia Dar es Salaam kwa ajili ya masomo ya sekondari na alijiunga na shule ya kimataifa ya Tanganyika (IST), hapo Mo alimaliza elimu yake ya Sekondari mwaka 1992. Na huu ndio ukawa mwisho wake wa kusoma nchini Tanzania .

Mwaka 1992 alienda kuongeza elimu mara hii akisafiri kwenda nje ya nchi kutafuta elimu na kufanikiwa kuingia katika Shule ya SaddleBrooke High School ya Marekani. Akiwa hapo ndipo Mo alipoanza kuonyesha dalili za kwanza za kuwa na sifa za uongozi pale aliposhika nafasi ya kuwa Rais wa wanafunzi wa shule ya SaddleBrooke. Kushika nafasi kama hiyo katika nchi ngeni lilikuwa ni jambo la kujivunia na heshima kubwa kwa familia na pia Watanzania kwa ujumla. Pamoja na kuwa na nafasi ya uongozi akiwa shuleni Marekani, Mo alipigiwa kura hapo shuleni ya kuwa kati ya wanafunzi waliofanya vizuri au tunaweza tukasema wenye vipaji( Most Accomplished student) na upande wa wanawake aliyepigiwa kura hapo mwaka huu alikuwa ni mchezaji maarufu wa tenisi duniani wakati ule Jeniffer Capriati.
View attachment 894268
Alipomaliza elimu yake hapo Saddle Brooke , Mo alipata nafasi ya kujiunga na moja kati ya vyuo vikuu bora duniani, GeorgeTown University iliyokuwa jijini Washington D.C, Marekani. Alisomea mambo ya biashara ya kimataifa na fedha, huku akichukua Theolojia kama somo la ziada.

Katika kipindi hicho cha masomo katika chuo cha GeorgeTown ndipo Mo alipoanza kubadilika kimaisha na kubadili mtazamo mzima wa kuangalia mambo ambayo binadamu anayafanya kila siku. Chuo hicho kinasifika kuwa na elimu bora na kimetoa viongozi na watu ambao wamefanikiwa sana katika maisha mfano Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, Mfalme Abdullah wa Jordan, Rais Gloria Arroyo wa ufilipino na hata wachezaji wa mpira wa kikapu maarufu nchini Marekani kama Allen Iverson na Patrick Ewing.

Alipohitimu masomo mwaka 1998 alirudi nyumbani Tanzania na moja kwa moja akaingia kwenye biashara za baba yake Mzee Gulam na akaanza na nafasi ya Mdhibiti mkuu wa Fedha katika kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL).

Jarida la Forbes la Marekani lilimtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group).“Dewji alibadilisha biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa na kuwa na viwanda vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea huyo Mtanzania .

“Alinunua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti,” inaongeza ripoti hiyo.

Metl ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.


Mbali na kuingia kwenye biashara, Mo alijiingiza kwenye michezo na kuanza kuifadhili Simba Sports Club ya Dar es Salaam. Huu ukawa mwanzo wa Watanzania kumuona Mo akiingia kwenye ulimwengu wa michezo wa Tanzania na hasa soka.

Ilipofika mwaka 2000, uchaguzi wa pili wa mfumo wa vyama vingi nchini uliwadia. Na Mo akajiingiza kwenye kinyanganyiro hicho akiwania kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Singida mjini. Katika kura za maoni Mo alimshinda Waziri wa Maji wa wakati huo Musa Nkhangaa kwa kura nyingi lakini kamati kuu ya CCM hawakumpitisha kugombea ubunge.

Kuna usemi mvumilivu hula mbivu, hivyo Mo akakubali na kuheshimu maamuzi ya chama na kumpigia kampeni mgombea wa chama na kuhakikisha wanashinda Uchaguzi wa 2000.

Pamoja na kushindwa kupata nafasi ya kugombea ubunge, Mo aliwasaidia wananchi wa Singida kwa hali na mali , huku pia akizidi kutoa mikataba minono ya udhamini kwa Simba iliyokuwa inazidi Milioni mia moja kwa mwaka.

Mwaka 2001 Mo aliamua kuachana na ukapera na kuamua kumuoa Saira, ambaye walijuana tokea enzi za shule. Kila kitu kinapangwa na Mungu kwani Mo alienda kusoma Marekani na kupoteza mawasiliano na Saira, lakini aliporudi kutoka Marekani ndipo wanandoa hao walianza kujuana zaidi na hatimaye kuamua kufunga ndoa ambapo wamejaliwa kuwa na watoto wawili, mmoja wa kike aitwaye Naila mwenye umri wa miaka sita na wa kiume anaitwa Abbas mwenye umri wa miaka mitatu.

Miaka miwili baada ya ndoa Mo alipanda cheo katika kampuni ya familia na kukabidhiwa rasmi kampuni nzima kama Mkurugenzi mkuu wa Mohammed Enterprises Limited (METL). Chini ya uongozi wake kampuni imepanda ngazi nyingi za mafanikio na kukua mara nane ya kiwango alichokikuta kuanzia pale alipoanza kufanya kazi, amewekeza kwenye sekta tofauti kama Kilimo, Fedha, Uzalishaji na Usambazaji wa bidhaa.

Takwimu zinaonyesha kampuni za Mo zinachangia pato la ndani la taifa kwa asilimia mbili na zinaajiri zaidi ya watu 20,000.

Mwaka 2005 ulikuwa mwaka wa uchaguzi na MO akachukua fomu tena za kuwania ubunge wa jimbo la Singida mjini. Kwa mara nyingine aliibuka kidedea katika kura za maoni akipitishwa na kamati kuu ya CCM kuwa mgombea na baada ya hapo akawabwaga wapinzani wake katika uchaguzi kwa kuchaguliwa kwa zaidi ya asilimia tisini ya kura zote zilizopigwa.

Tarehe 29 /12/2005 Mohammed Dewji ‘Mo’ aliapishwa kuwa Mbunge wa Singida mjini, na kuwa mwakilishi rasmi wa kero za wananchi wa Singida mjini bungeni.

2015 alitangaza kutogombea tena Ubunge jimboni humo wakati wa Mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida, mkutano uliofanyika katika viwanja vya People's Club.

Michezo na Mo hawakai mbali mbali. Rais Kikwete alikuja na ari mpya na kuwafanya Watanzania kupenda michezo na hasa timu yao ya taifa ya soka, Taifa Stars. Ili kufanikisha na kuleta maendeleo ya Stars kamati maalumu ya ushindi iliundwa huku Mo akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wake. Katika kipindi chake Taifa Stars wamebadilika kutoka kuwa kichwa cha mwendawazimu na kuwa timu inayoheshimika barani Afrika ikitoa sare na vigogo wa soka kama Cameroon na Senegal .

Pia chini ya uenyekiti wake Taifa Stars imepata kushiriki michuano mikubwa barani Afrika ya CHAN yaliyofanyika nchini Ivory Coast .

Mwaka 2007 kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa Chama (CCM) na Mo alijitosa na kuwania kugombea nafasi ya mjumbe wa Halmashauri ya taifa (NEC) na akafanikiwa kushinda kwa kupata kura za kutosha na kuweza kufanikisha azma yake hiyo.


Hii ni historia fupi ya Mhe. Mohammed Dewji ( Mbunge, Mjumbe wa Halmashauri ya Taifa (NEC) na mkurugenzi wa makampuni ya Mohammed Enterprises) ambaye anaendelea kusaidia jimbo na taifa lake kwa hali na mali pale anapokuwa na uwezo na nafasi ya kufanya hivyo.
tuanze na kauli tata za bashiteView attachment Ukawa Washington posted a video to his timeline. (3).mp4View attachment Ukawa Washington posted a video to his timeline. (2).mp4
 

Attachments

Back
Top Bottom