Kumbuka kuna raia wako vizuri kwenye crime and investigation kuliko hata askari, penye wengi hapaharibiki kitu,Ukiwaambia raia watoe ushirikiano bila kuwapa ushirikiano ni kuwadhiaki.
Nimesoma soma articles za mauaji mbalimbali na katika kesi hata kama CCTV footage ipo askari kuileta kwa raia hua ni last resort ambapo hua wanaamua kufanya open investigation.
Kesi za abduction/ kidnapping hua zinafanyiwa sana mtindo huu kwakua abductors tupo nao mitaani. Mfano katika kesi ya Rostov Ripper Askari waliprofile wanahisije mhusika wao atakavyokua kutokana na matukio yalivyoonekana.
Same kwa kesi ya BTK, na watu walitoa tips, ingawa nyingi ni za hovyo il za msaada zinakuepo.
Kwa hizo articles nilizosoma zinasema kwamba, mtu aliyetekwa hua na window of opportunity la kumpata akiwa hai. Kadri muda unavyoenda dirisha linazidi kutanuka na inaanza kua ni kuhisi zaidi kuliko kuongozwa na facts. Mfano kwa sasa hivi askari wanaweza kua na theory hata mia za wapi watekaji watakua wameelekea, ila lingekua jeshi la kisasa ilibidi wajitahidi dirisha lisitanuke zaidi.
Pia ninachoamini ni kwamba kama waliomteka ni pros na wanachohitaji ni ransom watasema ila kama siyo pros wanaweza kureact savagely kwa namna serikali na nchi ilivyolipokea hili swala.
Nchi nyingi hua hazinegotiate na kidnappers, simply kwakua mkiwapa leo ransom kesho watakuja kumteka Samata, wakifanikiwa kila mtekaji atajua hili ni shamba la bibi. Sijui nchi yetu sera yake juu ya negotiation ikoje.
Ila askari wana eneo lao la kulaumiwa katika hili.