Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakilimaliza hili kwa weledi wa kutukuka tutahoji tena kwa nguvu sana, vipi kuhusu Azory na Saanane? Vipi kuhusu "wasiojulikana" waliomjeruhi vibaya TAML?Kutekwa kwa Mo Dewji kutakuwa na athari nyingi sana.
Muathirika wa kwanza ni jeshi letu la polisi.
Kama tulivyoona habari za Mo zimetikisa dunia nzima, na macho ya dunia yana sikiliza kujua jeshi letu la polisi litatumia weledi gani kumpata Mo na watekaji wake.
Kwa vile watekaji inasemekana ni wazungu, hapa si tena kazi ya virungu na kutoa " kipigo cha mbwa koko" , maana watekaji ni maproffessionals, na polisi inabidi waonyeshe u proffessionalism wa hali ya juu kutatua tatizo hili.
The world is watching.
Mkuu wanaojua cha kuongea wako idara gani hiyo?Hakuna lolote la maana wanalolizungumza zaidi ya kuongeza maswali tu, huyo Waziri bora akae kimya tu maana ndio wale wale tu wasiojua nini cha kuongea na kuanza kuropoka tu
Ninyi watu wa ajabu sana...! Makonda kazunguza kidogo mumtie kaa la moto mdomoni...huku mkitaka akae kimya vyombo vya usalama vifanye kazi yake na ili ushahidi usivurugike...hakuja kucha sawa sawa mnamtaka Mh. Lugola aseme..ili mpate cha kuzungumza kwa kebehi...what is wrong with you, 'people'!?Hata mimi mpaka sasa najiuluza swali hilo na sipati majibu.
Mbwiga umeumia sana!Kwa sababu unaleta umbuzi
Nitajie nchi moja tu, yoyote ile ambayo tajiri wake mkubwa kuliko wote aliwahi kutekwa na saa 24 kupita bila vyombo vya dola kuwa na clue!
Kwamba, eti "haijalishi huyo mtu ni maarufu au kama mimi" hiyo ni kujaribu ku-justify uozo uliopo kwenye mfumo wetu wa ulinzi na usalama! Endelea kujidanganya kwamba akina eti sie tupo sawa tu na akina Reginald Mengi na kwamba, utekwaji wa yeyote miongoni mwetu hiyo ni ishara mbaya! Ni kweli, ni ishara mbaya lakini anapotekwa mtu kama Mo Dewji, hiyo sio tu ni ishara mbata bali ni ishara mbaya zaidi na zaidi!
Sie wengine miaka kadhaa iliyopita tulishuhudia Mzee Reginald Mengi akipewa ulinzi wa polisi nyumbani kwake Oysterbay baada ya kutishiwa kuuawa! Kama unaamini wewe na Mzee Mengi ni sawa, basi nenda kwenye kituo cha karibu ukaripoti kwamba unatishiwa kifo na kisha wathibitishe kwamba kweli unatishiwa kifo halafu uone kama unapewa askari polisi wa kuja kukulinda hapo unapoishi!!!
Mtu kama mimi, nitaenda viwanja gani kama sio Tandale, Mwananyamala, Manzese, Temeke n.k! Huko haitashangaza nikitekwa kwa sababu mfumo wetu wa ulinzi haujafika kisawasawa hadi Uswahilini!!! Lakini inapotokea mtu anatekwa maeneo kama ya Colleseum na kupita 24 hours bila vyombo vya dola kuwa na clue, hapo akina sie hatutaacha kujiuliza ikiwa maeneo kama yale na mtu kama yule anaweza kutekwa na watekaji kutokomea kusikojulikana! Maeneo ambayo angalau yana mifumo mizuri ya mitaa ambayo ingewezesha kuwa na street cams; vipi akina sie tunaoishi Kwa Mtogole! Huku kwetu watu si wanaweza kuingia hadi na vifaru na wasionekane!!
Ikiwa maeneo kama yake hayana hata Patrol inayoweza ku-respond kwa haraka anapotekwa mtu kama Mo Dewji, vipi huku kwetu?Ikiwa Richest Person anaweza kutekwa na polisi wasiwe na clue hata baada ya saa 24 kupita huku tukifahamu wamewekeza nguvu zao zote katika kufanya msako! Vipi ninapotekwa mtu kama mimi ambae polisi haitaweza kutoa japo askari mmoja kutafuta nipo wapi!!!
Kwa wale wanaoamini katika siku ya huku, mimi na Mo Dewji ni sawa lakini ni sawa mbele ya mwenye kiti cha enzi lakini hatuna usawa wowote mbele ya viti vya akina Magu!!
No wonder tunapotekwa akina sie wala hakuna anayejishughulisha! Endelea kuhangaika ku-justify ujinga!
Na wala hawawezi kwenda huko manake wanaweza kufanya assumption kwamba police wangeweza ku-react mapema na hivyo kuweka vizuizi kwenye barabarani hususani ya Kilwa Roand na ile iendayo Kisarawe! Pale si karibu na bahari! Unaenda kufanya tukio huku speed boat ikiwa standby! Mkishapata mtu wenu, moja kwa moja mlipoegesha boti itakayowatoa kwenye eneo la tukio kwa haraka! Huko mbele za safari, unamtoa kwenye boti ambayo inaweza ku-catch attention unamwingiza kwenye mashua ya uvuvi yenye wavuvi fake!
Hapo mtaenda na "mzigo" wenu hadi Mombasa bila kokoro! Kinyume chake, mnaweza kutia nanga maji marefu huku wavuvi fake wakijifanya wapo bize na nyavu huku wenye mchezo wao wakifanya chochote na mateka wao hadi watakapohitimisha walichokusudia kufanya!
Huyo waziri asijesema Mo ameenda kutafita maisha!Hakuna lolote la maana wanalolizungumza zaidi ya kuongeza maswali tu, huyo Waziri bora akae kimya tu maana ndio wale wale tu wasiojua nini cha kuongea na kuanza kuropoka tu
Hiki ni kizazi cha kuhoji mkuu usijae upepo.Msaidie na kihelehele chako
Umevurugika!Mleta thread ana IQ ya mende..
Ok, Ngoja nikaangalieJAMANI MWENYE ACCESS NA MILLADI AYO BLOG AANGALIE, NASIKIA KM KALIPOTIWA KUPATIKANA, PLZZ CONFIRMUNI JMN
Wanashangaa nchi yenye amani na utulivu yanatokea hayoNajiuliza swali hili baada ya kuona vyombo vikubwa vya habari duniani vikiwemo BBC, CNN, Al jazira, Xiua na Reuters vikiripoti na kulifuatilia kwa karibu tukio hili la utekaji lililotokea nchini mwetu!
Na wala hawawezi kwenda huko manake wanaweza kufanya assumption kwamba police wangeweza ku-react mapema na hivyo kuweka vizuizi kwenye barabarani hususani ya Kilwa Roand na ile iendayo Kisarawe! Pale si karibu na bahari! Unaenda kufanya tukio huku speed boat ikiwa standby! Mkishapata mtu wenu, moja kwa moja mlipoegesha boti itakayowatoa kwenye eneo la tukio kwa haraka! Huko mbele za safari, unamtoa kwenye boti ambayo inaweza ku-catch attention unamwingiza kwenye mashua ya uvuvi yenye wavuvi fake!
Hapo mtaenda na "mzigo" wenu hadi Mombasa bila kokoro! Kinyume chake, mnaweza kutia nanga maji marefu huku wavuvi fake wakijifanya wapo bize na nyavu huku wenye mchezo wao wakifanya chochote na mateka wao hadi watakapohitimisha walichokusudia kufanya!
Na vile vibunduki sidhani hata kama huwa vina risasi. Unakuta hotel nzuri eti mlinzi analinda na kirungu.Hivi hawa walizni wa Hoteli huwa wanafanya kazi gani?
mapambo tu na vibunduki vyao
Kwa serikali ya awamu hii hakuna hata mmoja mwenye kufanya jambo kitaaluma zaidi ya mihemko inayochagizwa kwa kulinda maslahi binafsiMkuu wanaojua cha kuongea wako idara gani hiyo?