Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Wakilimaliza hili kwa weledi wa kutukuka tutahoji tena kwa nguvu sana, vipi kuhusu Azory na Saanane? Vipi kuhusu "wasiojulikana" waliomjeruhi vibaya TAML?
 
Hakuna lolote la maana wanalolizungumza zaidi ya kuongeza maswali tu, huyo Waziri bora akae kimya tu maana ndio wale wale tu wasiojua nini cha kuongea na kuanza kuropoka tu
Mkuu wanaojua cha kuongea wako idara gani hiyo?
 
Hata mimi mpaka sasa najiuluza swali hilo na sipati majibu.
Ninyi watu wa ajabu sana...! Makonda kazunguza kidogo mumtie kaa la moto mdomoni...huku mkitaka akae kimya vyombo vya usalama vifanye kazi yake na ili ushahidi usivurugike...hakuja kucha sawa sawa mnamtaka Mh. Lugola aseme..ili mpate cha kuzungumza kwa kebehi...what is wrong with you, 'people'!?
 

Mkuu, Ishu hapo ni MASLAHI. Utatafutwa kwa bidii kiasi gani kuendana na wanaokutafuta wana maslahi kiasi gani na wewe.

Unaweza kuwa Tajiri mkubwa au mtu Maarufu lakini uhusiano wako na wanaokuzunguka ni mbovu au wivu ama wanakuchukia tuu kwa sababu wanazojua wao. Hapo ukipotea watu watasema bora tuu apotee, wataendelea tuu na shughuli zao kama vile hakuna kilichotokea. Pamoja na mapesa uliyonayo, no one will give a sht about yr disappearance!
 


Kumtoroshea Baharini kwa speed boat kwenda nchi nyingine wanaoweza kufanya kitu kama hiki ni Internationally organized criminal groups au majasusi tu na si nje ya hapo. Akili yangu inakataa majambazi wa kawaida wa nchini kwetu kuemploy mbinu kama hizi! And of course lazima jamaa wametumia akili nyingi katika kusuka na kutekeleza uhalifu kama huu.
 
Hakuna lolote la maana wanalolizungumza zaidi ya kuongeza maswali tu, huyo Waziri bora akae kimya tu maana ndio wale wale tu wasiojua nini cha kuongea na kuanza kuropoka tu
Huyo waziri asijesema Mo ameenda kutafita maisha!
 
Watekaji sio maboya wale " ... fununu nilizozsikia ni kwamba walitupa simu ya mo ". kama walikuwa na akili ya kufanya hivyo " basi tu assume kuwa walikuwa na kifaa cha kumfanyia scanning ili waweze kuona kama amefungwa GPRS ... (yote hayo yange jiri endapo itakuwa mo alifungwa hicho kifaa )
 
Najiuliza swali hili baada ya kuona vyombo vikubwa vya habari duniani vikiwemo BBC, CNN, Al jazira, Xiua na Reuters vikiripoti na kulifuatilia kwa karibu tukio hili la utekaji lililotokea nchini mwetu!
Wanashangaa nchi yenye amani na utulivu yanatokea hayo
 

Chavda aliwahi kukimbia na speed boat hapa enzi za Mwinyi au Mkapa na akatokomea, Pia kuna kisa cha boat moja ikijulikana kama seaexpress au butterfly (hapa sikumbuki vizuri jina) jamaa walikuwa wanadaiwa kodi nyingi sana lakini siku moja waliipandisha boti yao pale posta kwa ajili ya matengenezo na walipoenda for sea trial jamaa wakatokomea na walipojaribu kufuatwa hawakuonekana taarifa zikatoka kwa polisi wa Kenya/Mombasa kuwa jamaa walishakatiza maeneo ya Somalia muda mrefu sana. Hili la MO najaribu hata mimi kulifikiria katika angle hiyo kama kweli wale ni watekaji wenye shida naye kweli lazima watakuwa wametumia njia hiyo ndio maana strategically lazima atekwe maeneo ya oysterbay ambapo fukwe ziko karibu na wao ni rahisi kupark speed boat yao yenye horse power za kutosha, ukiwa na boat yenye horse power za kutosha kutoboa hapo ukanda wa Somalia, Yemen ni kugusa tu.
 
Duh ila wahusika nao watabe sana

Waliokamatwa miguu inakoma huko walipo
 
Hivi hawa walizni wa Hoteli huwa wanafanya kazi gani?
mapambo tu na vibunduki vyao
Na vile vibunduki sidhani hata kama huwa vina risasi. Unakuta hotel nzuri eti mlinzi analinda na kirungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…