Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ndio umeona mbali..Dah tunaletewa movie nyingine
.sijui itakuwa na part 2?
.sijui itachezwa kwa ustadi au itafanana na zile nyingine?
.sijui inataka kumpa kiki nani ?
Wakati utasema...stay tuned....!!!!
haya kumekucha.. ngoja tuone.. watakavyojihusisha na tukio hili la MO maana tunavojua hili tukio halina tofauti na la ANTIPAS T LISSU. Sasa tuone ufatiliaji utakavyofanyika na hatimae tupate majibu kwa muda mfupi kuliko tunavotarajia.. japo kwa tukio la LISSU mpaka leo hiii hata hiyo NISSANI JEUPE halijapatikana hata ile taarifa ya camera kunyofolewa haijatolewa maelezo.Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..
Mwenye habari kamili atujuze.
======
UPDATES:
Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.
RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini
UPDATE 1:
Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji
UPDATE 2:
RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji
UPDATE 3:
RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji
Chanzo cha habri?Ameshapatikana eti
Una uhakika?Keshapatikana na wahalifu wako rupango... Heko za kipekee zimuendelee mkuu wa mkoa kijana na mahiri wa Dar na kamanda mambo sasa ... Dar iko salama
Ndio tusijesingiziwa sisi ...[emoji2][emoji2] Yanga tena duh!
Hapana inategemea na mtu...fuatilia maisha anayoishi Warren buffet au aliyokuwa akiishi Steve job utaona..ni wewe tu jinsi unavyojiweka na jamii..
Hao ndio wale watumwa wanadhani mzungu ndio mtakatifu na mweusi ndio haramu.Kwani wazungu hawawezi kumteka?
Utakuwa wewe ni mke wake.. sasa mnataniana na bwana yako.Mi naamini amejiteka kutafuta kiki!
Huwa taarifa yake ya mwanzo inapingana na atayoitoa baadae, ngoja tuone na tukio hili kauli atakayoitoa tenataarifa zinasema watekaji walifunika nyuzo zao, mambosasa na kikundi chake tayari wameshajua ni wazungu. wamejuaje?
Kumbuka Jamii yenyewe ndo hii hii yenye majambazi Na vibaka.. Kuishi vizuri Na Jamii yako hakumzuii MTU kukudhuru mkuu. Mo alitakiwa akumbuke yeye ni asset.Hapana inategemea na mtu...fuatilia maisha anayoishi Warren buffet au aliyokuwa akiishi Steve job utaona..ni wewe tu jinsi unavyojiweka na jamii..
Inawezekana kuna jamboMo Kapatikana. View attachment 894150