Hakuna hapo kuna mchezo unachezwa. Haiingii akilini kuwa ametekwa, huenda kuna mpango unafanywa juu ya mtu fulani, I'll ikitokea watu tujue aaah kawaida, mbona MO nae alitekwa!! Lakini hakuna siri chini ya jua kila kitu kitakuwa peupe muda sio mrefu. La tatu kwanini MO anaishi maisha ya aina hiyo? Hivi kweli yeye hajijui kuwa na Tycoon, au anazani kuishi hivyo ndio kutamfanya apendwe? Lazima aamue kuishi tofauti kabisa, tena tofauti sana. Haiwezekanj MO akashindwa kuwa na fitness Center kwenye kasri lake, ok hana. Basi haiwezekani akawa hana bodyguard anapotoka ndani ya viunga vya kasri lake, jamani MO ni nembo ya taiga letu.
Natoa angalizo kwa wanaofanya huu mchezo, wanaliangamiza taifa. Wasidhanie ni suala dogo, hakuna wawekezaji watakaokuja Tanzania kuwekeza na hata wakija watakuja vibaraka wao.
Ni nani aneapanga ujinga huu, na kwanini wanamchekea? Baba wa Taifa alisema, ukizoea kula nyama ya watu, hautaacha. Wamezoea kuwateka akina Ben Sanane, Dr Ulimboka na wengine kuwaua kabisa, sasa dhambi inatamalaki wameanza kutekena wenyewe kwa wenyewe. Amini nakuambia kila kitu kitakuwa wazi, huenda wamemtaka kwa kumtisha ili aisaidie kifedha jamii , taasisi au kikundi cha watu fulani itajulikana. Sitaki kwenda mbali sana, ila anaepanga huu mchezo, lazima akamatwe ashtakiwe na kufungwa. Labda tu kama kuna baraka ya Mungu. Acha tu niingie mtaani kutafuta riziki ya kila siku.