Tuendelee kuwa watulivu wakati vyombo husika vikiendelea
na zoezi la kumtafuta ''MO''
Ninachoshukuru ni kuona jinsi watanzania tunavyoendelea
kuwa wakomavu katika mambo haya maana sijaiona lugha
ya kusema ''kajiteka'' na hii ni faraja kubwa kwa taifa.
Kuna haja ya watu maarufu,kuwekewa
vifaa maalum mwilini kwa ajili
ya kufuatiliwa mahali alipo,ila iwe siri yake
na familia yake,hili lingesaidia kipindi kama hiki
kurahisisha upatikanaji wa mhusika.
Lakini pia ni wakati muafaka
kwa watu maarufu kuwa na walinzi
binafsi wanaowasindikiza katika
kutimiza majukumu yao,maana tunayoyaona
kwenye sinema watu maarufu wanatekwa
ili watekaji wapewe pesa nyingi yanaweza
kufika hata huku kwetu.