Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Hii Serikali imeshamfanyia kila mdau figisu.
Sasa Jiwe akikaa ofisini anawaza;
"Labda ni wakenya niliowachomea vifaranga vyao Moto......??"
"Au labda ni Barick wananihujumu....??"
"Au ni Sumaye niliyemnyang'anya shamba.....??"
"Hapana, itakuwa ni Mbowe maana yeye ndio nimemvurugia club nikaharibu na shamba....??"
"Au ni Lissu,maana huyu nae alikula risasi nyingiiii...??"
"Au Nape....??"
"Au Lema....??"
"Itakuwa Maalim Seif kwasababu naiua Cuf..??"
"Atakuwa nani huyuu.,..??"
"Au Manji...??"
"Rugemalila na Seth...???"
"Sijui itakuwa nani...???"
"Au wananchi tu wananihujumu...??"
"Ila ntalala nao mbeleee...!!"
Aseee nimecheka kwa sauti mpk watu wamenishangaa
 
Write your reply... Aiseeeee hili nalo ni suala la kujiuliza? KWELI.....nadhani unatania Mkuu, sababu zipo wazi SANA
 
Najiuliza swali hili baada ya kuona vyombo vikubwa vya habari duniani vikiwemo BBC, CNN, Al jazira, Xiua na Reuters vikiripoti na kulifuatilia kwa karibu tukio hili la utekaji lililotokea nchini mwetu!
Nchi ya amani,
Msamiati wa kizamani unaotumika sasa
 
Vyombo vya usalama vifanye kazi yake ipasavyo bila kuingiza siasa siasa kama ambavyo Mambosasa alisema Jana kuwa wale ni wageni (wazungu) wenye lengo la kuchafua taswira ya nchi, jambo ambalo alilizungumza kwa mihemko sana wakati bado uchunguzi ukiendelea yeye akaja na hitimisho kana kwamba uchunguzi umekamilika tayari
 
Kuna watu sijui ni ugumu wa maisha!!? Yaani we unamuona Mo ni sawa na wewe? Hili kweli linashangaza?? Ulitegemea Mo atekwe alafu habari iishie hapo kwenu Missenyi?

Mo ni international figure. Sasa ajabu iko wapi kuona BBC, CNN, n.k kwao inakuwa habari kubwa??

Inaelekea hata Diamond akipotea ghafla utakuja kuuliza maswali yako haya haya ya kilevi

Dah...nyie watu wengine kwa majibu bwana hamjambo
 
Back
Top Bottom