Chavda aliwahi kukimbia na speed boat hapa enzi za Mwinyi au Mkapa na akatokomea, Pia kuna kisa cha boat moja ikijulikana kama seaexpress au butterfly (hapa sikumbuki vizuri jina) jamaa walikuwa wanadaiwa kodi nyingi sana lakini siku moja waliipandisha boti yao pale posta kwa ajili ya matengenezo na walipoenda for sea trial jamaa wakatokomea na walipojaribu kufuatwa hawakuonekana taarifa zikatoka kwa polisi wa Kenya/Mombasa kuwa jamaa walishakatiza maeneo ya Somalia muda mrefu sana. Hili la MO najaribu hata mimi kulifikiria katika angle hiyo kama kweli wale ni watekaji wenye shida naye kweli lazima watakuwa wametumia njia hiyo ndio maana strategically lazima atekwe maeneo ya oysterbay ambapo fukwe ziko karibu na wao ni rahisi kupark speed boat yao yenye horse power za kutosha, ukiwa na boat yenye horse power za kutosha kutoboa hapo ukanda wa Somalia, Yemen ni kugusa tu.